Machapisho

Adult attachment: Unaangukia kundi lipi katika haya manne?

Picha
ZIMEFANYIKA tafiti nyingi mno kuchunguza asili ya matatizo mengi ya kitabia tunayokabiliana nayo kama jamii.  Hapa tunazungumzia tabia katika upana wake kwa maana ya vipengele vyake vitatu: 1) ufahamu na imani zilizojengeka na kufungamana na akili zetu, 2) mitazamo na nia (attitude) zetu kuhusu masuala, watu, na kadhalika, na 3) matendo yetu yanayoonekana kwa wengine ambayo kimsingi hutekeleza  mawili ya mwanzo kwa maana kilichojengeka akilini na mitizamo uliyonayo. Chukulia mfano wa tabia za ubaguzi wa kikabila, kidini au rangi. Tabia hii huanzia kwanza kabisa kwenye namna tunavyokuchukulia mambo kwa ujumla jumla na kuyahukumu kwa kutumia tunachokijua tayari kama short cut ya kuyaelewa mambo kwa wepesi (stereotype) . Uelewa huu unakolezwa na imani ya jumla kuwa kundi unalokuwa wewe ni bora na linastahili mema kuliko makundi mengine. Mfano dini yangu ni bora kuliko za wengine, na hivyo kila muumini wa dini yangu anastahili mema. Ni mkakati tu wa kisaikolojia wa kukufanya uji...

Sababu zipi hufanya tofauti za attachments kwa watoto?

KATIKA mfululizo wa makala haya, tumeeleza namna watoto tangu wanapozaliwa,wanavyoungamanishwa na mama zao kwa kihisia. Tulitumia neno attachment kuelezea mahusiano baina ya mama na mwanae, mahusiano ambayo kimsingi ndiyo huamua mtoto anakuwa na tabia gani huko mbeleni kama tutakavyoeleza. Vile vile, tulieleza namna tunavyoweza kubaini usalama wa kihisia walio nao watoto kwa kuangalia namna wanavyoitikia kuondoka kwa mama, na kadhalika wanavyoitikia kurudi kwa mama. Tafadhali fuatilia makala haya hapa , kabla hujaendelea zaidi. Katika makala haya, kwa ufupi, tutatazama sababu zinazochangia sana hisia hizo za usalama anazokuwa nazo mtoto. Tutazungumzia sababu tatu pekee: Ubora wa malezi ya mama, mazingira ya familia na maumbile ya mtoto mwenyewe. Ubora wa malezi ya mama Msomaji atakumbuka kuwa tumegusia kidogo wajibu wa mama katika kumfanya mwanae ajenge mahusiano naye. Kimsingi, tunapozungumzia ubora wa malezi ya mama, kwa mujibu wa magwiji wa masuala haya kama vile Belsky ...

Aina za 'Emotional attachments' kwa watoto wenye umri hadi miaka mitatu

Picha
TULIGUSIA namna mahusiano ya awali kabisa kati ya mtoto na mama yanavyojenga muunganiko wa hisia za usalama kati ya mama na mtoto. Soma utangulizi huo hapa. Tuliona kwamba mhusika mkuu wa attachment (muunganiko wa kihisia) anaokuwa nao mtoto, ni mama.  Kwa kweli ni sahihi kusema kwamba katika umri wa miaka miwili ya mwanzo, mtoto huwa na mradi endelevu wa ama kuwaamini watu au kuwatilia shaka. Na ni bahati mbaya kuwa haya yote hutokea mapama na katika umri mdogo ambao wazazi wengi hudhani watoto ni wadogo mno kuweza kuelewa yanayoendelea. Kwa ufupi, katika umri huu, wa miaka miwili, mama anaweza kabisa kufanya jaribio dogo la kujiridhisha ikiwa mwanae amejenga attachment naye au la. Watafiti wa mahusiano ya kihisia kati ya mama na mtoto wakiongozwa   na Anne Ainsworth, kwa kufanya tafiti za kutosha kwa vichanga (infants) wamewagawanya watoto katika makundi mawili makubwa ya kihisia: La kwanza ni watoto wanaojisikia salama kihisia (securely attached infants) na wat...

Attachment: How secured is your infant?

Picha
KAMA lipo hitaji kuu na la msingi kabisa kwa mwanadamu ni usalama. Kujisikia upo katika mazingira yenye usalama. Security . Leo hii wageni wengi wanaogopa kwenda Mogadishu shauri ya hisia za kukosekana usalama. Al Shabab wanatishia usalama wa watu. Kisaikolojia usalama ni zao la dhana inayoitwa kwa kimombo attachment ambayo ni muunganiko wa kihisia ambao mtu, aghalab mtoto, huutengeneza na mtu mwingine. Ni matarajio na imani za jumla anazokuwazo mtoto kuhusu wanaomzunguka.   Papalia na wenzake wanauona muunganiko huu kama uhusiano baina ya mtoto na mama, ambapo kila mmoja huchangia katika uhusiano huo. Ingawa zipo sababu nyingi zinazosababisha mahusiano haya ya kihisia, lakini watafiti wengi wanakubaliana kuwa mama ndiye mhusika mkuu. Tafiti zinaonesha kwamba muungamaniko huu wa kihisia ni msingi wa uwezo wa mtoto kuelewa na kuhusiana na watu wengine. Attachment humwezesha mtoto kuuelewa ulimwengu unaomzunguka na kumfanya ama auamini kuwa unaaminika na unabashirika n...