Adult attachment: Unaangukia kundi lipi katika haya manne?
ZIMEFANYIKA tafiti nyingi mno kuchunguza asili ya matatizo mengi ya kitabia tunayokabiliana nayo kama jamii. Hapa tunazungumzia tabia katika upana wake kwa maana ya vipengele vyake vitatu: 1) ufahamu na imani zilizojengeka na kufungamana na akili zetu, 2) mitazamo na nia (attitude) zetu kuhusu masuala, watu, na kadhalika, na 3) matendo yetu yanayoonekana kwa wengine ambayo kimsingi hutekeleza mawili ya mwanzo kwa maana kilichojengeka akilini na mitizamo uliyonayo. Chukulia mfano wa tabia za ubaguzi wa kikabila, kidini au rangi. Tabia hii huanzia kwanza kabisa kwenye namna tunavyokuchukulia mambo kwa ujumla jumla na kuyahukumu kwa kutumia tunachokijua tayari kama short cut ya kuyaelewa mambo kwa wepesi (stereotype) . Uelewa huu unakolezwa na imani ya jumla kuwa kundi unalokuwa wewe ni bora na linastahili mema kuliko makundi mengine. Mfano dini yangu ni bora kuliko za wengine, na hivyo kila muumini wa dini yangu anastahili mema. Ni mkakati tu wa kisaikolojia wa kukufanya uji...