Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti, 2017

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma

Picha
PICHA: Oxford Learning Kusoma kitu usichokielewa ni hasara. Mbali na kuongeza uwezekano wa ‘kupigwa chenga’ wakati wa mtihani, kutokuelewa kunaharibu dhima ya elimu. Mtu asiyeelewa kile alichojifunza, kwa mfano, hawezi kutumia maarifa aliyonayo kuleta tija kwa jamii.

Kinachofanya Wanafunzi Wasielewe Wanachokisoma

Picha
PICHA:  SciTech Daily Ujifunzaji (learning) ni mchakato wa kupata uzoefu mpya katika maeneo makubwa matatu. Kwanza, kubadili namna mtu anavyofikiri. Maarifa mapya huja na uzoefu mpya unaobadilisha uelewa wa mambo.

Elimu Isinoe Ufahamu Pekee, Itufanye Tuwe Binadamu Timamu Wanaojitambua

Picha
PICHA: EDUCATION / BUNKIE BILA shaka umewahi kukutana na mtu unayeamini ni msomi akifanya mambo usiyoyatarajia. Jambo hilo hilo lingefanywa na mtu asiyekwenda shule wala usingeshangaa. Lakini kwa kuwa anayefanya hivyo ni ‘msomi’  basi unakata tamaa na kuhoji, “Hivi huyu naye amesoma? Kama kusoma kwenyewe ndio huku, basi hakuna haja ya kusoma.”

Wanavyokufahamu Watu Ndivyo Ulivyo?

Picha
PICHA: NCC PE ‘Jamaa ana madharau sana!’ alilalamika Lazaro. ‘Nani?’ alihoji Msafiri. ‘Si Peter?’ Uso wa Msafiri ulionesha mshangao. Hakufikiri Peter anaweza kuwa na dharau kama Lazaro anavyodai. Msafiri anamfahamu Peter mwenye tabia nyingine kabisa. Kwake, Peter ni rafiki,  mtu wa watu asiye na neno na mtu. ‘Peter huyu huyu ninayemfahamu mimi?’ Msafiri aliwaza kimya kimya akikumbuka namna Peter alivyomsaidia hivi majuzi alipokuwa na shida ya fedha. Hakuna rafiki aliyemsaidia isipokuwa Peter. Hakupata kufikiri hata mara moja kwamba Peter angeweza kuwa dharau akaona aulize imekuwaje, ‘Kwa nini umefikiri hivyo Lazaro?’ ‘Jamaa ana kiburi sana aisee. Nimepishana nae mjini kati jamaa kama hanifahamu vile. Na kile ki Vitz chake yaani kama hanioni vile!’ ‘Labda hakukuona mkuu. Peter hayuko hivyo.’ ‘Hapana alikuwa ananiangalia kabisa. Kaudhi sana jamaa. Tangu awe na hicho kigari kabadilika mbaya. Kijiweni haji tena. Anajifanya yuko busy.’ Msafiri haamini a...

Nafasi ya Mzazi Katika Kukuza Vipaji vya Watoto

Picha
Jioni moja, mwanzoni mwa miaka ya tisini, nikiwa darasa la tatu, mama alikuja nyumbani na barua aliyoniambia ilikuwa yangu. Barua hiyo fupi iliyoanza na maneno, ‘Mpendwa mwanangu Christian,’ ilikuwa ndani ya bahasha yenye barua ya mama kutoka kwa baba yangu, ambaye kwa wakati huo alikuwa masomoni.

Unamsaidiaje Mtoto Asiyefanya Vyema Kimasomo?

Picha
PICHA: BBC News Kwa mzazi mwenye mtoto anayesoma shule, ni rahisi kuelewa inakuwaje pale unapokuwa na uhakika mwanao ana uwezo mzuri lakini matokeo anayoyapata shuleni hayalingani na uwezo wake. Kama mzazi unayejali unajaribu kufanya wajibu wako, unamsaidia kazi za shule, unamwekea mazingira mazuri yanayomhamasisha kujisomea akiwa nyumbani, unashirikiana na walimu wake, lakini bado matokeo yanakuwa kinyume.

Fikiria Yafuatayo Unapoomba Nafasi ya Kujiunga na Chuo Kikuu

Picha
  PICHA:  HuffPost Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imeviruhusu vyuo vikuu hapa nchini kuanza zoezi la kupokea maombi ya wanafunzi kwa mwaka wa masomo wa 2017/2018. Katika kufanikisha zoezi hilo, tume imewaelekeza wanafunzi wanaofikiri wana sifa za kujiunga na elimu ya juu, kutuma maombi yao kupitia vyuo husika tofauti na ilivyokuwa awali. Kabla ya utaratibu huu mpya, wanafunzi walituma maombi kupitia mfumo wa udahili wa pamoja uliokuwa ukiratibiwa na tume yenyewe.