Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba, 2014

Kuogopwa kwa wanawake wenye mafanikio na dhana ya kichwa cha familia

Picha
NILIPATA fursa ya kushiriki mjadala mmoja kwenye mtandao wa Facebook leo mchana. Mjadala wenyewe ulianzishwa na Samuel Sasali , ambaye kwa maoni yangu ana uwezo mkubwa wa kuchokoza mada zinazohusu maisha yetu ya kila siku. Hoja iliyokuwa mezani ililetwa kwa njia ya mchoro unaoonesha changamoto anazokabiliana nazo mwanamke anapofanikiwa kielimu. Kwamba kadri mwanamke anavyokwea ngazi ya mafanikio ya kielimu, ndivyo wanaume wanavyozidi kumkimbia.

Muhtasari na Hitimisho, 'Kanuni zinazoongoza mahusiano na migogoro ya wanandoa'

Picha
TANGU tulipoanza mfululizo wa makala za mahusiano , jambo kubwa nililojaribu kulionesha ni nafasi ya mahitaji ya hisia katika kuimarisha au kuvuruga mahusiano. Na msingi wa haya yote ni kusema kwamba mahusiano hayana miujiza. Mahusiano yanaongozwa na kanuni za kawaida sana ambazo ukifanikiwa kuzitambua na kuzitumia utapunguza kama sio kuondoa matatizo mengi. Kwa mhutasari, ningependa tuyapitie mambo makuu yaliyojitokeza katika mjadala wetu kwa kuyaweka katika makala moja inayojitegemea.

Umuhimu wa kutofautiana ili kujenga mahusiano imara

Picha
Kwa wale wafuatiliaji wenzangu wa tamthlia isiyopendwa na wengi, Isidingo the Need, mtakuwa mmeona mgogoro wa kimahusiano kati ya Rajesh Kumar na mkewe Priya. Wawili hawa wamejaliwa mtoto mmoja wa kike, Hiranya, ambaye si mtoto wa kuzaa wa Rajesh. Sasa ikafika mahali mwanaume huyu akatamani kuwa na mtoto ‘wa kumzaa mwenyewe’. Priya hayuko tayari kupata mtoto mwingine. Anadhani   kilicho muhimu kwa sasa ni kumlea mtoto wao na sio kuongeza majukumu ya malezi.

Mwaliko wa Mkutano wa Global Voices, Dar es Salaam, Novemba 1, 2014

Tunayo furaha kubwa kutangaza mkutano wa Global Voices unaotarajiwa kufanyika Dar es Salaam, Tanzania siku ya Jumapili, Novemba 2, 2014 kuanzia saa 6 mchana hadi saa 10 adhuhuri. Mkutano huo utafanyika kwenye Kituo cha Teknolojia na Mambo ya Jamii, KINU , washirika wa Global Voices Swahili hapa nchini.

"Ningerudia ujana tena, kipaumbele changu kingekuwa familia!"

Picha
Re-living my life ? " anauliza halafu anajijibu mwenyewe, "Ningebadili mtazamo wa tafsiri ya mafanikio. Mafanikio yangemaanisha ubora wa mahusiano yangu na familia yangu. Hivyo, ningewajibika zaidi kujenga na kuilea familia yangu kwa karibu. Ningetumia muda mwingi na wanangu na mke wangu. Ningepunguza ukali usio  na sababu kwa mke wangu na wanangu. Ningewafanya wanangu wajisikie kuwa na baba anayewaelewa na anayejua mahitaji yao. Ningepatikana zaidi. Ningemfanya mke wangu ajione ni kipaumbele cha maisha yangu.

Tunapambana na UKIMWI kwa kupambana na utu wa watu wanaoishi na VVU?

Picha
Hivi majuzi nilipata fursa ya kushiriki mradi unaojaribu kudhibiti maambukizi ya virusi vinavyosababisha UKIMWI kwa kuwasaidia watu wanaoishi na virusi hivyo kukabiliana na hali hiyo ambayo kwa hakika hugeuza kabisa maisha yao. Fursa hii adhimu ilinifungua macho kuona kile ambacho sikuwahi kukiona kwa muda mrefu. Nisingependa kutoa takwimu za tafiti za majumuisho zinazojaribu kuonesha hali ikoje kwa ujumla bali takwimu za hali halisi niliyoiona kwa macho yangu.

Siku ya Blogu Oktoba 16: Shiriki Kujadili Dhana ya Kutokuwepo kwa Usawa

Picha
Tangu 2007, Siku ya Wajibu wa Blogu Duniani imekuwa ikitumika kuwaweka pamoja wanablogu kutoka duniani kote ili kujadili mada muhimu zinazokuwa zimewekwa mezani. Siku hiyo, wanablogu kwa pamoja, huwa utaratibu wa kuvamia anga la blogu kwa kuchapisha maelfu ya posti kuhusu masuala ya maji, mabadiliko ya tabia nchi, umasikini, chakula na nguvu ya pamoja. Kwa mara nyingine mwaka huu, Global Voices Online inayo fahari kuwa mshirika rasmi wa siku hiyo.

Chimbuko la wivu na athari zake katika mahusiano

Picha
Umewahi kuhisi unaachwa na mtu unayetarajia kumwoa au kuolewa nae? Umewahi kutamani kuwa na 'access' na simu au barua pepe ya mwenzi wako ili angalau ujisikie kutulia moyoni? Umewahi kujisikia vibaya mwenzi wako akizungumza na mtu mwingine hata kama hukuwa na ujasiri wa kumwambia? Umewahi kumchukia mtu na hata kupambana nae kwa siri au wazi sababu tu umehisi anahatarisha uhusiano wako? Kama lolote kati ya hilo linaelezea hali yako, basi makala haya yanakuhusu.

'Usawa wa kijinsia' unavyoweza kuharibu mahusiano

Picha
Wanawake wanatafuta haki ya kuwa sawa na wanaume. Na wamefanikiwa. Katika makala haya tunajaribu kuonesha hatari ya wanawake kudhani wanaweza kuwa sawa kijinsia na wanaume na bado waweze kuwa na mahusiano imara na wanaume. Ni salama zaidi kwa wanawake kuelewa kwamba usawa wa kijinsia haumaanishi kufanana kwa wanaume na wanawake. Ingawa ni kweli tunapigania usawa wa fursa, bado twapaswa kutambua haitawezekana wanaume wakageuka kuwa wanawake na wanawake kadhalika wakageuka kuwa wanaume.

Iweje waliotulia hawaolewi, aolewe huyu asiyetulia?

Picha
Si mara zote uhusiano wa ndoa ni matokeo ya upendo kama inavyotarajiwa. Yapo mahusiano mengi tu ya ndoa ambayo kimsingi ni arrangements za watu kujipatia mahitaji mengine kabisa yasiyohusiana na mapenzi. Katika makala haya, tunajaribu kuonesha kwamba si kila mwanamke aliyeolewa maana yake ni kuwa anafaa na kadhalika, si kila asiyeolewa maana yake ni kuwa hafai.

Msomaji anauliza, 'Nilipenda pesa zake, naweza sasa kumpenda mwenyewe?'

Picha
Wapo watu hujikuta wameingia kwenye mahusiano na watu wasiowapenda kwa sababu kadha wa kadha. Katika makala haya, tunajaribu kuonesha kwamba kisaikolojia, upo uwezekano mkubwa wa watu hao kuingia kwenye mapenzi ya dhati na wenzi hao ikiwa mambo kadhaa yatafanyika. Ni mambo gani hayo?