Mambo Yanayoweza Kumvutia Mwanamume kwa Mwenzi Wake -1
Swali hili huulizwa na karibu
wanawake wote wanaotamani kuwa na uhusiano wa kudumu na wanaume. Kwamba mambo
yepi hasa yanayoweza kumvutia mwanaume pale anapoanzisha uhusiano na mwanamke.
Ingawa zipo tofauti ndogo ndogo
miongoni mwa wanaume, kwa ujumla, uchambuzi wa tafiti mbalimbali za mahusiano
unabainisha mambo kadhaa yanayowaunganisha wanaume wengi kimahitaji. Tuyatazame
katika mfululizo wa makala hizi.
Kutambuliwa uwezo wake
Mwanaume anatamani kujisikia ni shujaa asiyeshindwa. Fahari ya mwanaume siku zote ni uwezo anaoamini anao unaomfanya mara nyingine awe tayari kufanya mambo yanayoweza kuhatarisha maisha yake kwa lengo tu kuthibitisha kuwa wanaweza. Ndio kusema kutambuliwa uwezo wake ni hitaji la msingi.
Kama unatamani mwanaume umpendaye aanze (aendelee) kuvutiwa na wewe, chukua hatua ya kubaini vitu vya pekee alivyonavyo na onesha kwa dhati kuwa unavitambua. Kwa kawaida kila mwanaume anayo maeneo yake anayoyaweza vizuri kuliko wengine.

Inawezekana ikawa ni uwezo fulani wa
kipekee ambao si wanaume wengi wanao. Huenda ni tabia fulani maalum ama ujuzi,
maarifa na sifa nyingine za kipekee unazojua anazo. Inawezekana ni uaminifu wa
muda, kujali familia yake, kuwahi nyumbani na kushiriki kazi za ndani,
ufuatiliaji wa mambo kwa karibu, bidii ya kazi, ucha Mungu na mengineyo kama
hayo. Chukua hatua ya kumfanya afahamu unauelewa uwezo alionao.
Katika mazingira yetu ya ki-Afrika,
wakati mwingine tunaogopa kuwatambua watu kwa sifa zao nzuri hata kama
tunazitambua sifa hizo. Wakati mwingine tunafikiri kile chema anachokifanya mtu
ni wajibu wake usiostahili kutambuliwa.
Hata haivyo, ni vyema kama mwanamke ujifunze
kusema wazi kwa moyo wa dhati, kwa kurudia rudia, kuwa unatambua uwezo wa mume
wako. Ukifanya hivyo utamfanya ajiamini zaidi, awe na moyo wa kuchangamka zaidi
na atajaa nguvu za kufanya vizuri zaidi ili awe shujaa wako.
Anahitaji kuheshimiwa
Heshima ni hitaji kubwa kwa binadamu yeyote anayejitambua. Tunapenda watu watufikirie katika hadhi ya juu. Ndio maana mtu yeyote anayetufanya tujione hatuna hadhi tunazozitaka, ni rahisi kutofautiana naye. Hii ni hulka ya kawaida ya binadamu.

Kwa mwanaume hitaji la kuheshimiwa
ni kubwa zaidi. Tunapozungumzia heshima kwa mwanaume, katika mazingira yetu, tunamaanisha
hali ya kutamani kujiona yu na hadhi ya juu, yu na mamlaka zaidi pengine kuliko
mwanamke. Kinyume chake ni kudharauliwa, kuwekwa katika mazingira ya kujiona
hana hadhi, hana mamlaka, asiye na kauli wala uwezo kufanya lolote bila
mwongozo wa mwanamke.
Kwa wanaume wengi, heshima ni namna
unavyoongea nae, maneno unayoyatumia katika kueleza mawazo yako, ishara za
mwili wako katika mazungumzo, kumpa nafasi ya kwanza katika maamuzi na mambo
kama hayo.
Heshima, vile vile, ni kumstahi
mwanaume unayempenda hata anapokosea. Kosa linapotumika kama sababu ya kufanya
vitendo vinavyodhalilisha hadhi yake ni kujipunguzia alama. Ndio kusema, staha
ni kuongea naye kwa nidhamu hata katika mazingira ambayo ni dhahiri yeye ndiye
mkosaji.
Kadhalika, heshima ni kuwa tayari
kumtunzia hadhi yake kwa watu wengine. Kumjengea taswira inayomwongezea thamani
yake kwa watu unaojua anawaheshimu. Kuonesha fahari yako kwake unapoongea na
watu wengine kwa kauli, matendo na hisia kunaongeza alama za sifa anazozitafuta.
Anatamani kusikilizwa, sio kukosolewa
Wanaume wengi hawapendi kukosolewa hata kama hawasemi. Unapomkosoa mwanaume unamfanya apoteze hali ya kujiamini na hivyo hujisikia kama mtu anayeongozwa. Si wanaume wengi hufurahia kuongozwa. Kinyume na kumkosoa, ifanye sauti yake isikike.
Tuchukulie mfano kuwa mwenzi wako amekuja na wazo la kufanya jambo fulani analodhani ni muhimu mlitekeleze. Kwa mwanamke msomi mwenye uwezo wa kuchambua mambo, wakati mwingine ni rahisi kubaini kwa haraka hitilafu ya pendekezo analolitoa.

Kwa haraka, unaweza kuonesha upinzani wa wazi wazi kuwa
kinachopendekezwa hakina mashiko. Si wanaume wengi wanaweza kuvumilia kuonekana
wana mawazo yasiyo na mashiko hata kama ni kweli.
Hulka ya mwanaume kutamani kuwa na sauti, inaweza kumfanya mwanaume aamue
kusisitiza wazo lake akiamini ana haki ya kuungwa mkono. Si busara hata kidogo kumpinga
wazi wazi kwa lugha inayolenga kuonesha mapungufu yake. Kufanya hivyo
kunamnyong’onyeza, hali ambayo hatakubali itokee.
Ikiwa unataka kukamata moyo wa mwanaume, jifunze kushuka na kumtanguliza katika maamuzi. Linda hadhi ya mume wako kwa kuonesha heshima kwa mawazo yake. Ukiweza kugusa moyo wake kwa kuonesha umuhimu wa anachokisema, itakuwa rahisi kutoa pendekezo lako kwa namna ambayo ni rahisi kupokelewa.

Soma sehemu ya pili inayoendeleza makala haya.
Twitter: @bwaya
Maoni
Chapisha Maoni