Kanisa Katoliki na ushirikina...

Nasikitika kwamba sijawa na muda wa kutulia kuendelea na mijadala ya imani ambayo nimekuwa niiendesha huko nyuma. Mijadala hiyo imenipa uzoefu mpya ambao mwanzoni sikuwa nao. Mijadala hiyo imenifanya nishangae inakuwaje watu wenye imani ama dini kumtukana mtu anayejaribu kuhoji masuala yaliyo ndani ya dini yake. Mtu akikuonyesha upungufu wako kwa hoja, si ni bora kumshukuru? Pengine ndiyo hulka ya dini: Waamini hujadili kwa kuongozwa na ushabiki na hisia zaidi na sio hoja.

Katika blogu ya Strictly Gospel ambayo ni blogu maalumu kwa mijadala ya Kikristo, nimekutana na mjadala ambao pamoja na kuwa bado haujapata wachangiaji wa kutosha, nadhani utakuwa mjadala moto moto huko mbeleni.

Mjadala wenyewe unahusu uchawi wa kanisa Katoliki. Hebu bonyeza hapa kushiriki mjadala huo.

Muhimu sana kushiriki kwenye mijadala. Na unaposhiriki kubali kujifunza. Ujue tumedanganywa vingi. Tumezungukwa na uongo. Katika familia zetu. Katika shule zetu. Katika siasa zetu. Dini. Na kadhalika. Na katika namna zote hizo za uongo, uongo wa dini ni mbaya zaidi. Sina shaka unajua sababu.

Mijadala, nadhani ni mahala sahihi pa kushughulika na namna zote hizo za uongo, ikiwa ni pamoja na dini zetu.

Maoni

  1. Tatizo la dini i IMANI. NA ujiamini MBUYU unameki sesi kwako kuwa ni MINGU kwakuwa hata Yesu na Muhamadi kii mani kama unaimani si tofauti sana na mwenye imani ni msafi akichambia tishu kama kuna uwezekano wa kuchambia maji.:-(

    Ukiwasikiliza wasabato unaweza kufikiri umegundua kipya mpaka uwasikilize wayahudi.

    Na ukimsikiliza Papa Mkatoliki unaweza kujisikia mjinga mapaka usikie walutheri wakigombana Kilimanjaro halafu eti Waziri Mkuu wa zamani anasikilizwa na maaskof kuliko YESU

    Samahani ngojea niende kwenye mjadala unao unukuu kabla ya kuongeza mlolomo:-(

    JibuFuta
  2. Kaka hili ni jambo ambalo wengi hawataki kuamini. Yako mengi na kwakuwa tunaamini tu toka enzi hatujipi nafasi ya kutafakari. Kaka Bwaya nakupa swali jepesi tu. KAINI ALIMWUA ABERI, JE NI SIALAHA GANI ALIYOTUMIA? hivi unajua kuna watunzi walitumia kipengere hicho kuhoji? labda ni suala la imani zaidi maana wengine wanasema alitumia akili. sasa katika blog yangu ukisaka sana utakuta nilidokeza kitabu cha THE BOOK OF LIES nilieleza tu kitabu hicho kilivyo ila sikutoa msimamo wangu. kabla sijaingia ktika mjadala huo nakupa kiini kingine cha ITOLIA YA UTATU(labda kwa kukusaidia angalia MDAHALO ambao kaka Matondo ameuandika kuhusu Papa na mzee wa kiyahudi asiyejua kusoma kuhusu walivyoshindana vidole vitatu ambapo Papa alidai fumbo la utatu lakini mzee wa kiyahudi akadai kidole kimoja). Je nini asili ya ITOLIA YA UTATU? mjadala mtamu. Na wasabato wanafunzana sana kuhusu somo moja linapewa jina la LESSON, je wajua mwanzo wake?......... mkuu ngoja niende kwenye huo mjadala......nitarudi hapa tena baadaye.......................

    JibuFuta
  3. Bwaya. Wakati ninapenda kufuatilia mijadala huwa nina kawaida pia ya kutazama approach ya uanzishwaji mijadala mbalimbali. Kwenye makala yako hii fupi ... ambayo ni utangulizi wa namna fulani ... umeanza na kwa kusisitiza kwamba tumejazwa uongo katika kila tulipowahi kukanyaga ... uongo ... uongo ... uongo ... (sorry nimeparaphrase kauli yako).
    Binafsi ninaona kwamba approach yako tayari iko biased. Unataka kutuvalisha miwani yako ili kupitia miwani hiyo tuone uhalisia. Kama miwani yako ni ya rangi nyekundu basi sote kwa kutazama kupitia miwani hiyo tutaona uhalisia ukiwa na rangi nyekundu ...

    Mimi nafikiri ... inafaa kumwaga hoja na kisha watu kwa kutumia vipawa vyao vya kuelewa na kudadisi na kuchanganua na kuchambua waamue au kukubaliana na wewe au kupingana na wewe.

    Nakumbuka niliwahi kuwa na mjadala mrefu wa ana kwa ana na wewe kuhusu IMANI. Hebu jaribu kukumbuka baadhi ya hoja tulizoongea naamini zitatusaidia katika kuchambua mambo na kuyaelezea.

    Tupo pamoja ...

    JibuFuta
  4. @Kitururu, kwa nini hali inakuwa hivi?

    @Mpangala, nimekupata. Asante kwa maoni yako.

    @Kaka Simba, je kuna kosa kuwa biased? Ni wakati gani tunahitaji kuficha miwani tuliyovaa? Asante kwa changamoto. Muhimu: makala hii nimeidesa tu kusudi wachambuzi kama wewe mkamwage maoni yenu kule!

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?