Stella mwanablogu mpya

Kila siku jamii ya wanablogu wa kiswahili inazidi kupanuka. Hivi sasa zipo blogu za kiswahili zaidi ya mia mbili na zinaendelea kuongezeka.

Dada yetu Stella naye kajiunga na jamii yatu. Bofya hapa kumkaribisha, kuona maudhui ya blogu yake na pia kuendelea kumsoma.

Dada stella, karibu sana.

Maoni

  1. Dada Stella karibu sana katika ulimwengu huu wa kublog pia katika familia hii.

    JibuFuta
  2. Karibu sana dada yetu Stella katika kijiji hiki kizuri kikuacho siku hadi siku.

    JibuFuta
  3. Albert, kwa nini unadhani blogu ni 'kijiji'?

    JibuFuta
  4. Nimetumia kijiji kama ishara ya kuonyesha kuwa bloggers na wasomaji ni wamoja,wakiwa na malengo yanayofanana yakiwemo,kuelimisha,kuburudisha,kusaidiana, n.k. vyote hivi vikilenga maendeleo chanya.Sikuandika kuwa blog ni kijiji,yawezekana ulinielewa vibaya,nilimaanisha wale wote wenaomiliki blogs wanaunda kijiji. .Nimetumia misingi ya namna ambavyo kijiji kwa tafsiri ya kawaida kinavyotakiwa kuwa.Namna mtu anavyotafsiri blogging kuanzia uwepo hadi kwenye umuhimu wake na kujaribu kufikiria anaweza kufananisha na nini, ndivyo nami nilivyofanya. Dada Yasinta mathalani,ameamua kuita ulimwengu wa kublog kuwa ni "familia" Unaweza kujiuliza pia na yeye katumia vigezo gani. Kama unajua familia ni nini,au kijiji ni nini,na misingi yake ni ipi, ndivyo jinsi pia ulimwengu wa ku-blog ulivyo. Sidhani kama kuna yeyote atakayewaza kufananisha ulimwengu wa ku-blog na jela.
    Kulingana na kumbukumbu zangu,Prof Mbele wa "HAPA KWETU" aliwahi kufananisha ku-blog na kijiji. . Hebu tembelea hapa kwetu, Www.hapakwetu.blo.spot.com na uangalie miongoni mwa posti zake,utaikuta na naimani utapata maelezo zaidi.

    Ndugu Marenga,bila shaka nitakuwa nimekujibu. Karibu sana.

    JibuFuta
  5. Nisiseme moja kwa moja kuwa kwa kulinganisha na tafsiri sahihi ya kijiji na blogging, ndivyo ulimwengu wa ku-blog ulivyo,hapana,bali blogging inapaswa kuwa na tafsiri sahihi ya kijiji . Na pia nilitumia kijiji kama kumkumbusha Dada Stella kuwa ablog kwa kuzingatia tafsiri ya namna kijiji kilivyo, japokuwa kila mmoja ana uhuru wa kuandika atakacho. Na ikumbukwe kuwa niliamua kutumia "kijiji" kulingana na tafsiri ya namna nionavyo blogging kama nilivyoeleza awali.

    JibuFuta
  6. Bw. Paul tafsiri unayoitumia ni ya kale. Vijiji vya leo si hivyo unavyovifikiri wewe. Vijiji vimekuwa kitu kingine kabisa siku hizi. Sijui kwa nini unakwepa kutumia neno jela wakati kiukweli jela haina tofauti yoyote na kijiji

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Uislamu ulianza lini?

Zijue Tabia Nne za Kiongozi Bora Kazini

Tabia za Mtoto wa Miaka 0 – 3 Kimahusiano na Kihisia