Kutoka Maktaba: Ndesanjo unaombwa kurudi kundini

Katika safari ya kupitia kilichomo kwenye maktaba yetu, niliyoisemea kidogo jana, nilimfuma mdogo wangu anayenifuata, akirejea makala za mwandishi Ndesanjo Macha. Makala hizi ni zile alizoziandika kati ya mwaka 2005 mpaka 2007 katika magazeti ya Mwananchi Jumapili.



Wakati huo mdogo wangu akiwa kidato cha tano na sita alianza kuzifuatilia kama matokeo ya mkumbo tu (pengine) lakini baadae ukawa ndio ugonjwa wake mpaka zilipotoweka ghafla zaidi ya miaka miwili iliyopita. Sasa akiwa anamaliza Chuo Kikuu mwaka 2010, makala hizo anazisoma kwa kupitia 'hifadhi' ya magazeti yale ya chumbani kwetu.


Nimeshawahi kumkuta mwaka jana akiwa na vipisi vya safu ya "Rai ya Jenerali" vyenye tarehe za mwaka 1995 mpaka 2005 vikiwa vimeungamanishwa kwa pamoja na kufanya kitu kama kitabu fulani hivi ambacho alikuwa akitembea nacho kwenye begi lake. Kwa hiyo sikushangaa kukutana na shughuli hii ya kukusanya makala za Ndesanjo hivi majuzi.




Picha hizi ni ombi maalumu kwa Ndesanjo Macha. Arudi ukumbini.






Ukiangalia makala hizo kwa haraka huwezi kukosa kubaini jambo la wazi kwamba mchango wa Ndesanjo Macha ulikuwa bayana katika harakati za ujenzi mpya wa taifa letu. Itakuwa ni vyema sana, akirudi kwenye gumzo hilo, na ikiwezekana kwenye blogu yake ya Jikomboe, ili mchango wake uendelee kuwafikia waswahili wenzake kama ilivyokuwa wakati huo.


(picha ya globalvoicesonline.org)

Najua aliko kwa sasa. Analo jukwaa kubwa zaidi. Lakini huu uwe ni wito maalumu kwa Ndesanjo Macha. Jukwaa la nyumbani nalo ni muhimu.

Maoni

  1. E MWENYEZI MUNGU WA MBINGUNI,
    SIKIA KILIO HIKI MOLA WANGU,
    USITUTIE MAJARIBUNI,
    TUSAIDIE KUMREJESHA KAMANDA WA JESHI LETU,
    TWAKUOMBA KWA KILA SALA
    TWAKUOMBA MOLA MKUMBUSHE KAMANDA WETU,
    HAKIKA TUPO JANGWANI TENA UTUMWANI MISRI,
    TUNAUGULIA KWA KITU TUNALIA SANA NDUGU YETU NA KAMANDA WETU HUY,
    EEEH MOLA SIKIA KILIO HIKI,
    NIMEWAAMBIKIZA WADOGO ZANGU UGONJWA WA NDESANJO SILA MACHA EFFECT,
    SIJUI NIJIBU NINI MAANA KILA NIULIZWAPO SINA JAWABU,
    MUNGU WA MBINGUNI TWAKUOMBA MREJESHE MUSA HUYU ATUOKOE HUKU NYIKANI UTUMWANI MISRI,

    EEEH MOLA NAKUSUJUDIA TENA TURUDISHIE KAMANDA HUYU

    JibuFuta
  2. Eeh Mola uisikie sala yetu! Amina.

    JibuFuta
  3. Twakuomba Mola uisikie sala yetu. Amen.

    JibuFuta
  4. Ee Mola wasikie hao hapo juu, kama mimi hunisikii!

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?