Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba, 2008

Kamwe usikate tamaa

Haya tena. Siku zinakimbia kama nini vile. Ni juzi tu mwezi umeanza. Leo eti masaa machache yajayo mwezi unakatika hivi hivi. Mwaka ndio usiseme. Mwezi wa kumi na moja huu. Bado mwezi tu na mwaka ukatikie mbali. Sijui kinachosababisha siku kukimbia namna hii. Muda ni mfupi kuliko matarajio. Mambo mengi kuliko dakika zilizopo. Kazi kweli kweli. Binafsi mwezi huu umepita vizuri pamoja na changamoto za hapa na pale. Nafurahi nimeweza kuzitazama changamoto hizo kwa jicho la kujisahihisha. Nawe ndugu msomaji bila shaka mwezi umekuendea vyema. Hata kama inawezekana umekumbana na changamoto mbili tatu hakuna haja ya kukata tamaa. Usikate tamaa. Kuna mtu aliwahi kuniambia picha nzuri kusafishwa kwenye chumba cha giza. Giza ni muhimu ili kusafisha picha. Maana yake yake unapojikuta kwenye hali inayofanana na giza vile, kwa maana ya changamoto, kukatishwa tamaa, chukulia hiyo kama mchakato wa kukutengenezea picha nzuri mbeleni. Usikate tamaa. Pigana kiume. Songa mbele. Anza mwezi wa kumi

Haiba ni nini?

Sipendi kutumia kiingereza kwa sababu kwanza ninadhani kiswahili kinanitosha kabisa kuelezea kile ninachotaka kusema. Hata hivyo najua pia matumizi ya kiswahili chetu hayajawa katika kiwango kile kilichokusudiwa. Kuna maneno mengi yasiyoeleweka vizuri katika kiswahili cha kitabuni. Moja wapo ya maneno hayo ni hili ninalolitumia leo hii. Haiba. Pengine niweke msisitizo kwa faida ya wale wasiolifahamu neno hili vizuri. Personality. Wengine wanasema maana ya hichi kinachoitwa personality ni utu kwa kiswahili. Ni bahati mbaya kwamba niliyakimbia masomo ya lugha siku nyingi. Ila nimejiridhisha kwamba haiba ndiyo tafsiri muafaka kabisa. Haiba ni nini? Watu wengine watafikiria tunazungumzia mwonekano wa mtu kimavazi. Lakini haiba ni neno pana zaidi ya mwonekano wa mtu kwa nje. Haiba ni jumla ya tabia za mtu zinazotokana na kile anachofikiri, anachopenda, anavyojichukulia yeye mwenyewe, anavyowachukulia watu wengine na kadhalika. Haya yote hujenga mwonekano wa mtu unaopimika (tabia) kama vi

Nadharia ya kuwaelewa wenzio

Bila shaka umeshawahi kugombana. Kupishana na mtu. Kushindwa kuelewana na mwenzako. Kupishana maana yake ni wawili ninyi kushindwa kuelewa kila mmoja wenu anataka nini. Pengine tuanzie hapo. Kuwaelewa wengine. Je, tunaweza kuwaelewa watu wengine? Na tutajuaje kuwa tunawaelewa? Kuelewa mawazo ya mtu, imani yake, matakwa, nia na kadhalika ni jambo la muhimu. Na pengine si tu kuelewa mtu mwingine anawaza vipi, bali vilevile kutumia uelewa huo ili kutafsiri ya kile kinachosemwa na kufanywa na mtu mwingine. Pengine tunaweza kukubaliana kwamba ni kushindwa kuwaelewa wengine ni upungufu mkubwa katika masha ya kimahusiano. Upungufu wa kuwaelewa wengine kujionyesha katika dalili zifuatazo: o Kutokuguswa na hisia za watu wengine. o Kutokuweza kuzingatia wanachojua wengine o Kutokuweza kusuluhisha mambo kwa kuitazama nia ya mtu mwingine wakati alipokosea o Kushindwa kuelewa ikiwa anayekusikiliza anavutiwa na unachosema ama unaongea tu kwa sababu una mdomo o Kushindwa kubashiri maana il

Teknolojia ya simu kwa maendeleo ama kuongeza upuuzi?

Siku hizi kila mtu ana simu ya mkononi. Na kama huna simu unaonekana kama mshamba flani hivi. Kijana gani huna simu? Na si tu kuwa na simu bali ughali wa simu yenyewe. Tunaambiwa asilimia karibu 35% ya watanzania wanamiliki simu za kiganjani. Pengine hayo ni maendeleo. Chukulia Tanzania ambayo ni nchi fukara kuliko hata zile zinazoitwa za ulimwengu wa tatu eti nayo katika hili la simu za mkononi unaambiwa ni kati ya nchi wateja wazuri wa teknolojia hii. Hapo unaona uhusiano wa simu hizi na akili za kimaskini. Sasa tuachane na hayo. Tuje katika matumizi yenyewe ya hizi simu. Kusema kweli wengi wa watumiaji simu hizi, wanazitumia katika mambo ambayo kuainisha faida zake hasa si kazi rahisi. Simu ni mapenzi. Simu ni ngono. Simu ni kuongea upuuzi tu kwa mamia ya dakika. Na ni ajabu sana kwamba waathirika wakuu ni wanafunzi wa vyuo vikuu. Wasomi. Kama vile intaneti zinavyotumika kwa mambo ya kipuuzi na wasomi hawa, ndivyo simu nazo zinavyoendeleza kasumba ile ile: Matumizi wa teknoloj

Kwa nini tunatafuta kasoro zaidi? Mchango wa Nuru Shabani

Tuliwahi kuzungumzia tabia ya kuwaza kupenda kutafuta kasoro. Ilijitokeza michango kadhaa. Hapa ningependa kukuletea mchango mmojawapo uliojaribu kueleza sababu za watu kuwa na tabia hiyo. Namshukuru msomaji Nuru Shabani asiyeishia kusoma na kuondoka. Yeye kuacha maoni yenye lengo la kupanua mjadala zaidi. Anasema: "Watu wengi tumelelewa katika kuutafuta udhaifu au makosa ya mtu na ndiyo tunachokina zaidi kuliko uimara wake. Hiyo siyo asili ya mwanadamu ila ni malezi ambayo tumefundishwa na wazazi nyumbani,walimu mashuleni na jamii iliyotuzunguka. Vitabu vya dini vinatuambia tumeumbwa kwa mfano wa Mungu, sasa Mungu huyo ambaye ametuumba mbona haangalii kasoro zetu?? "Hii inaonesha kuwa tabia ya kukosoa ni ya kufundishwa na wanadamu wenzetu tena wale wasiojiamini na wenye kutazama mambo kwa upande mbaya. " Kutizama mambo kwa mkabala hasi ni jambo ambalo tumekuwa tukifundishwa kila siku na watu ambao kwa namna moja au nyingine tumepita katika mikono yao kimalezi,n

Je kuna uhusiano kati ya kutembea kwa mtu na tabia yake?

Nuru shabani ni mchangiaji mzuri katika kibaraza hiki. Michango ya msomaji huyu ama kwa hakika kuleta mawazo mapya na yenye faida. Asante sana Nuru Shabani. Kuna swali ameliuliza na nadhani kwa sababu blogu hii ni uwanja wa kujadili mambo yanayohusiana na tabia zetu, swali hili lipo mahali pake. Nimeona ipo haja ya kuliweza wazi kwa ajili ya tafakari za wasomaji wengine wanaopenda mijadala ya aina hii. Yeye anauliza: " Je, kuna uhusiano kati ya kutembea kwa mtu na tabia yake?" Karibuni kwa michango ya maandishi kupitia kisanduku cha maoni kwa faida ya wasomaji wengine. Je, anavyotembea mtu, kunaweza kutafsiri anavyowaza/tabia yake? Asante Nuru Shabani kwa usomaji wenye faida.

Je, hatuwezi kuishi bila ngono?

Siku hizi ni kawaida watu kukutana kimwili  bila ndoa. Ndio maana neno tendo la ndoa halitumiki. Ni ngono. Na hata hivyo inaonekana pia chaweza kufanyika bila mapenzi, kwa hiyo wakabatilisha kukiita kufanya mapenzi. Hiyo ndiyo hali halisi. Mjadala wenyewe ulikuwa katika kuhoji ikiwa kijana wa kisasa anaweza kufikisha miaka zaidi ya ishirini na tano bila kuonja ngono(na kijana mwenyewe asiwe mgonjwa, kwa maana ya hitilafu katika mfumo wake wa uzazi) Je, anaweza kuahirisha kuanza ngono hata kama mwili wake unamshawishi kufanya hivyo? Maana inasemekana kwa mujibu wa wadau hawa, katika siku za leo, ngono haikwepeki! Wewe unasemaje? Ngono ni kama chakula? Kwamba usipoipata utaumwa? Na je, haiwezekani kuwa na mahusiano ya karibu (mno)lakini 'no' ngono? Na kwamba huu mtindo wa kuanza ngono mapema kwa vijana wengi unasababishwa na nini? Ni mwili tu ama ni tatizo la kisaikolojia zaidi? Kwamba ni kujilemaza fulani hivi kuwa aah kila mmoja anafanya bwana? Jielewe

Siri ya mwandiko wako (2)

Kama tunavyoweza kumwelewa mtu kwa maneno anayoongea, pia twaweza kumwelewa kwa kuuangalia mwandiko wake. Unapoandika kwenye karatasi, ukweli ni kwamba unatupa dodoso kuhusu tabia zako. Hebu na tuangalie mifano michache ya aina za miandiko na tabia zinazojidhihirisha kupitia miandiko yenyewe: 1. Mwandiko wa kukandamiza: Maana yake akiandika nundu nundu za herufi zinaonekana upande wa pili wa karatasi. Ni dalili ya fikira chanya, kujiamini (hata kunakozidi mipaka) jeuri saa nyingine, majigambo. 2. Kuandika juu juu kwa kuparua: Kutokujiamini, na tabia ya kufikiria mambo kinyume. Yaani kufikiria ubaya, udhaifu wa jambo zaidi. 3. Mwandiko unaolalia kulia: Mwandishi anafikiria anakoenda zaidi, anafikiria mbele. Mara nyingi hana muda wa kutafakari makosa yaliyowahi kumtokea kwenye maisha yake. 4. Mwandiko unaolalia kushoto: Hufikiria jana na yaliyopita. Hujilaumu kwa makosa aliyowahi kuyafanya. 5. Mwandiko unaoongozeka ukubwa kadiri unavyoandika: Mwandikaji ni mbunifu, mkali, huju

Siri ya mwandiko wako

Hivi umewahi kujiuliza kwa nini mwandiko wako unatofautiana na miandiko ya watu wengine? Hivi unajua kwamba mwandiko unaweza kutupa habari za kutosha kuhusu tabia yako, mwenendo wako, kiasi cha akili ulichonacho na kadhalika? Kuna siri gani katika miandiko yetu? Subiri kidogo nakuja...

Jinsi ya kumsikiliza mwenzio

Tulikwisha kuangalia kwa utangulizi umuhimu wa kusikiliza. Kwamba watu tunaozungumza nao wanaweza kuwa hawajui yale tunayoyajua ama hata kwa kiwango chetu. Lakini je, tunajua kila kitu? Jibu ni wazi kwamba si kweli. Wapo watu wengi wanaojua kuliko sisi katika maeneo kadha wa kadha. Watu hao hawana alama usoni inayowaonyesha weledi wao. Bahati mbaya ni kwamba wajuao huonekana kama vile hawajui. Kwa hivyo, kwa sababu hiyo ya kutoweza kumtambua ajuaye kwa kumwangalia tu, basi hiyo iwe ni sababu tosha ya kukushawishi kuwasikiliza watu wanaokuzunguka. Tufanyeje kusikiliza kwa makini? Tutumie mbinu gani? Hapa tutataja kadhaa, ambazo hata hivyo si msahafu. Tuzijadili kuona kama zaweza kufaa kutufanya kuwa wasikilizaji wazuri zaidi. Mawasiliano ya kweli baina ya watu wawili yana hatua tatu: 1. Kusikiliza: Maana yake kufanya jitihada za dhati kujaribu kusikiliza kile hasa kinachosemwa na mwenzio. 2. Kuelewa: baada ya kufanya jitihada za kusikiliza kinachosemwa, sasa unajitahidi kupat

Jifunze kusikiliza kuliko kusema

Kusema ni rahisi kuliko kusikiliza. Kumsikiliza mtu ni kazi ngumu. Hasa kama anayezungumza anaonesha kuwa na mawazo unayodhani yanatofautiana na mawazo yako ama pengine yanapingana kwa kiasi kikubwa na mawazo yako. Kazi inakuwa kubwa kweli kweli hasa inapoonekana kama vile mzungumzaji ana uelewa mdogo kuliko wako. Yaani anapozungumza unahisi kama unaelewa anakokwenda, anachotaka kusema, anawaza nini na kwa nini anataka kusema hivyo anavyovisema. Unaelewa na unashindwa kujizua kuonyesha hisia hizo na hivyo unathubutu kuingilia sentensi zake. Kumsikiliza mwenzio na kusoma mawazo ya mwenzio si kazi rahisi. Ni kazi ngumu kweli kweli. Ni bahati mbaya sana kwamba wengi wetu tunapenda kusema. Tunapenda kusikilizwa. Tunapenda watu wengine wasikilize zaidi mawazo yetu kuliko sisi tunavyowasilikiza wao. Pengine ni kwa sababu ya ile hulka kwamba "Ninajua..." Hatuwezi kuukana umuhimu wa sisi kujitahidi kujifunza kwa bidii kuwasikiliza wenzetu. Sababu ni kwamba vile tunavyovijua n

Kwa nini miungu ni mingi kiasi hiki?

Hakuna jamii ambayo haijawahi kuwa na wazo la uwapo wa nguvu iliyo juu ya asili ya ulimwengu. Nguvu hii imeitwa majina mengi lakini lililo maarufu ni mungu. Wengi wetu, hata kama hatuna ushahidi wa kujitosheleza, bado hatusiti kabisa kuamini kuwa mungu yupo. Ukiangalia vyema utaona namna ambavyo dunia inayo miungu kwa maelfu, na kila mungu ana sifa zake tofauti na miungu wengine. India kwa mfano, tunaambiwa kuwa idadi ya miungu inaweza kuzidi hata idadi ya waumini wenyewe! Na ni makosa kudhani kwamba wingi wa miungu hiyo ni majina tofauti tofauti kwa mungu huyo huyo. Sababu ni kwamba hata mahitaji yao yanatofautiana. Kanuni wanazotoa ili tuwafikie zinatofautiana. Tabia zao zinatofautiana. Kwa hiyo, ni wazi kuwa miungu wako wengi. Sasa kwa nini dunia inayo miungu mingi hilo ndilo swali ninalotaka kukuachia leo. Inakuwaje kila jamii inavutiwa na wazo kuwa yupo mungu hata kama haonekani? Wapo wanaoamua mpaka kutengeneza sanamu kuhusianisha kile wanachokiamini na kitu kinachoonekana.

Kulikoni JUMUWATA?

Picha
WENGI wetu tunakumbuka namna ambavyo vuguvugu hili la blogu lilikuja kwa kasi kama miaka mitatu hivi iliyopita. Na Ndesanjo Macha akiwa mhamasishaji mkuu katika ukuzi wa Teknolojia ya blogu katika kiswahili kwa kujitolea. Kampeni zake zilitufikia wengi wetu kupitia ukurasa wake wa gumzo la wiki katika gazeti la mwananchi . Nina hakika kwamba kazi hiyo hakuifanya kwa malipo. Alijitolea muda wake na matunda yake yalikuwa wazi. Bila yeye, bila shaka blogu maarufu kama Michuzi , Bongo celebrity , Kijiji cha Mjengwa , Haki Ngowi , Now and then na nyinginezo nyingi bila shaka zisingekuwepo. Narudia neno bila shaka. Historia ya Blogu Tanzania haiwezi kukamika bila kumtaja yeye. Basi. Kasi ya blogu iliendelea kukua kwa kasi mno kiasi cha kufikia kuundwa kwa Jumuiya ua Wanablogu Tanzania. Wakachaguliwa viongozi tarehe 29 Juni 2007. Tukafurahi. Hata hivyo, lazima tuwe wazi kwamba kasi ya ukuaji wa blogu imeendelea kuwa ndogo kwa karibu mwaka sasa. Jeff Msangi aliwahi kuzungumzia suala h

Hivi watoto 'wa mitaani' wakikua huenda wapi?

Mimi sikuwahi kujiuliza swali hili. Baada ya kuisoma makala ya Ayoub Ryoba katika Gazeti la kila wiki la Raia Mwema nilifikiri mara mbili mbili: Hivi kweli hawa watoto tuliowabandika majina mengi ya fedheha kama eti watoto wa mitaani huenda wapi wakikua? Hapo tu. Hawa watoto ambao wengi wetu hatuna habari nao, si wanakua? Je, wakikua 'wanaishiaga' wapi? Ni watoto waliokata tamaa. Hawana amani. Wanaiona jamii kama inayowaonea. Wana kisasi. Je, wanapokuwa huishia kuwa akina nani? Hii ni changamoto ya aina yake. Namshukuru mwandishi huyu kwa kutukumbusha eneo hili kwa uzito unaostahili. Fikiria watu kama wabwia unga. Majambazi sugu. Makahaba na kadhalika. Uone mzunguko wa aibu tunaoujenga katika jamii. Kama unadhani kuwa matatizo yao hayakuhusu, tafakari kwa bidii. Tunaweza kupunguza tatizo hili la kuwa na watoto wengi wa aina hii, amabo wakiisha kukua wanaturudia kwa mlango wa nyuma kwa kuacha tabia ya hovyo ya kupenda kuzaa bila kuhesabu gharama.

Kura nipige mimi, kula wale wenyewe?

Niko saluni jioni Jumamosi. Kuna vijana wanne. Umri wao wote ni kati ya miaka 20-30. Kinyozi: (Huku akininyoa baada ya kimya kifupi)…Ee bwana watu wengine noma. Mie: Imekuwaje? Kinyozi: Hapa watu karibu wapigane kisa Simba (timu ya mpira wa miguu) kafungwa mbili na Azam kitimu kidogo... Mie: Kwani tatizo ni nini? Kinyozi: Tatizo ni kwamba wanaopigana hata kadi za uanachama hawana. Mie: Labda ushabiki si unajua tena…au wewe hushabikii mpira? Kinyozi: Mi hata sifuatilii sana mambo ya kijinga haya. Mi nafuatilia mambo yangu bwana. Mie: Kwa hiyo mpira hufuatilii kabisa? Kinyozi: Hata mara moja bosi wangu. Upuuzi mtupu. (Akalalamikia uongozi mbaya wa timu zetu kwa zaidi ya dakika tano kisha…) Mi labda timu za Ulaya. Napenda Aseno. (Akatumia dakika kadhaa kuifagilia) Mie: Una kadi ya Aseno? Kinyozi: (Akicheka) Sina ila sipigani wakifungwa Mie: Sasa hapa home unafuatilia nini? Kinyozi: Bongo nifuatilie nini hapa pamechoka hivi… kwanza ningekuwa na uwezo ningezamia

Mtembelee mwanablogu mpya Kristine Missanga

Karibu umtembelee mwanablogu mwenzetu, ambaye bila shaka anayo mengi mapya. Falsafa. Mtizamo mpya. Maswali. Lengo lake kama anavyosema mwenyewe ni kutujengea utamaduni wa kujiuliza. Blogu yake inaitwa Jiulize. Unaweza kumtembelea kwa kubofya hapa kumsalimia.

Maisha hayawezekani bila wanasiasa?

Kama kuna 'kazi' ambazo zinanitatanisha ni zile zenye uhusiano wa moja kwa moja na kile kinachoitwa siasa. Kazi hizi zimepata umaarufu sana katika nchi za dunia ya tano ikiwamo Tanzania. Kuna wanaoamini kuwa siasa ni porojo. Siasa ni usanii. Siasa ni uchezewaji wa wazi wa akili za watawaliwa. Udanganyifu. Utapeli wa wazi. Siasa. Sina hakika kama ninakubaliana na mawazo haya. Bado natafakari. Kwamba siasa ina uhusiano na maendeleo yetu (hasa sisi wa dunia ya tano) hilo ni jambo la kufikirisha. Siku hizi siasa imekuwa kama muziki wa Bongo Flava. Kila mtu anataka kujihusisha nayo. Wataalamu wa fani mbambali wenye ujuzi adhimu, wanazitosa ofisi zao na kukimbilia siasa. Tunawafahamu walimu wa Vyuo Vikuu ambao hata hawana haiba ya siasa, bado walidiriki kuzitosa ofisi zao. Kisa? Ulaji. Samahani siasa. Na idaidi yao haihesabiki. Mtu unajiuliza mwananchi aliyesomeshwa kwa fedha ya walipa kodi fukara, na akawa mathalani daktari bingwa, ama mtaalam wa uchumi kwa mfano, anaachana

Furaha ni uamuzi wako mwenyewe, amua

KILA mtu angependa kuwa mwenye furaha. Wapo wanaamini kuwa lengo la maisha ya mwanadamu hapa duniani ni kuitafuta furaha. Kwamba purukushani zote hizi katika maisha zina lengo la kuisaka furaha. Fikiria vitu kama pesa, elimu, ndoa nzuri, familia, umaarufu na kila kilichojema ambacho mwanadamu hukitafuta kwa bidii lengo ni kuitafuta furaha. Vitu kama dini kimsingi lengo ni hilo hilo -furaha. Kwamba dini inakuwa ni kimbilio rahisi katika kuyasahau matatizo tunayokumbana nayo hapa duniani kwa mawazo kwamba tuendako ni bora kuliko hapa. Matokeo yake tunakuwa na matumaini zaidi. Tunakuwa wenye furaha. Lakini ni bahati mbaya sana kwamba watu wengi hatuna furaha. Tunatafuta elimu tukidhani tunaweza kupata furaha lakini si hivyo inavyokuwa.(Inasemekana kwa kadiri unavyokuwa na elimu ndivyo unavyozidi kuziona kasoro katika maisha yanayokuzunguka na hivyo kukupungizia furaha) Tunatafuta pesa, kwa matumaini hayo hayo, lakini hata tunapokuwa nazo bado hazitupi furaha. Tunapata mahusiano tuna

Kukosoa, kutafuta makosa, si tabia njema

Siamini kwamba ukosoaji ni asili ya mwanadamu. Kufikiria kinyume (negative). Kwamba watu wote wanakosea isipokuwa wewe. Kwamba watu wote wamepotea isipokuwa wewe. Kwamba watu wote wanahitaji msaada isipokuwa wewe. Kufikiria ubaya zaidi wa jambo kuliko uzuri wake. Kufikiria udhaifu kuliko ubora wake. Kufikiria uharibifu zaidi kuliko uboreshaji. Kwamba unaweza kusoma kitabu cha mwandishi fulani, si kwa sababu unataka kujifunza, bali kupekua wapi kakosea. Kwamba unaweza kuzungumza habari za mtu, si kwa nia ya kujenga, bali kwa nia ya kumtafutia makosa yake. Kwamba watu wanaweza kukwambia jambo zuri na la manufaa, lakini wewe ukalichukulia kwa mtazamo hasi. Ukakosoa. Kwa nini iwe rahisi zaidi kufikiria udhaifu/ubaya wa mtu/suala kuliko kufikiria uzuri wake? Hivi mwanadamu anavutiwa na nini kutafuta kasoro? Je, kutafuta/kupekua kasoro ni asili ya mwanadamu ama ni tabia inayojiotea kulingana na mazingira ya mhusika?