Ni kweli, Fossils, mabaki ya viumbe wa kale ni ushahidi wa Evolution?

Msomaji mwenye historia ya elimu ya viumbe anaweza kuuliza: Uhusiano tunaouona baina ya viumbe (phylogenetic relationship) una maana gani?

Kusema kweli, viumbe wanaonekana kuhusiana kwa karibu. Na uhusiano huo unaleta mawazo kuwa huenda kila kiumbe ametokana na mwenzie.

Kwa mfano inavyoonekana, maisha hasa ya viumbe yalianzia baharini. Kwa maana hii, viumbe wa kwanza waliishi majini wakibadilika badilika na kuishia kufanya aina nyingine ya maisha yasiyotegemea maji, yaani maisha ya nchi kavu. Sasa katika kuangalia mlolongo huu, tunaambiwa viumbe walijikuta wakijiongezea “viungo” (adaptive features) vilivyowawezesha kukabiliana na aina vyingine ya maisha.

Kwa ule mfano wetu wa samaki, ni kwamba baadhi ya samaki walianza kupoteza uwezo wao wa kupumua kwa kutegemea maji, na badala yake, wakaanza kuwa na vitu kama mapafu vilivyowasababisha kugeukia maisha nje ya maji. Baadae makoleo yao yaliyotumika kuogelea (fins) yakatengenezeka kuwa (miguu?) ili waweze kuishi vizuri nchi kavu. Na mlolongo kama huo unaotufikisha kwa viumbe kama binadamu.

Kama ambavyo msomaji wa kawaida ataona, “tuhuma” hizi ni nzito sana. Tuhuma kwamba viumbe waligeuka geuka tu kutafuta maisha mengine, si habari nyepesi. (Hasa unapodai kuwa mabadiliko haya yalijiongoza yenyewe).

Ninakubali kuwa viumbe wamehusiana. Lakini sikubaliani na wazo kuwa mageuzi haya yanamaana kwamba viumbe “waliota” kutokea kwenye viumbe waliokuwapo.

Haiingii akilini kwamba chembechembe za viasili eti vibadilike kizembe zembe tu kwa madai kuwa vinatawaliwa na mabadiliko ya asili yenyewe.

Ni vigumu kwa sababu hata ushahidi wa nadharia hizi unakosa maana bila kwanza kuhusisha “imani”.

Ushahidi mwingi unategemea zaidi mabaki ya viumbe wa kale waliopotea (extinct) yanayoitwa fosili. Na mara nyingi daraja kati ya uhusiano wa aina moja ya viumbe na vingine linaundwa na viumbe hawa waliopotea kwa ushahidi wa mabaki hayo. Na inapobidi, kwa kutumia uhusiano unaojionyesha baina yao kwa kile kinachoitwa mtiririko wa mabadiliko yao (phylogenetic tree).

Kwa nini ninafikiri kuwa uhusiano baina ya viumbe una maana nyingine tofauti na hii tuliyokwisha kuiona, hilo ndilo litakaloanza nalo baada ya muda mfupi.

Hitimisho la leo: Mabadiliko kutoka kiumbe mmoja kwenda kiumbe mwingine, si jambo linalowezekana isipokuwa kwa agenda ya kuikana asili ya uendeshaji wa uhusiano baina ya asili na viumbe vyenyewe.

Maoni

  1. Kama viumbe vinabadilika kukabili ana na hali halisi, basi tusiogope hali mbaya ya mazingira au magonjwa kama UKIMWI. SI itamaanisha binadamu wata adapt tu?

    JibuFuta
  2. I recommend you to listen to the following lecture at www.thinairevent.com
    You will known all the answers about evolution.

    JibuFuta
  3. makubwa haya na hii science ya adaption to evolution ,na UKIMWI utaingia huko??Itachukuwa muda gani hadi tu adapt?

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Haiba ni nini?

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Uislamu ulianza lini?

Makundi Manne ya Tabia za Watoto Kitabia