Kwani akina mama wanatumia nywele za bandia? Ni ili iweje?

Kama kuna mambo ambayo huwa yanathibitisha kuwa waafrika wengi hatuoni raha ya kuwa waafrika ni hili la nywele za bandia.

Wanawake wa kiswahili wanateketeza muda mwingi na fedha nyingi kutengeneza nywele zao ama 'kununua' nyingine zenye asili tofauti. Kwao huko ndio kupendeza. Ukibaki na za kwako ukazitunza zikawa nzuri, zikabaki za kiafrika, hujapendeza bado.

Kwamba kwa kufanya hivyo wanapendeza ama vipi, hilo kwangu sio suala. Kinachonitatiza ni sababu ya kuzitengeneza ziwe na asili tofauti: Hivi ni kwa nini? Hawawezi kupendeza bila kubadili asili ya nywele? Si kwamba ni dalili flani ya kujiona mwenye asili duni kuliko watu fulani? Si kwamba hii ni dalili ya udhaifu wa kujielewa na kujiamini?

Wewe unafikiri vipi kuhusiana na hili? Kwangu hii ni aibu moja wapo ya waafrika. Kabisa.

Maoni

  1. SIO NYEWLE TU LAKINI HATA MKOROGO.WAAFRIKA TUNA NGOZI YETU NYORORO TENA NZURI AMBAYO INAWEZA KIPAMBANA NA HALI ZOTE ZA HEWA YAANI JOTO KALI NA BARIDI PIA, LAKINI TUNAAMUA KUUA NGOZI YA JUU(MELANAINI SKIN)NA KUACHA KIDONDA KTK NGOZI NA KUJIITA KWAMBA SISI NI WEUPE. ALIKUAMBIA WEUSI NI MBAYA NI NANI?

    JibuFuta
  2. Umesema kweli ndugu yangu. Weusi ni ufahari. Kabisa.

    Asante kwa kuacha maoni yako. Karibu tena.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?