Ni kweli, tusiwategemee wanasiasa!

Jamani ninasikitika siwezi kublog mara kwa mara maana kidogo shule inanibana. Hata hivyo, huwa najitahidi kujua kuna nini kinaendela katika mtandao. Kwa kifupi, ninafuatilia sana soga za wanablogu (saaaanaa!)hata kama sitoi mawazo moja kwa moja kulingana na muda na masuala fulani ya shilingi. Namshukuru Mungu, ninakaribia kuwa huru, nitaonekana kila inapobidi.
Mimi ni mpenzi wa safu ya Gumzo la wiki katika Mwananchi Jumapili. Pamoja na ukata mkali unaotukabili sisi tulio "wa kusoma", sikumbuki ni Juma lipi lilipita bila kulipitia kujua lina gumzo gani. Ni gazeti la kusoma ingawa ndio hivyo vijana wengi hatuonekani kupendelea magazeti siriaz, kama alivyobaini Padri Karugendo katika Rai toleo fulani.
Juma lililopita kulikuwa na hoja nzito kwamba tusilogwe kuwategemea wanasiasa kutuletea maendeleo binafsi. Mwandishi alifanikiwa kunishawishi kwa hoja kwamba kuendelea kunahitaji mikakati na juhudi binafsi zaidi, kuliko kulia lia tukiwategemea wanasiasa wasiotabirika! Somo hili limenijia kwa namna tofauti zaidi pamoja na kwamba tuliwahi kulipitia kwenye soga zetu za kishule shule zisizorasmi.
Kwa kweli nadhani kuna haja ya watanzania kubadilika na kuacha kufikiri kuwa mkombozi wao ni mtu aitwaye mwanasias, kwani hilo haliwezekani abadani, hasa hasa mwanasiasa mwenyewe akiwa ni chama Twa-wala.
Kuna haja ya kubadilika.

Maoni

  1. Watwawala wanapenda sana watawaliwa wakidhani kuwa bila wao (watwawala) hakieleweki kitu. Siri kubwa kabisa ambayo wananchi wa kawaida wanatakiwa kuijua (ingawa ukweli hii sio siri) ni kuwa sisi ndio tuna nguvu na mamlaka ya kuamua jinsi gani tunataka maisha yetu yaendeshwe na nchi yetu ielekee wapi. Lakini hawa jamaa wamebadili mambo, badala ya kuwa watumishi wetu, sisi ndio tumekuwa watumishi wao.

    JibuFuta
  2. naungana kabisa na kaka ndesanjo katika hili la maana iliyopinduliwa! kati ya kiongozi na raia nani kumtumikia mwenzie! kwa tanzania mtwa waliwa ndio anamtumikia mtawala. ndio maana watu hukimbilia uongozi! nikiwa ninasikitika kufuatilia kupoteza nguvu upinzani bungeni, nilikutana na rafiki yangu toka eritrea akaniuliza kulikoni nikamjibu. akaniuliza kwanini imekuwa hivyo nikamjibu pia jinsi mifumo ilivyoundwa undwa pamoja na wananchi kuukosa ufahamu wa uraia! akashauri kuwa kumbe inabidi watu wawe kwanza huru kabisa ili waweze kufanya maamuzi toka moyoni mwao! na akasisitiza kuwa ni vyema watu wakajiwekea mikakati ya kujitegemea zaidi ya kuitegemea serekali - mfano ajira kwani huo ndio utumwa namba moja! sijui wenzangu mnasemaje!

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?