Tunawezaje kujinasua na matatizo ya msongo wa mawazo?
Hivi sasa imekuwa ni kawaida kukutana na mtu anayezungumza mwenyewe. Na si tu kuzungumza mwenyewe, bali hata kurusha rusha mikono huku na kule. Waweza kukutana na mtu anayetazama lakini haoni, anayesiki lakini hasikilizi, na anayesema asichojua anachokisema. Si hivyo tu. Imeanza kuzoeleka kukutana na mtu ofisini mwenye hasira za mafungu dhidi ya kila anayehitaji huduma yake. Hasira zinazoambatana na kufoka, kusema pasi mpangilio, na hata kutukana watu wasio na makosa ya moja kwa moja hovyo hovyo. Vile vile, ni kawaida kukutana na watu wenye ghadhabu katika sehemu za umma, kama kwenye usafiri wa wote, foleni za benki na kadhalika. Watu wanaonekana kuwa na hasira ambazo kimsingi chanzo chake si hapo alipo. Hizi ni dalili za msongo wa mawazo. Na zipo nyingi. Kuyasema haya hatujaribu kuonyesha kuwa msongo wa mawazo/stress ni kitu kibaya moja kwa moja. Hapana. Kwa hakika kiasi fulani cha stress kinahitajika ili kutufanya tuhimizike kupiga hatua fulani. Hata hivyo, msongo huu ...