Arusha warembo ni majasiri wa kibiashara
Nimewapenda akina dada hawa wanaojishughulisha na biashara halali kama hizi. Ni majasiri wasiosita kufanya shughuli kama hizi kujipatia kipato licha ya urembo wao.
Hapa niliwafuma wakimsubiri mwenzao. Then wakaendelea na shughuli zao. Pongezi kwao.
Kwa mtazamo wangu ujasiri kama tabia huongezea bonge la chachandu katika urembo wa kibonge.
JibuFutaBora ya hivyo maana wakizubaa watalala njaa, nawapongeza sana kwa ujasiri wao
JibuFutaHiivi ndivyo inavyotakiwa Hongera akina dada.
JibuFutaBinafsi sishangazwi na muonekano wa kina dada ukilinganisha na kazi waifanyayo. Mimi naona ni swala la kujipenda na pia kuweka imani kwa wateja.
JibuFutaAu ndo yale ya mwalimu haruhusiwi kuvaa tisheti na jinsi? Au kwa vile mpasua mawe kavaa suti na akikueleza kazi afanyayo unasita kuamini? Au aliyevaa suti hategemei kupewa kwanja akafyeke nyasi na hajiulizi kama akipewa itakuwaje.?
tawile yasinta ngonyani. badala ya kulalamika kumtafuta mchawi wa matatizo yako ni vema ukajishughulisha.
JibuFutaHuo si ujasiri ni picha kamili ya namna gani mfumo mbovu wa uendeshaji shughuli za uzalishaji mali unavyowatenga wananchi hayo ni mateso,na si ujasiri,kwa mfumo mzuri walitakiwa wawe wametengewa maeneo ya biashara wapewe mikopo na ekimu bora,na ujasiri utakuja kuonekana pale watakapoweza kurudisha mikopo na kuweza kusimamia miradi yao bila madeni vinginevyo hao wapo katika mateso kwa sababu ya sera mbovu za uendeshaji nchi za ccm.
JibuFutamzazi chopanga