Mwezi Desemba na suluba zake

HIVI unajua kuwa mwezi kama huu, mwakani, serikali iliyopo madarakani itakuwa imeenda zake? Hivi hivi tunashuhudia serikali hii ikimaliza muda wake. Namna gani tunalishuhudia hili inategemeana na asomaye mistari hii.

Nilisahau hata nilichotaka kusema. Ni bukheri wa afya nasubiria mwisho wa mwaka. Kama kuna mwezi wenye sikukuu kibao ndio huu. Halafu naona kama siku kuu zote hazina mantiki kabisa. Kuanzia hii ya kesho kutwa (ya kusherehekea uhuru usiokuwepo) mpaka zile nyingine za kuadhimisha siku za kiroho kwa ubwabwa na mavazi.

Uzuri wa mwezi huu tuna uhakika wa siku kadhaa ambazo tutabaki tumelala nyumbani. Kisa? Hakutakuwa na kazi kwa hivyo ofisi zitafungwa na kama kawaida tutaendeleza kwa kasi umasikini wetu ambao wapo wenzetu wanautumia kuendesha harakati za kuubakiza ili dili lisife.

Unakumbuka wakati wa mzee Mwinyi, siku kuu ikiangukia siku za wikendi, basi siku hiyo inahamishiwa Jumatatu ili watu wale raha na kusahau kuhudumia wananchi.

Ayaa... nimeenda nje ya pointi. Nimejistukia. Nasubiria siku kuu za mwezi Desemba. Baada ya hapo, mwaka bila shaka utaanza kwa machungu ya bajeti iliyoharibika kama sio madeni kabisa.

Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?