Tuiamini sayansi? Au ni ghiliba tu?

MIONGONI mwa maeneo ambavyo sayansi imekuwa ikijihusisha nayo, elimu ya viumbe ni mojawapo. Unapozungumzia viumbe unalazimika kuanzia na uhai wenyewe, Uhai ulitokea wapi? Tunaambiwa baharini mahala ambapo viini urithi viitwavyo DNA vinaaminika kutokea kirahisi rahisi. Bahari nayo ilitokea wapi, tunajibiwa utafiti bado unaendelea, tuvute subira. Dunia yenyewe ilitokea wapi, hapo nako tunaambiwa wanaotaka kufanya Shahada ya uzamifu, wazame. Hapo hatujauliza ulimwengu uliobaki (universe).

Jambo moja ni wazi. Kuwa katika sayansi, mambo yanapokuwa magumu, rufaa huwa: TUNGOJE, maarifa hukua taratibu! Lakini ni ukweli kwamba kauli hii ni kichaka kile kile cha kukimbiwa maelezo.

Tukiachana na asili ya uhai, sayansi inajaribu “kupendekeza” nadharia ya utokeaji wa idai tofauti tofauti ya viumbe tulivyonavyo leo. Mahala pa kuanzia ni kwamba inavyoonekana viumbe vyote vinavyo asili moja (common ancestry). Asili hiyo ilibadilika na kufanya viumbe kwa wingi tuuonao leo. Msingi hapa ni mabadiliko/evolution.

Chevalier de Lamark alikuwa mwanasayansi wa kwanza-kwanza kuonyesha uhusiano uliopo baina ya mahitaji ya kiumbe na mabadiliko ya mwili wake. Kwamba kiumbe hubadilika kutokana na mabadiliko yanayotokea katika mazingira yake. Mabadiliko hayo husababisha kubadilika kwa tabia zake, ambazo hurithiwa na uzao wake na hivyo kusababisha utokeaji wa aina nyingine ya viumbe ambavyo havikuwepo kabla.
\
Eti hii nayo iliitwa sayansi. Huhitaji darasa lolote kujua kuwa kinachosemwa ni uongo unaorembwa na kanuni zinazokubalika.
Miaka michache baadaye, akaja fyatu mwingine kwa jina Charles Darwin. Yeye akaja na nadharia nyingine yenye “akili” kidogo: Natural selection. Darwin alifikiri kule kuzunguka dunia na mashua yake ya The Beagle, basi kulitosha kuhalalisha madai yake kwamba viumbe vilitokea kwa bahati tu.

Hoja ya Charles Darwin
Viumbe havikuumbwa hivi tunavyoviuona sasa bali vilibadilika kutokana na mabadiliko ya kimazingira na hivyo kusababisha utokeaji wa aina nyingine ya viumbe na kupotea kwa baadhi ya aina ya viumbe. [Aina hapa ikimaanisha kundi la viumbe wanaofanana kiasi cha kuweza kuzaa kiumbe]

Kivipi?
Kwamba katika viumbe wa jamii moja, huwapo tofauti za msingi zinazomtofautisha kiumbe mmoja wapo na wenzake. Tofauti hizi husababisha tofauti za kukabiliana/kupambana na adha zitokeazo katika mazingira. Viumbe wengine hushindwa kupambana na adha hiyo na hivyo hufa, wakati wengine katika kundi hilo hilo hukifanikiwa kupambana na hivyo kuendelea kubaki kwa sababu ya “kuchaguliwa na asili yao” wenyewe. Hiki ndicho kinachoitwa Natural selection. 

Ushahidi alioutumia
Viumbe huzaliana kupindukia. Lakini ajabu idadi yao hubaki karibu ile ile.
Katika kitabu chake maarufu cha On the Origin of species by Natural selection or Preservation of Favoured Races in the Struggle for life, Darwin anaandika “As many more individuals of each species are born than can possibly survive; and as, consequently, there is a frequently recurring struggle for existence, it profitable to itself, under the complex and sometimes varying conditions of life, will have a better chance of surviving and thus be naturally selected. From the strong principles of inheritance, any selected variety will tend to propagate its new and modified form

Mimi sikubaliani na akili ya aina hii kama nitakavyoonyesha baadaye.

Maoni

  1. Tupo kijiweni, na tunasubiria Mkuu!

    JibuFuta
  2. Asante Simon.

    Nitahitisha hoja wakati wowote kuanzia sasa. Shule inakamata shati, nikiachiwa kidogo ninataraji kujikita katika saikolojia zaidi. Kuna mambo nadhani itafaa nikijitolea kuyajadili kwa kiswahili chembamba.

    Karibu sana

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Haiba ni nini?

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Uislamu ulianza lini?

Makundi Manne ya Tabia za Watoto Kitabia