Uhindu: Dini inayoamini dini zote ni sahihi!

Kwa muda sasa, pale Jikomboe/dini kulikuwa na mjadala kuhusu tofauti ya Dini na Imani ukiongozwa na mwanablogu Mwidimi Ndosi. Mjadala huo hatukuumaliza ili kuruhusu maoni ya wasomaji wengine. Kama unapenda mijadala hii, nakushauri upite hapa halafu uache maoni yako.

Wakati mjadala ukiendelea, na mara nyingine nje ya ukumbi, kuna wapenzi wa mijadala hii wanadai ipo haja ya kupeana habari zaidi kuhusu dini ambazo wengi hawazijui. Sababu ya kufahamika ama kutokufahamika kwa baadhi ya dini inaweza kuambatana na nguvu za kisiasa na kiuchumi za wasambaza dini husika.

Na ni kweli kwamba waumini wengi huwa hawajishughulishi na kujua dini nyingine zaidi ya hizo wanazoziamini. Siwezi kudai kuwa ninazijua sawasawa, ila ni kule kupenda kufuatilia hapa na pale na kuzungumza na huyu na yule, basi ninakuwa na japo kiberiti kidogo cha kutafutia wapi pa kuanzia na hapo wengine wanaongoza na matokeo yake tunavunja ile mila ya kutokujifunza mengi.

Wapo watu wanaodhani kuwa dini zao ndizo zilizo sawa kuliko za wengine. Na kwamba ili uende huko aliko Mungu, tunaambiwa ni mbinguni, basi piga ua lazima uwe mwanachama ama muumini wa dini yao. Tatizo linakuja: Kila dini inaamini kuwa yenyewe ndiyo bora na iko katika mstari sahihi wa kukupeleka kwenye raha ya milele, mbinguni. Na kila dini inalo la kukosoa katika dini nyingine. Hapo ndipo panakuwa na mtafaruku wa kiimani mpaka wengine wanaamua kuwa katikati.

Pengine hukuwahi kusikia sana kuhusu Uhindu. Uhindu unaamini tofauti kidogo na dini nyingi za kimagharibi. Nimekuandalia maelezo mafupi kuhusu dini hii ambayo ina waamini takribani Bilioni moja duniani. Bonyeza hapa kujua zaidi. Ukishasoma hapo, kesho nitakupandishia maelezo mafupi kuhusu Ubuddha.

Maoni

  1. Bwaya, hongera kwa kuamua kubeba mzigo mzito wa kutuelimisha kuhusu mada pana, ndefu, na ngumu kuhusu dini. Umeanza vyema na dini za Kihindu, Kibudha maana wengi wetu tunaposikia neno dini tunachofikiria ni uislamu na ukristo. Nami pale India nimeongeza ufahamu wangu juu ya dini hizi toka India. Maisha ni shule.

    JibuFuta
  2. Asante Bwaya kwa mada hizi

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Tabia za Mtoto wa Miaka 0 – 3 Kimahusiano na Kihisia

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Uislamu ulianza lini?