Ni lini tutajifunza kujifunza?

Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) ulikuwa na kasoro kubwa. Kasoro hizi zinaelezwa kujikita kuanzia kwenye utengenezwaji wake (in put) na utekelezaji wenyewe ambao ulileta matokeo yaliyotafsiri mpango mzima kuwa uliharibika.

Sirikali ya uwazi (utandawazi) na ukweli ililaumiwa sana kwa kutokuwasikiliza wananchi ambao ndio wadau wakuu wa haya yanayoitwa maendeleo ya elimu. Malalamiko yalielekezwa katika mitaala yenyewe iliyoletwa kinguvu nguvu kwa msukumo wa Bosi wa Elimu wa wakati ule, Yusufu Mungai. Mitaala ambayo mtu unashindwa kuelewa hivi ilikuwa inatetea itikadi gani na kwa maslahi ya nani.

Watoto wetu wakafutiwa masomo ya Historia, Uraia na Jiografia. Masomo ambayo yalikuwa yanajaribu kuwajenga moyo wa uzalendo watoto wa Kitanzania. Badala yake likaletwa somo linaloitwa Maarifa ya Jamii ambalo mumo watoto walijazwa maarifa ya mambo yanayohusiana na utandawazi na viwanda vya ulaya na mengine mengine ambayo kimsingi mtoto wa Mtanzania wa kawaida anayaona kuwa ndoto za saa saba mchana.

Watu walilalamika sana kokote walikopata pa kusemea, lakini salaalee! kama ilivyokuwa kawaida yake sirikali hiyo ilishikilia kuwa ilikuwa katika mstari sahihi katika kuboresha elimu nchini. Na kila aliyeendelea kuleta kisebu sebu yalimkuta yaliyomkuta. Bofya hapa kuendelea.

Maoni

  1. Ni sawa Bwalya. Kuna kujifunza, na kuna kujifunza kujifunza. Kujifunza kujifunza ni muhimu zaidi ya kujifunza.

    JibuFuta
  2. Afadhali sasa hakuna matatizo ya kuweka maoni.

    JibuFuta
  3. Na hasa kama kujifunza kujifunza huko kunatokana na makosa yaleyale uliyowahi kuyafanya.

    Kurudia makosa yaleyale maana yake, hata kujifunza kwenyewe kutakuwa hakupo.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Uislamu ulianza lini?

Zijue Tabia Nne za Kiongozi Bora Kazini

Tabia za Mtoto wa Miaka 0 – 3 Kimahusiano na Kihisia