Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba, 2022

Mwanaume anapokimbia 'kelele' nyumbani

Picha
  Mwanadamu ana uwezo mkubwa wa kuficha tabia. Samahani. Namaaminisha mwanaume. Unajua, katika jamii zetu, ni aibu mwanaume kukiri mahusiano yamekushinda. Kuliko kuitwa kila aina ya majina saa nyingine tunalazimika kujenga taswira ya ukamilifu hata kama kiuhalisia tunaugulia maumivu makali. Jumlisha hapo dini, kwa maana ya hizi itikadi za ufuasi wa halaiki, kiwango cha kuonesha ukamilifu lazima kiwe juu zaidi.   Tumeaminishwa ndoa ni kielelezo cha ukamilifu. Hakuna kukosea. Ukishasema una changamoto na mwenzako, watu wanakupiga jicho la dhihaka, “Hukumwomba Mungu akupe mke? Humtegemei Mungu vya kutosha?” Nani yuko tayari kuonekana hana uhusiano mzuri na Mungu?   Kwa upande mmoja, ninamuelewa sana Godi. Hofu ya kuchafua jina lake inamfanya aigize amani ya ndoa isiyokuwepo.   Swali nililojiuliza, kwa nini sasa Godi amefikia mahali hajali watu wa nyumbani kwake? Kama ana tatizo na mkewe, inakuwaje anashindwa kujali hata watoto?    Kila tabia, kwa kawaida, haikosi historia.  “

Usidanganyike. Wema huanzia nyumbani.

Picha
Umewahi kukutana na mtu mwema kiasi kwamba unawaonea ‘wivu’ familia yake? Unajiuliza, “kama huyu jamaa anaweza kuwa mkarimu hivi kwa sisi wapita njia tusiomhusu kivile, nyumbani kwake si watakuwa wanamfaidi sana?” Sasa usinielewe vibaya. Silengi kukukatisha tamaa. Ni vile tu nimeshangazwa hivi majuzi.   Godi ni rafiki yangu wa siku nyingi. Kwa hulka, ni mtu mchangamfu mwenye wingi wa bashasha. Kaa na Godi mzungumze utapenda namna yake ya kuzungumzia masuala. Godi anajua aseme nini wapi na kwa nani.   Halafu kuna wema. Godi hasubiri umtafute. Haipiti wiki hajakupigia na wala hatakuuliza kwa nini humpigii. Hivyo. Ukiwa na shida, Godi huyu hapa. Hana uwezo sana kifedha. Maisha yake ni haya haya kama ya wengi wetu. Sema ni ule utajiri tu wa roho ya mtu. Usha’nfahamu? Godi. Ukiniuliza mtu mwema nimewahi kukutana naye, nitakwambia Godi bila hata kupepesa macho.   Jamaa yetu mmoja aliwahi kumsifia kiutani lakini alikuwa sahihi. Kwa jinsi alivyo mwema, jamaa alisema, Godi anaweza a

Jinsi ya kumlinda mtoto na tofauti zenu

Picha
Simulizi la Renee limenikutanisha na wadau wa ushunuzi mjini Moshi. Tunapata kahawa jioni baada ya shughuli za siku. Hatujaonana muda. Tunasalimiana na kisha mada inageuka ghafla. Rebert anarejea mfano wa Renee, “Suala la mgogoro wa wazazi kumuathiri mtoto hilo halina mjadala.” Robert ‘anavuta’ kahawa kidogo kama mtu anayesikilizia ladha ya kinywaji cha moto sana na kisha anaendelea.   “Ukimsoma huyu dada ni dhahiri migogoro ya kifamilia ilikuwa na nguvu ya kuchora mwelekeo wa maisha yake ya kimahusiano.” Robert anasita. Wajumbe wamepotelea kwenye vioo vya simu zao. Kajihisi anaongea mwenyewe. Natingisha kichwa kumwitikia.   “Inasikitisha sana namna maamuzi yetu kama wazazi yanavyoweza kumnyanyasa mtoto kwa kiasi kile. Sitamani niwe mzazi nitakayemfanya mtoto awe na kazi kubwa ya kurekebisha tabia alizojifunza kwangu,” anajitahidi kujieleza Robert lakini kakatishwa tamaa. Wanaume hawamsikilizi wanacheka na simu zao. Hata mimi pia ninahisi huenda ninamsikiliza mwenyewe.   K

Usiyempenda anaweza kuwa baba wa mwanao?

Picha
  Watoto wanahitaji uwepo wa mzazi. Simulizi la Slaquara lilitukumbusha hakuna muujiza kwenye malezi. Mzazi unavuna ulichopanda. Renee anakazia funzo hilo. “Umeongelea athari za umbali kati ya mzazi na mwanae. Nayajua maumivu yake,” anasita na kufafanua, “Sikumbuki lini niliongea na mama yangu. Siwezi kusema ni adui yangu lakini sio mtu naweza kumtegemea kwa lolote.”   “Mara ya mwisho kuonana naye ni miaka miwili iliyopita alipokuja kusuluhisha mgogoro wangu na mzazi mwenzangu,” leso anayoitumia kujifutia inalowa machozi. Renee anaikunjua na kuigeuza kutafuta penye ukavu. “Nilimpa nafasi ya pili akaitumia vibaya. Badala ya kusikiliza upande wangu anielewe, aling’ang’ania kuwa upande wa yule mwanaume akinilazimisha kuishi naye. Hakutaka kabisa kuelewa kwa nini nilichagua abaki kuwa mzazi mwenzangu na si zaidi ya hapo.”   Mgororo huu mkubwa wa mzazi na mwanae umeanzia wapi? Renee anasimulia, “Nimekuzwa kama mtoto yatima. Nasimuliwa baba alipofariki nikiwa mdogo sana, mama alinipe

Usipompata utotoni, ukubwani atakutoroka

Picha
  Kuna umri ukifika maisha hudai vingi. Tunakimbizana na pilika za kuongeza kipato. Tunapambana na majukumu mengi kiasi kwamba wazazi tulio wengi tunakosa muda wa kuwa karibu na watoto. Ukaribu hapa ukiwa na maana ya kumsikiliza mtoto, kuelewa maendeleo yake na ha ta kujua nini kinausumbua moyo wake. Ingawa wazazi wengi tunaelewa fika kwamba watoto wanatuhitaji, lakini sasa tufanyeje na mambo yalivyomengi?   Simulizi la rafiki yangu Slaquara linaweza kukusaidia mzazi kufikiri upya vipaumbele vyako katika maisha. Katika mazungumzo yetu kuhusu familia, Slaquara ananisumulia jambo linalonishangaza kidogo:   “Mzee wangu analalamika sana kwamba siwasiliani naye. Namwelewa. Inaweza kupita hata mwezi mzima sikumbuki kuulizia hali yake. Kwa umri wake kusubiri kupata habari zake kupitia kwa mke wangu si sawa.” Namfahamu Slaquara kama mcha Mungu anayejali sana watu. Hili la kumtelekeza mzazi wake limekaaje?   “Hata sijui. Lakini ni kama sina kabisa habari naye. Hata tukionana huwa si