Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari, 2018

Tabia Tano Zitakazokupa Nidhamu ya Muda Kazini

Picha
Mafanikio katika eneo lako la kazi, kwa kiasi kikubwa, yanategemea matumizi ya muda ulionao kwa siku. Kile unachokifanya kati ya saa 6:00 usiku na saa 5:59 usiku wa siku inayofuata, ndicho kinachoamua utekelezaji wa majukumu yako.

Ukitaka Mwenzako Akuamini, Jifunze Kutanguliza Mahitaji Yake

Picha
PICHA: Merriam-Webster WIKI iliyopita nilitoa mifano michache ya namna ubinafsi unavyoweza kuwa na manufaa katika kutusaidia kupambana na hatari zinazotishia usalama wetu –kimwili na kisaikolojia. Nilisema ubinafsi pamoja na ukakasi wake unalenga kutusukuma kupata mahitaji yetu ya msingi. Jambo hili liliwahi kuelezwa na Abraham Maslow.

Tumetengwa na Watu ili Tuunganishwe na Teknolojia?

Picha
PICHA:  The Brown Daily Herald Ukisoma gazeti au kitabu, kuna mahali utakutana na ishara kuwa umefika mwisho hivyo utaliweka gazeti au kitabu chini, na kuendelea na mambo mengine. Vivyo hivyo unapoangalia filamu, unapofuatilia kipindi au taarifa ya habari kwenye radio au televisheni. Kuna mahali utafika utakutana na ishara kuwa sasa umefikia mwisho. Kipindi kimeisha, taarifa unayofuatilia imeisha, basi unapata nafasi ya kufanya maamuzi ya ama usibiri kingine au uendelee na mambo mengine.

Umuhimu wa Kusema Hapana kwa Ngono Kabla ya Ndoa

Picha
PICHA: eskimi.com Majuzi niliwaambia wanafunzi wangu wakitaka kuwa na ndoa bora hapo baadae, lazima wajifunze kuacha ngono kabla ya ndoa. Kusikia hivyo, walicheka mithili ya watu waliosikia kichekesho kipya cha mwaka. Sikushangaa. Kwa mujibu wa takwimu zisizo rasmi, wastani wa umri wa kijana kuanza ngono ni miaka kati ya 14 na 15. Wanafunzi wangu walikuwa na kati ya umri wa miaka 21 na 23.

Watu Wasikupotezee Lengo

Picha
PICHA:  Steemit Huenda kuna kitu kimekatisha tamaa leo. Huna matumaini tena. Kile unachokitarajia hakionekani kutokea. Umeanza kufikiri kubadili mipango yako. Ujumbe wangu kwako ni mfupi. Usikate tamaa.

Vitabu Nilivyosoma kwa Mwaka 2017!

Picha