Tabora wamemsamehe Lowassa, au ni dalili za kukubalika kwa UKAWA?

Matokeo ya utafiti mdogo uliofanywa na mwandishi wa makala haya katika mitaa ya mji wa Tabora jioni ya leo, umeonesha kwamba kuna ushindani mkali kati ya Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Ufisadi wa Richmond, Edward Lowassa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dk Wilbroad Slaa, kama uchaguzi mkuu ungefanyika kati ya saa 10 – 12:30 jioni hii. Matokeo hayo yanaonesha kwamba Lowassa ana asilimia 28 na Dk Wilbroad Slaa angepata asilimia 22.


Utafiti huo ulifanywa leo na mwandishi wa makala hii alipotembelea Manispaa ya Tabora kwa shughuli nyingine za kikazi. Lengo la utafiti huo mdogo lilikuwa kujua hali halisi ya kisiasa katika manispaa hii inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi. Kazi hiyo ilifanyika kati ya saa 11 mpaka saa 12:30 jioni siku ya Alhamisi ya Machi 5, 2015.

Methodolojia
Jumla ya washiriki wa Utafiti huu walikuwa 100, wanaume wakiwa 61 na wanawake 39. Aidha, washiriki 12 walioharibu kura zao ama kwa kuogopa kushiriki au kuonesha kutokujua kinachoendelea katika siasa, waliondolewa katika sampuli. Haikuwa rahisi kuzingatia usawa wa kijinsia katika idadi ya washiriki 100 waliokusudiwa.

Washiriki walipatikana kwa njia ya nasibu kwa kuzingatia vigezo kama umri, aina ya kazi anayoonekana kuifanya mshiriki pamoja na kujaribu kuwianisha jinsia ingawa haikuwezekana kwa asilimia 100. Washiriki waliganyika katika makundi kadhaa ya kikazi kulingana na walipokutwa na mtafiti.

Mtafiti alimchagua kwa nasibu mshiriki akiwa pekee yake. Na ikiwa mshiriki alikuwa kwenye kundi/au aliambatana na mtu mwingine, mtafiti alimwomba mshiriki faragha kwa kumhoji akiwa peke yake. Aliokuwa nao/aliyekuwa naye hakuhojiwa/hawakuhojiwa. 

Kadhalika, washiriki walipatikana kwa njia ya mtawanyiko kwa maana kwamba mshiriki aliyehojiwa baada ya mshiriki mmoja, ilibidi apatikane kwenye umbali wa zaidi ya mita 100 kuongeza nafasi ya mtawanyiko.
 
Uulizaji wa Swali
Mtafiti alijitambulisha kwa ufupi bila kutaja taasisi yoyote anayohusiana nayo. Kisha, alimwarifu mshiriki lengo la utafiti na kumtaka asitaje taarifa zake binafsi kulinda faragha yake. 

Kisha swali lililoulizwa kwa washiriki wote lilikuwa, “Ikiwa uchaguzi ungefanyika leo, na ukapata nafasi ya kupiga kura kumchagua Rais mpya wa Tanzania; Je, ungemchagua nani kama angejitokeza na kuteuliwa na chama chake kuwa mgombea?” Mshiriki aliongezewa ufafanuzi kwa kuelezwa kuwa kilichotakiwa ni jina na mtu na si chama na alihakikishiwa kwamba jibu lolote atakalolitoa litakuwa sahihi.


Matokeo

Matokeo ya Utafiti mdogo uliofanyika leo mjini Tabora. Chanzo: Jielewe

Washiriki 28, sawa na asilimia 28 walisema wangemchagua mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond, Edward Lowassa. Washiriki 22, sawa na asilimia 22 walisema wangemchagua Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakati washiriki 8, sawa na asilimia 8 walisema wangemchagua Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Professa Ibrahim Lipumba. Washiriki wengine 7, sawa na asilimia 7 walisema wangemchagua Waziri wa Ujenzi, John Magufuli

Hata hivyo, washiriki 21 sawa na asilimia 21 walisema hawajaamua au wanasubiri wagombea wafahamike rasmi.

Wanasiasa wengine waliopata kura kwa kutajwa, na asilimia za kura zao kwenye mabano ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (4), Tundu Lissu (2), Freeman Mbowe (2), James Mbatia (2) na Zitto Kabwe (2). Wengine ni Januari Makamba (1), Bernard Membe (1) na Samwel Sitta (1).

Ukomo na tafsiri ya Utafiti 

Matokeo ya Utafiti huu yananaakisi maoni ya washiriki katika mitaa ya Manispaa ya Tabora katika muda uliotajwa pekee. Hayawezi kutumika kuelezea hali ya kisiasa kwa maeneo mengine ya Tabora zaidi ya Manispaa. 

Kadhalika, matokeo haya yanaonesha kwamba upo uwezekano mkubwa wa mgombea atakayesimamishwa na UKAWA kuibuka mshindi kwenye Manispaa ya Tabora kwa kuzingatia idadi ya kura walizopata wapinzani. Hata hivyo, kuongoza kwa Edward Lowassa katika kura hizo kuna maana kwamba huenda wakazi wa Tabora hawana habari na kashfa iliyowahi kumpa mbunge huyo miaka michache iliyopita au hawachukulii kwa uzito kashfa hiyo.  
Aidha, kwa kuwa asilimia 21 ya waliohojiwa hawajaamua, ni vigumu kubashiri kwa hakika, ni mgombea yupi angeweza kushinda katika kipindi cha Utafiti. 

Vile vile, njia ya kuuliza swali kwa mdomo inaweza kumfanya mshiriki atoe majibu tofauti na yale ambayo angeweza kuyatoa ikiwa angeulizwa kwa maandishi au bila kuonana na mtafiti. Kuna uwezekano wa mshiriki kutoa majibu anayodhani yanatarajiwa na mtafiti ingawa jitihada zilifanyika kupunguza athari hiyo.

Swali linabaki kuwa, Je, wakazi wa Manispaa ya Tabora wanaangalia nini wanapofikiri mtu anayefaa kuwa Rais wao?

Utafiti huu ni matokeo ya shauku binafsi ya mwandishi wa makala haya kuelewa hali ya kisiasa mjini Tabora kwa njia ya kisayansi. Kwa namna yoyote ile, kusudi la utafiti huu, halihusiani na taasisi inayomhusu mwandishi wa makala haya. Shukrani za pekee kwa Justine Mwombeki, kwa ushauri  wake wa kitaalam.

Maoni

  1. Dewa Poker I think it's a good thing to do, how about you?
    Nowadays there must be a change for us all, therefore your article very useful thank you

    JibuFuta
  2. Greetings from Belgium, visit my weblog on: https://koivis.wordpress.com/

    JibuFuta
  3. Utafiti ni mzuri japo naona idadi ya uwakilishi katika jamii ya watu wa Tabora manispaa haitoshi kutoa hitimisho. Pia matokeo hayo yataathiriwa sana na mikutano ya kampeni za mwezi wa tisa zitakapoanza maana watanzania wengi ni wale wanaofuata matukio au mkumbo. Napongeza juhudi hizi endelea zaidi na mikoa mingine kama utakuwa na nafasi, especially Pemba. well done!

    JibuFuta
  4. I like it this blog information, thanks for sharing

    JibuFuta
  5. Menarik sekali topiknya, saya suka dan ingin sangat bermanfaat bagi saya. terimakasih banyak gan.

    Obat Herbal Radang Sinusitis Mujarab

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?