Pedagogy of the oppressed
Paulo Freire katika sura ya pili ya kitabu chake "Pedagogy of the Oppressed" anazungumzia dhana inayosisimua anayoiita "the banking concept of education" kama chombo kinachotumika kuwakandamiza wanyonge. Kwamba katika hayo yanayoitwa madarasa, wapo waungwana wanaojichukulia kuwa wanajua, hulipwa kwa kuwajaza wenzao "elimu" ambayo kimsingi ni chombo cha kuwakandamiza raia wanaoonewa. Freire anadhani hii si sawa kwa binadamu mwenzako kujiweka juu sana kiasi cha kuamua usome nini, na uache kipi (bila kujali mahitaji yako halisi). Anatoa mfano pale mwalimu anapoweza hata kupendekeza kwamba kitabu fulani kisomwe kuanzia ukurasa wa 10 hadi wa 15! Na eti anadhani anamsaidia mwanafunzi! Kwa mujibu wa Freire, elimu hii haiwezi kumkomboa mnyonge. Je, elimu yetu ina tofauti? Wanafunzi zaidi ya asilimia 50 "walishindwa" mtihani hivi majuzi, ni kweli walishindwa ama ni namna nyingine ya kuwakandamiza vijana wasio na hatia?