Safari zinavyotukutanisha na mengi

Nimekuwa na pilika pilika za hapa na pale. Sehemu kubwa ya muda wangu nikiutumia katika vijiji vyetu. Nilianzia Morogoro. Tukuyu. Kyela. Baridi ile mbaya. Watu wanalima kahawa wa kununua haonekani. Akiwepo basi bei ni ya kutupa. Mtu unajiuliza hivi ni lini wakulima watapata thamani sawa na watu wengine? Mwananchi anahangaika na mashamba ambayo hayamsaidii kujikwamua. Watu wamekata tamaa.

Ndugu zangu tuache kufarijiana. Wananchi wamekata tamaa. Majuma kadhaa ya mwezi Julai nimeyatumia Tunduma na Vwawa. Watu wanaishi maisha magumu sana. Wanajua kuwa nchi yao inazo hela, lakini zinaliwa na walafi wachache. Ukitaka kuijua Tanzania, usiishie dasalama. Vwawa na Mbozi panaweza kukupa picha ya nchi yetu.

Nikiwa Mbeya mjini nikajaribu kupandisha picha kwenye blogu, ikawa ngumu. Hata sijui palikuwa na nini hapo.

Nikiwa Ipogolo Iringa nako sikuweza kukaa na kuandika. Juma moja likaishia Dodoma nikiwa na heka heka nyingi kidogo. Nikadhani nikiwa Singida ningeandika. Wapi bwana. Singida ndio basi tena kila siku nikiwa "vijiani" manake kule hatuna barabara. Nikawa kijijini hata umeme hakuna. Yaani nguzo za umeme zinapita kwenye mapaa ya nyumba ajabu umeme kijiji kizima hakuna. Hiyo ndiyo Tanzania B. Singida kuzuri asikuambie mtu. Fika uone. Wananchi wanaipenda Checheme (Sisiemu) asikuambie mtu.

Hawana barabara. Maji safi hakuna. Huduma muhimu hakuna. Lakini ajabu Sisiemu ndiyo nambari wani. Naambiwa katika uchaguzi wa mwaka 2005, Singida ndiko Sisiemu ilikojizolea ushindi wa kifo (Manake sio Sunami tena). Naongea na vijana hawajui kinachoendelea. Wazee wangu ndio basi tena. Nikajifunza jambo moja. Nchi hii ina utulivu kwa sababu tu wananchi wake wengi hawaelewi kinachoendelea. Hawajasoma japo wanapenda kusoma. Serikali imewaacha walivyo ili iwatawale kiulaini.


Niko Moshi kwa sasa na naona bado sijatulia. Nitarudi.

Maoni

  1. Dah! watu wamekataa tamaa haswa hawajui kama kesho itafika.Nimegundua kitu kimoja wengi wa watu kule Tanzania B hawana elimu ya uraia.

    Wewe nafikiri umejionea hali ya "Singapore" ambapo CCM walijizolea mijikura kibao,lakini jaribu kuwaambia mbona CCM haiwatendei haki au imewasahau.Hawatakuelewa.Wanahitajielimu ya uraia.

    Wasalimie Moshi

    JibuFuta
  2. Ama kweli hatuna vita kwa sababu wananchi ni wajinga. Angalia juzi wananchi wameandamishwa sijui na nani kuunga mkono kitu wasichokijua.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Haiba ni nini?

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3

Uislamu ulianza lini?