Afrika: Bara linalokimbiwa na Waafrika wenyewe

Katika kujadili matatizo ya bara letu, watu wengi tumekuwa tukiwalaumu wazungu eti kwa kupora mali zetu. Nimesoma vitabu vingi vilivyoandikwa kuhusu Afrika. Nilichokiona katika maandishi ya wengi, ni malalamiko. Tunawalaumu wazungu. Hatusemi chochote kuhusu namna tulivyouchangia umasikini wetu wenyewe. Na inakuwa kama vile ukijaribu kuzungumzia upande wa pili, basi wewe si muungwana. Watu wanakutizama kwa jicho la marienge. Maandishi haya yanakusudia kugeuza kibao cha lawama. Bonyeza hapa kuendelea.

Maoni

  1. Nimekubali!Lakini nikaanza kujiuliza kama picha hii ya maendeleo iliyowekwa na hawa magharibi isingekuwepo, je watu si bado wangekuwa na kipimo kingine?Sasa tatizo la mfumo huu wa dunia tuna hakimu anayetumia kipimo kimoja tu hivi sasa. Kipimo hicho ndio kitufanyacho tupiganie kuwa kama magharibi. Wale wenye vipimo kama furaha ya watu wanaonekana wamezidiwa na wale waliojilundikia mali wakati hawana furaha. Wale waki sovieti na kichina ambao walitaka tu watu wawe sawa naona nao ndio hivyo wameshindwa.Tukirudi Afrika ndio hivyo hata kipimo cha kujiamini hatukifikii.Afadhali hata sasa tunaanza kuongelea haya mambo kiundani.Naamini bado tunaweza kugeuza mwelekeo.

    JibuFuta
  2. kijana umeshusha pointi sana. mungu akubariki kwa kusema ukweli bila uwoga. Ni wachache kama nyie mnajua ukweli ba mnaamua kusema. Tache ujinga wa kujidai mzungu ni adui yetu mkubwa. Wakituona kwenye televisheni tunapiga raia wetu wenyewe (Darfur) na kuwatawanyisha mpaka wanakosa malazi na chakula, huwa wanatuonea huruma. Wengine hata wanajaribu kuingilia kati kusaidia wasio na uwezo.

    Hawa viongozi wetu wakisema kuhusu unyonyaji wa wazungu tunatakiwa tuwe jasiri kuwauliza wanafanya nini kuhusu unyonyaji wa mwafrika kwa mwafrika?

    JibuFuta
  3. Niende wapi kaka! Nimeshikwa masikio kidogo nitarejea punde. Napitia kwako sasahivi kupibu!

    JibuFuta
  4. bwaya nimepita tu kwako na kuona 'hii maneno' sijaisoma. Nitasoma badaye.

    Kule kwangu uliandika kuhusu kufikiria masuala fulani pale ikifika 2010. Kahamu bado ninako.

    JibuFuta
  5. ni kweli wafrika tumefikia wakti wa kuacha lawama za ajabu ajabu eti atujaendelea kwa sababu wazungu walitunyonya,ebu angalia mfano wa Norway hii nchi ilikuwa chini ya utawala wa Danmark kwa muda wa miaka 400,na siku Danmark walipowaachia huru Sweden akawakamata tena kwa mika 100,hiivi nianavyooandika hapa ni kwamba tokea Norway wapate uhuru wao miaka 102 iliyopita sasa hivi ni matajiri wa pili duniani,na utajili wao umepatikana kwa jitihada zao miaka 50 iliyopita,sasa bongo tumekazania kila siku nchi eti bado changa hivi ni vichekesho maana sijawai kumuona mtoto mchanga mwenye umri zaidi ya 30,bora wangesema nchi bado kijana kidogo ningewaelewa.na ule usemi esemao kijana ni taifa la kesho ni bora tuufute kabisa kwani kijana na Taifa la leo kesho atakuwa mzee. ommy pengo

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Haiba ni nini?

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3

Uislamu ulianza lini?