Tumeiachia teknolojia itulelee watoto wetu?
Picha: reviewed.com Jijini Dodoma. Jioni ya Jumatano. Kikombe cha kahawa kinanikutanisha na maswahiba Gwamaka na Dk Mugisha. Tumezungumza mengi. Kisha mada inabadili uelekeo, “Unajua nikiangalia namna hawa wadogo zetu wanavyoyachukulia mahusiano sipati picha itakuwaje kwa watoto wetu.” Mada mpya ya malezi inachukua nafasi yake. Dk Mugisha anakiita kizazi hiki generation X , kumaanisha kizazi kilichozaliwa kwenye teknolojia. Kawaida, kila kizazi huona kilikuwa afadhali kuliko kizazi kinachofuata. Hata wazazi wetu, kimsingi, walikuwa na wasiwasi na sisi. Lakini ni ukweli pia kuwa mabadiliko makubwa ya kiteknolojia tunayoyashuhudia hivi sasa yamebadili kabisa namna tunavyoishi na kuchukulia mambo. Gwamaka anaona huu urahisishwaji wa kupata taarifa umeunda tatizo jipya tunalohitaji kulitazamwa. “Teknolojia imerahisisha mno watu kuyatangaza maisha yao mitandaoni. Tunajilinganisha mno na kuyatazama maisha kwa mizania ya vitu. Hili linaweza kuwasumbua sana vijana wanaochipukia hivi ...