Wanablogu wanasemaje kuhusu utaratibu wa "Kutuzwa"?


Tangazo lilianzia hapa kwamba kuna mwuungwana -japo hakuwa anafahamika jina lake wala mahali aliko- kapata wazo la kutunuku kazi za wanablogu. Huenda hili bado halijulikani kwa wanablogu wengi kama ilivyokuwa kwangu kabla ya kusoma posti ya mwanablogu matata, Bw. Mubelwa Bandio juma lililopita.

Blogu ya mwandaaji wa Tuzo hizo inajinadi kwa maneno haya:

"...Our wish is to help bloggers to success, beat the odd and push past their limitation. We believe bloggers can play an important role keeping their places, villages, towns, cities or countries visible.
Tanzanian Blog Awards is another opportunity to showcase your blog to the world and get some free traffic and subscribers..."


Pamoja na kupongeza wazo hilo (la kuandaa tuzo kwa wanablogu), Mubelwa Bandio alionyesha wasiwasi wake ikiwa zoezi hilo litafanyika katika mazingira ambamo masuala ya msingi kuhusu blogu hayajafanyiwa kazi. Kwamba blogu zinaeleweka vyema kwa wadau (wateuzi na wateuliwa), hilo lilimtia mashaka. Je, ni kweli blogu pamoja na malengo yake, zinafahamika? Je, wanaouchagua "ubora" wa blogu, wanatumia tafsiri gani? Umaarufu ama maudhui?

Hoja nyingine ya Mubelwa ni ushirikishwaji wa walengwa. Mubelwa anashauri ingelikuwa bora kila mwanablogu angelijulishwa kinachoendelea:

"Ni vibaya kusema ni tuzo za blogu bora ilhali wapo wanao-blogu na hawajui kuwa kuna tuzo. Kwa hiyo waandaaji watafute orodha ya blogu zote ili kuhakikisha mnazijua.
Ninalopendekeza ni kuwa bloggers wote waandikiwe emails na kuuliza kuhusu CATEGORIES za blogu zao ili kuhakikisha kuwa kila blog inatambulika kuwa iko kwenye CATEGORY gani na kama itapendekezwa katika category isiyo, basi irekebishwe. Ni lazima blogs ziwekwe kwenye sehemu husika ili thamani ya tuzo iendane na category yake."


Zaidi ya hayo, Ndugu Mubelwa alihoji nafasi ya umoja katika zoezi hili. Soma zaidi hoja hizo kwa kirefu hapa.

Pamoja na maoni hayo, Mubelwa anaamini ikiwa ipo haja basi ya kutoa tuzo kwa mwanablogu yeyote Tanzania, ni vema kumpa heshima anayostahili Bw. Ndesanjo Macha, mwasisi wa blogu nchini. Itakumbukwa kwamba Ndesanjo Macha ndiye Mtanzania aliyetia kiberiti cha kwanza kuwasha moto wa blogu unawaka hivi sasa (kiasi cha wengine wetu kufikiria "kuzitunuku") kupitia jikomboe.blogspot.com aliyeianzisha mwaka 2004. Heshima kwa kwake.

Akijibu baadhi ya hoja zilizotolewa na Bw. Mubelwa Bandio, mwandaaji wa Tuzo hizo alianza kwa kubainisha kwamba hakubaliani na hoja zote hizo.

Kuhusu kushirikisha wadau wa zoezi lake, mwandaaji anasema:

"...unavyosema sijui tuwaandikie watu watueleze blog zao zinahusu nini. Kwa taaarifa yako kuna watu wengi wanablog lakini hawajui hata blog zao zinaelekea wapi. Kuna maswali tumetuna na kuna wengi wamesharudisha lakini nakwambia ni kama 50% ya waliorudisha mpaka sasa hivi hawajui blog zao zinahusu nini au wasomaji wa blog zao ni nani...Hivyo baada ya watu kuwakilisha blog zao tutakaa chini kuona kama kila blog iliyopitishwa inastahili kuwekwa katika hiyo category.".

Kuhusu umuhimu wa wahusika (wateuzi na wateuliwa) kuzifahamu blogu na dhima yake kwa jamii, mwandaaji anasema:


"
...unavyosema kabla ya tunzo kwanza tufundishane umuhimu wa blog kwa jamii…hilo sitakubaliana na wewe kabisa kwa vile mpaka leo kuna filamu hazina maudhui yeyote katika jamii zaidi ya kufurahisha tu. Na hilo utalikuta kwenye blog nyingi tu, sio zote zitakua za kufundisha jamii kuna blogs ambazo zitakua zinafurahisha tu lakini zote zitashirikishwa katika mashindano... Na sisi hapa hatutalazimishwa na mtu yeyote ni wajibu wetu kuiweka award yetu katika kiwango cha juu. Na uzuri wa award yetu ni kuwa watu wanaosoma hizi blogs ndio watakao chagua wenyewe... hapa kwetu ni people’s choice hata yule mtu ambaye amejitahidi sana kujitangaza na hakuonekana tunampa jukwaa la kuonekana."

Zaidi bonyeza hapa kusoma majibu hayo neno kwa neno.

Baada ya kukutana na habari za harakati za kuandaa tuzo hizo kwenye blogu ya Ndg. Mubelwa Bandio na ukurasa wake wa Facebook, baadhi ya wadau walikuwa na maoni yafuatayo:

Ndugu Baraka Mfunguo anashuku harakati hizi za kuandaa Tuzo na kuziunganisha na dalili za ufisadi:

"...Nadhani hajatoa majibu zaidi ya kuitetea hoja yake(yuko zaidi defensive). Kiukweli wazo la kuwa na tuzo ni zuri lakini ni vyema kila mtu akashirikishwa. Na pia ni vizuri kitu kama hicho kikawa wazi. Hata hivyo hoja ya kusema kwamba ni tuzo ...hilo zimetolewa kulingana na matakwa ya kundi fulani (wanabloga wanaokutana Dar) Si la msingi. Na hapa ninaamini kuna mbegu ya ufisadi inayopandikizwa ambayo inakuja kuleta mgawanyiko. Wapo wale wenye pesa ambao wanautumia mwanya huo kuwalaghai baadhi ya watu na baadaye kuwagawa na kundi lingine la watu. Matokeo yake ni chuki dhidi yetu lakini yeye anajua alichopata kwa makusudi anayoyajua."

Mfalme Mrope, mwendeshaji wa blogu ya Je, huu ni uungwana anahoji mchakato mzima:

Nani yuko kwenye kamati ya kuteua hizi blogs na ni nani mpiga kura na pia mpendekezaji ni nani na tangazo la hii kampeni lilitolewa lini? na ati? Michuzi iko kwenye best designed blogs?? HUH?

Yasinta Ngonyani, baada ya kunukuu kauli mbiu ya mwandishi wa makala hiyo, anahoji ni akina nani walifikia uamuzi huo:

Naungana na kaka Mrope nani alipiga kura? na nani aliamua kila kitu?...

Sophie Kessy anadhani wanablogu hatupendani na ndio maana tumeshindwa kuwa na umoja:

"Ni kweli hatuna umoja wana blogger hatupendani twachukiana na kupigana vikumbo ufanyike mkutano wa kuelimishwa kuwa wa moja mengine baadae kama imeweza kufika mahali wakateuliwa wana blog bora bila wengine kufaham lolote katika jambo hili kubwa linalo wahusu? mpaka hapo hakuna umoja wala ushirikiano hamuoni kuwa dalili ya mvua ni ma wingu?...cha msingi ni kwamba vigezo gani vinatumika washiriki wanatambuliwaje? wanachaguliwa kwa mtindo gani mpaka kushinda. ndugu zangu waandaaji ni vyema kujenga msingi ulio imara na bora wa umoja na ushirikishwaji tusije onekana wale wale ni mtazamo wangu mniwieradhi."

Prof. Masangu, mchambuzi mahiri wa masuala ya kijamii na kisiasa alikuwa na haya ya kusema:

Mimi nilipoona tangazo hili wala sikutaka kusema cho chote. Ingekuwa vizuri hao waandaaji wakajaribu kuwasiliana na wanablogu wote ili tukashirikishwa.

Kamala Lutanisibwa anashuku zoezi hilo analodhani linafahamika zaidi kwa watoa fedha kuliko walengwa (wanablogu):

"...wafanye wafanyavyo. sina cha kusema. Tanzania tuna utaratibu wa kutumia watu kupta miradi yetu. Angalia hata NGOs. Ziko NGOs za kushughulikia watu kibao lakini zinajulikana zaidi kwa watoa fedha kuliko walengwa. haka ni kaujanja ka wajanjakujinufaisha..."

Malkiory Matiya, mwanablogu wa Sauti ya mnyonge alifikia kutilia shaka malengo ya tuzo hiyo:

...Inashangaza kuona blogs ambazo ni chachu katika kuelimisha watanzania popote pale duniani, ndizo zimepigwa chini. Na zaidi ya yote zile blogs ambazo hufanya uchambuzi yakinifu katika masuala ya siasa, utawala bora nazo zimepigwa chini. Kuna kila sababu ya kutilia shaka Lengo, nia, madhumuni na vigezo vya tuzo hii.

Sambamba na Mubelwa Bandio, mwanablogu mwingine mkongwe Bw. Kamala Lutatinisibwa naye anaandika waraka mzito akiuelekeza kwa muandaaji wa tuzo hizo. Katika maandishi hayo, mwananablogu huyo anaonyesha mashaka yake kuhusu nia hasa ya hao wanaoandaa tuzo hizo kimya kimya pasipo kuwashirikisha wadau. Kamala anaenda mbali kwa kuhisi kwamba wanablogu sasa wanaanza kutumika kama daraja la watu kufikia malengo yao!

Kamala ana wasiwasi na namna blogu mpya zinavyochukua nafasi kuliko inavyotarajiwa.
Anasema:


"
sasa wamegroup bloggs vile waonavyo wao ndivyo visitahirivyo awards na sio kiuhalisia. blog mpya zimeshika nafasi nyingi za awards, sijui ni watu gani walikaa na kuamua walivyoamua. ni awards, ni tunzo 'kwetu ma-bloggers' japo kuwa hatujui hasa ni nani kapangilia na kuamua kutoa hizo tunzo"

Bofya hapa kusoma post hiyo.

Naye mwanablogu Yusuph Mcharia wa blogu ya Mtayarishaji, aliweka ufafanuzi alioupata kutoka kwa muandaaji huyo.

Alihoji ikiwa blogu ambazo ndizo msingi wa Tuzo hizo zinafahamika kwa anayeratibu zoezi hilo na ikiwa ipo nafasi ya Jumuiya ya "ma-blogger" katika zoezi hilo.

Majibu ni haya:

Blog zinazowekwa hapa tunaletewa na watu na zingine tunatafuta wenyewe. Hili shindano ndio limeanza na tuna kama week tatu tu. Hivyo bado tunajitahidi kutafuta blog ambazo hatujaweza kuzipata basi tuziweke humu. Na blog hizo sio lazima ziandikwe kwa kiswahili bali ziwe zimeandikwa na Mtanzania yeyote pale alipo ulimwenguni.

Kuhusu nafasi ya umoja wa blogu hizo wanazozishindanisha;

"...Sisi hatupo katika umoja wowote na wala hatujapata mwaliko wa umoja wowote. Hivyo kujibu maswali yako sitaweza kwa vile hatupo kwenye umoja wowote wa bloggers wa kitanzania wowote ule."

Unaweza kusoma majibu kamili ya mwandaaji huyo hapa kwa hisani ya Mtayarishaji.

Una maoni gani na zoezi hili kwa ujumla? Kuna tunachoweza kujifunza namna wenzetu wa hapo Kenya wanavyoweza kuendesha zoezi kama hili?

Tazama namna walivyoendesha zoezi lao mwaka 2006, ambapo Mtanzania mwenzetu, baba wa blogu za Tanzania Ndesanjo Macha alishinda Tuzo hizo. Je, kuna ladha ya wanablogu wenyewe kupitia Jumuiya inayotambulika ili kuendesha zoezi hilo kwa uwazi unaotakikana na hivyo kuondoa hisia zisizo za lazima kwamba "kuna jaribio la kutaka kuwatumia wanablogu kuijipatia kipato"?

Jielewe, usisubiri Kueleweshwa!

Maoni

  1. Huu ni waraka wa kusambazwa. Kaka umefanya kazi kubwa sana kukusanya na kuweka mantiki ya maswali.
    Kubwa kwangu ni kuwa KWANINI MTOA TUZO HAJULIKANI NI NANI NA ANAKAA WAPI?
    Kwanini wanaotoa maoni wawe Anonys pekee? (nahisi ni yeye mwenyewe anayekuja na maoni ya sifa)
    Kwanini TUZO ZITEULIWE NA WATU WASIOJULIKANA? Katika majibu yake kwangu amesema "Na unavyosema sijui tuwaandikie watu watueleze blog zao zinahusu nini. Kwa taaarifa yako kuna watu wengi wanablog lakini hawajui hata blog zao zinaelekea wapi. Kuna maswali tumetuna na kuna wengi wamesharudisha lakini nakwambia ni kama 50% ya waliorudisha mpaka sasa hivi hawajui blog zao zinahusu nini au wasomaji wa blog zao ni nani."
    HAPA NDIPO NINAPOWAZA kuwa KAMA MTU HAJUI ANAANDIKA KUHUSU NINI, NA ANAMUANDIKIA NANI, NI KWANINI AWE NA TUZO?
    Naungana na Kaka Kamala kuwa HII NI BIASHARA

    JibuFuta
  2. Ahsante kaka kwa kuligundua hilo, huu ni waraka wa kuusambaza kama alivyosema Mubelwa ili kila mwenye jicho aone/some...mwenye ufahamu hata kosa la kuamua.

    Kinachonishangaza pia, iweje jambo lianze ghafla tu tena kimya kimya? Hata mfumo wa majibu yake kila ninapoyasoma tena na tena napata picha kuwa kuna jambo nyuma ya pazia.

    JibuFuta
  3. Yale yale...nashukuru wanablog wameligundua hili mapema, ...nahisi nii ile ile ya `umeshinda billioni kadhaa, toa anuani na account namba yako...' mwisho wa siku kila kitu kipo wazi...
    Sijui , kama kuna ukweli hapa, kupo upo waandaji wajiweke wazi...!

    JibuFuta
  4. Tuwenii macho na vitu kama hivi, sidhani kuwa tulianzisha blog zetu ili tupate hizo zawadi.
    Ok, labda ni tuzo, na kama ni tuzo, hawo waandaji wapo wapi, na ni akina nani, na masharti au vigezoo vya hizoo tuzo ni vipi
    Tuelewe kuwa nyanja hii ya mawasiliano imegubikwa na sintofahamu nyingi, wapo ambao kila kukicha wanabuni mbinu za kupata kwa kutumia migongo ya watu.
    Hatuna uhakika na hili, kama lipo na watu wana nia njema, waweke wazi, sio mbaya mkawajali wanablog...cha msingi mjue kuwa wengi wa wanablog ni wapiganaji kwa ajili ya manufaa ya jamii, sio kwa ajili ya biashara au zawadi, kama zipo tutashukuru, sio mbaya.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?