Kitabu hiki nilikisoma mara ya kwanza mwaka jana. Yeye mwenyewe alinielekeza mahali pa kukipata baada ya kuwa amesoma mjadala uliomhusu kwenye blogu hii baada ya kusemekana kuwa Padre Karugendo alikuwa "amevuliwa" upadre. Nilijifunza mengi kuhusu dini. Pengine unaweza kujiuliza; Kwa nini aliandika kitabu hiki? Pamoja na kukieleza kisa kizima kilichosababisha yeye "kufutwa" upadre kupitia tangazo la gazetini, Padre Karugendo anasema katika uk. 22: "...lengo zima la kutafakari kwangu na kukushirikisha wewe msomaji, ni kutaka kujenga utamaduni kama ule wa kule zilikotoka dini hizi za kigeni. Utamaduni wa kuamini kitu unachokifahamu vizuri, unachokitafakari, kinachogusa maisha yako ya jana, leo na kesho. Imani inayojenga historia yetu - historia ya Mungu na watu wake wa taifa la Tanzania!" Pamoja na hilo, Padre karugendo anasema kwa sauti kubwa kabisa kwamba, "Si haki Maaskofu kukemea ufisadi ndani ya serikali na kuacha ufisadi unaoendelea ndani y...