Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari, 2011

Ninapoahirisha mafanikio yangu kwa "kukwepa" kuamua

Mambo mengi yenye matokeo mazuri, si rahisi kuyafanya. Hasa ikiwa utekelezaji wake unadai utashi, “usilolazimishwa” na mamlaka iliyo nje na mtu mwenyewe. Ugumu wa mambo haya, ni zile zinazoonekana kuwa gharama za papo kwa hapo, zinazoweza kutukwaza tukate tama ya kufanya yale tuyapendayo. Matokeo ya haya yote, ni kujikuta tukiishi maisha yasiyo na utimilifu. Maisha yasiyo yetu. Pengine uliwahi kusoma maneno ya mtu mmoja aitwaye Albert Gray yanayosema: The successful person has the habit of doing things failures don’t like to do. They don’t like doing them either necessarily. But their disliking is subordinated to the strength of their purpose. Nukuu hii imekuwa na maana tofauti kwangu. Kwamba kile ninachokiona kwamba kana kwamba hakivutii kukifanya, ndicho chaweza kufanyika utimilifu wa ninachokikusudia. Mambo gani ambayo unajua ni ya muhimu yafanyike lakini unayaahirisha? Ni mangapi mazuri unayakosa kwa kule tu kukwepa kulipia gharama ya kuyatekeleza hayo unayoyaona kuwa ni

Katuni husema vingi! Tazama hii.

Picha
Kazi ya mchora katuni, Fede wa http://artsfede.blogspot.com

Je, jamii ingekuwaje bila dini?

Picha
Hebu tutafakari ingekuwaje bila dini. Ili kusaili hali hiyo ya kufikirika, hebu tuyasaili masuala haya kuona ikiwa dini inatufaa ama ndilo tatizo linalotukabili. Je, dini zinamsaidia binadamu kumjua Mungu? Je, bila dini tunaweza kuwa na uhusiano na Mungu? Je, dini zinasaidia kujenga jamii ya watu waadilifu na wanyoofu? Je, dini zinawasaidia waumini wa dini moja kuheshimu mitazamo ya waumini wa dini nyingine? Je, dini zinasaidia kujenga upendano katika jamii? Je, dini zinapunguza unafiki katika jamii? Je, dini zinapunguza migongano na misuguano katika jamii? Dini ni nini? Ni kumjua Mungu? Ni chama cha wanaomtafuta Mungu? Dini na imani vinauhusiano? Kwa nini dini? Mimi nafikiri tatizo ni dini zenyewe na sio watu. Wewe unafikiri nini? Tungekuwaje bila dini? Jumapili njema.

Unajua wanyaturu walipangaje uzazi?

Yapo mambo mengi katika jamii zetu yaliyofanyika zamani ambayo tukiyatazama twaweza kujifunza mengi. Mengi ya hayo, si sehemu ya jamii za kisasa hivi leo, lakini yalekuwa na msaada wa namna Fulani kwa jamii. Katika jamii ya asili ya wanyaturu, kabila dogo linalopatika katika wilaya ya Singida (na kidogo manyoni), mahusiano kati ya baba na mama yalikuwa na sura tofauti sana na ilivyo leo. Wakati leo hii, wazazi kulala vyumba tofauti huchukuliwa kama ishara ya kufifia kwa mahusiano baina ya wawili hao, kwa Wanyaturu hiyo ilikuwa na maana tofauti. Kikawaida, wazazi wa Kinyaturu hawakupaswa kukaa nyumba moja (sio chumba kimoja, nyumba moja) ndani ya boma. Katika boma analojenga mwanaume kama himaya ya familia yake, alipaswa kuzingatia uwepo wa nyumba mbili ndnai ya boma moja. Baba ambaye ndiye mkuu wa boma, alilala na wanawe wa kiume katika sehemu maalumu ya nyumba inayojulikana kama "Idemu/Ikumbu". Nyumba hiyo ilijitenga pembeni na nyumba kuu alikoishi mama na wanawe wa