Msaada wa msamiati...

Baada ya kimya cha ukumbi huu kwa muda mrefu na mwendo wa 'kuibuka na kuzama' kwa sababu zilizokuwa nje ya uwezo wangu, sasa nimerejea rasmi. Tutaendelea kujadili, kuhoji, kuelimishana na hata kupotoshana inapotulazimu. Kumbuka huwezi kuelimika pasipo kupotosha mtazamo ulionao.


Sasa nitangulie kuwaomba misamiati ya maneno haya kwa kiswahili fasaha:

ethics, ethos, morality na morals. Nayafahamu maneno haya vizuri lakini sina maneno husika kwa kiswahili fasaha. Sipendi ule mtindo wa kutumia sentensi nzima kuelezea neno moja. Naomba mnisaidie kuongeza msamiati. Nitafurahi kupata majibu hayo hata kwa barua pepe kwa watakaopenda kutumia njia hiyo.

Natanguliza shukrani za dhati!

Maoni

  1. kwa ufahamu wangu unaotokana na kitabu nilichodesa, morals ni maadili, ethics pia waswahili huita maandali lakini ukiangalia kwa kiigereza, ethics sio maadili bali ni nijia zakuyafikia maadili.

    hilo la ethos sijawahi kuliona popote ndo mara ya kwanza nalisoma hapa

    ila ikumbukwe kuwa hakuna maadili jumla ambayo kila mtu analazika kuyafuta / kuyaheshimu

    soma kitabu cha adolf mihanjo cha falsafa kutoka uyunani mpaka ugiriki

    JibuFuta
  2. Sijajiandaa kutoa maana halisi ya maneno uliyouliza, labda hapo baadaye.
    Karibu tena kwenye uwanja wa kuelimishana na kupotoshana pia! :-)

    JibuFuta
  3. Asante sana Kamala kwa mchango wako na pendekezo la kitabu.

    Chib, nasubiri mchango wako pia.

    Kuna neno jingine nitahitaji msaada pia sambamba na hayo niliyokwisha kuyataja: values!

    JibuFuta
  4. Habari za siku kaka,
    Karibu tena uwanjani, maan nili kumiss sana Bro!

    Kuhusu hiyo mada yako uliyoanza nayo, naona ni vyema tukiomba msaada kwa kaka John Mwaipopo.

    JibuFuta
  5. Asante kwa ukaribisho dada Koero. Tuko pamoja sana

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Uislamu ulianza lini?

Zijue Tabia Nne za Kiongozi Bora Kazini

Tabia za Mtoto wa Miaka 0 – 3 Kimahusiano na Kihisia