Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2010

Ubabe wa dini wa kuhodhi maarifa isiyonayo

Dini kama msamiati, inaeleweka. Lakini tafsiri rasmi naweza kusema ni vigumu kuipata maana inategemeana mara nyingi na matakwa, maoni, makusudi ya huyo anayetafuta maana. Wapo wanaotafsiri dini kwa kuhusisha na dhana ya Mungu kama msingi mkuu wa dini. Wengine wanatafsiri dini kwa kuihusisha na masuala ya ‘kiroho’ yaani spirituality, hisia na imani. Wengine wanaposikia dini mawazo yao yanakimbilia kwenye ‘vyama vya ushabiki wa kiroho’ yaani makanisa, misikiti, mahekalu na vitu kama hivyo. Inachekesha kwamba neno tunalolitumia mara zote, eti linatusumbua kulitafsiri. Sababu ni kwamba tafsiri sahihi yapaswa kuwa ile itakayotuwezesha kuzikusanya ‘dini’ mbalimbali kwa pamoja. Mkusanyiko huu hauwezi kufanywa kwa matumizi ya tafsiri ya dini fulani tu. Kwa maana hiyo, tunaweza kuzikusanya dini zote kwa kusema kwamba ni jumla ya imani zinazohusiana na vile tusivyoviona kwa macho, zinazojaribu kuleta majibu juu ya mikanganyiko ya maisha ili kuleta namna fulani ya matumaini ama ridhiko la

Mjadala wa dini na sayansi unaendelea...

Najaribu kupangilia mambo yangu niweze kujadili masuala ya dini wakati wowote kuanzia sasa. Wadau wa masuala haya ninawakaribisha nyote. Jana nilianza kwa kujiuliza swali kuu: Je, ni dini inaiogopa sayansi ama sayansi ndiyo inayoiogopa dini? Mdau wa mjadala huo, Profesa Matondo alikuwa na mchango huu wa kusisimua: ' ''Hili ni suala zito ambalo limehangaisha mafilosofa kwa muda mrefu sana. Kuna mambo ambayo sayansi haijaweza kuyaeleza. Dini kwa upande wake, kwa vile haihitaji vithibitisho kama vile sayansi, inaweza kujibu kila kitu kwa mwenye imani. Kuna mzozo mkubwa sana unaendelea hapa Marekani kuhusu ufundishaji wa nadharia ya Evolution ya Charles Darwin. Walokole wa hapa Marekani wanataka ama ifutiliwe mbali kufundishwa mashuleni au uumbaji (creationism) wa Mungu pia nao ufundishwe kama nadharia mbadala (alternative theory). Wanasayansi wanabisha kwamba uumbaji hauwezi kuthibitishwa kisayansi kama kweli ulitokea na kwa hivyo hauwezi kufundishwa mashuleni. Sij

Dini inaiogopa sayansi?

Nilitegemea kwamba dini na sayansi vingeenda pamoja. Kwa sababu nionavyo mimi, upo uhusiano mkubwa kati ya vitu hivyo viwili. Kwanza, vyote vinahusu maisha ya watu japo kwa namna tofauti. Lakini pili si lazima viwili hivyo vitengane ili kujenga heshima yake. Lakini ajabu, karibu mara zote tangu maendeleo ya sayansi maumbile yanaanza inaonekana wazi kuwa dini imekuwa kinyume nayo. Je, ni hali hii ni halisi au ni hisia? Je, ni dini inaiogopa sayansi ama sayansi ndiyo inayoiogopa dini? Nitafafanua nikirudi

Blogu mpya nyingine

Picha
Sogea karibu usome blogu ya Ndugu Renatus Kiluvia . Yeye ni mwandishi wa habari na mtangazaji wa kituo cha redio cha 87.8 Ebony fm cha Iringa lakini kwa sasa yuko kwenye studio ndogo ya Dar. Kwa mujibu wa maelezo yake mwenyewe, blog hiyo inahusu muziki na maisha katika nyanja tofauti-tofauti. Pia itahusika kuzungumzia burudani zingine kama filamu n.k. Bonyeza hapa upate kila kitu .

Stella mwanablogu mpya

Kila siku jamii ya wanablogu wa kiswahili inazidi kupanuka. Hivi sasa zipo blogu za kiswahili zaidi ya mia mbili na zinaendelea kuongezeka. Dada yetu Stella naye kajiunga na jamii yatu. Bofya hapa kumkaribisha , kuona maudhui ya blogu yake na pia kuendelea kumsoma. Dada stella, karibu sana.

Kutoka Maktaba: Ndesanjo unaombwa kurudi kundini

Picha
Katika safari ya kupitia kilichomo kwenye maktaba yetu, niliyoisemea kidogo jana, nilimfuma mdogo wangu anayenifuata, akirejea makala za mwandishi Ndesanjo Macha. Makala hizi ni zile alizoziandika kati ya mwaka 2005 mpaka 2007 katika magazeti ya Mwananchi Jumapili. Wakati huo mdogo wangu akiwa kidato cha tano na sita alianza kuzifuatilia kama matokeo ya mkumbo tu (pengine) lakini baadae ukawa ndio ugonjwa wake mpaka zilipotoweka ghafla zaidi ya miaka miwili iliyopita. Sasa akiwa anamaliza Chuo Kikuu mwaka 2010, makala hizo anazisoma kwa kupitia 'hifadhi' ya magazeti yale ya chumbani kwetu. Nimeshawahi kumkuta mwaka jana akiwa na vipisi vya safu ya "Rai ya Jenerali" vyenye tarehe za mwaka 1995 mpaka 2005 vikiwa vimeungamanishwa kwa pamoja na kufanya kitu kama kitabu fulani hivi ambacho alikuwa akitembea nacho kwenye begi lake. Kwa hiyo sikushangaa kukutana na shughuli hii ya kukusanya makala za Ndesanjo hivi majuzi. Picha hizi ni ombi maalumu kwa Ndesanjo M

Amana ya ‘nguvu zangu’

Picha
Hivi majuzi, nilipata fursa ya kula pasaka nyumbani kwetu, Singida. Katika niliyoyafanya, ni pamoja na kukagua ‘maktaba’ ambayo mzee wangu alitutengenezea chumbani kwetu. Ni kijishelfu kidogo ambacho alikitumia enzi hizo kutuwekea vitabu kadhaa kila mara na kutuhimiza kuvisoma. Pamoja na vitabu, humo aliweka nakala za magazeti ya Rai ile ya zamani na mengineyo. Na kweli tuliyasoma, mimi na mdogo wangu. Namshukuru baba yangu kwa hilo. Maana nakumbuka alinifanya nianze kugharamia nakala za magazeti tangu nikiwa kijana wa darasa la sita na saba. Niliweza kubana matumizi ili kumudu kununua gazeti hilo kila wiki. Ndio ulikuwa ulevi wangu. Pia nimshukuru kwa sababu alinijengea ari ya kuiba vitabu kila nilikopita. Ujue kila mtu hukumbuka siku zile za ‘adolesensi’ kwa jinsi yake. Wengine kwa idadi ya wasichana aliowatongoza. Wengine kwa michezo ya ‘baba na mama’. Na kadhalika. Mimi huzikumbuka zaidi kwa wizi wa vitabu. Sikuwa na uwezo wa kumudu kununua vitabu nilivyovipenda. Kwa hiyo