Vijana wengi hawana elimu ya uraia?

Ninablog nikiwa Singida.
Nimekuta harakati nyingi zinazohusiana na uchaguzi mkuu, utakaofanyika Desemba 14. Yupo Mhindi mmoja hapa anasumbua akili za watu kwa wingi wa hela alizonazo. Ukweli ni kwamba wananchi wa Singida wamekubali awe Mbunge wao si kwa sababu ya sera zake. Ni kwa sababu ya pesa! Hii ni ajbau maana ukimsiliza Mgombea huyu utashangaa kapita pitaje hadi kuteuliwa kuwa mpeperushaji wa bendera ya chama Kikongwe kama CCM? hajui kujieleza na akisimama anachokijua ni kutaja ahadi za miradi ya mamilioni atayoifanya akiwa Mbunge.
Ni wazi, nimegundua, Vijana wengi wa MJi huu na mkoa kwa ujumla hawana elimu ya Uraia. Wengi wanafuata mkumbo na hawajuai umuhimu wao kushirikji katiuika masuala ya siasa. Utakuta wamejaa kijiweni wakilaumu kwa nini huyu bwana (Mhindi) kapitishwa na chama chake awe mgombea...wanalalamika sana. Ajabu ni kwamba ukiwauliza kama wamejiandikisha kupiga kura, watakwambia "hilo halihusiani na wala si muhimu...kura moja itaathiri nini?"
Naam.Hiyo ndio Singida, mji wenye vijana wanaojua umuhimu wa kulalamikia wagombea, lakini wasiojua umuhimu wa kupiga kura!
Tatizo hili la kukosa elimu ya uraia haliko hapa SIngida tu, limeenea mahali pengi. Watu hajaelimiaka kuhusu siasa. Ndio maana ukiwauliza wazee wa hapa watakwambia kuwa "Kuchagua chama kingine cha siasa mbali na Chama hatamu, uanachagua vita!" Hizo ndio propaganda ziznazotumiwa kuwapoteza wananchi hapa.
Lakini naambiwa Mbowe amegeuza fikra za vijana wa mji huu na lolote linaweza kutokea kwa maana ya CCM kupoteza umaarufu hapa.

Maoni

  1. Watawala hufurahi sana wananchi wa kawaida na hasa vijana wanapokuwa hawana elimu ya uraia. Wanapokuwa hawajui nini kinaendelea. Wanapokuwa hawajui haki zao.

    Habari hii haijanishangaza ila inanisikitisha.

    JibuFuta
  2. Chris, huwezi amini jinsi nilivyofurahi na kufarijika mara baada ya kuingia kwenye hii blogu yako! nimeanza kukubaliana na wale wenzangu kuwa kama wanamageuzi wa ukweli hawajazaliwa basi ni hawajapewa nafasi! ninaona tofauti iliyopo kati ya vijana na wazee katika taifa letu! ninaona jinsi unavyojitahidi pamoja na ukapa wa kianafunzi kuingia kwenye internet kuamsha fikra. sisi wanablogu tunafikiria ni jinsi gani tutasaidia kutoa mafunzo ya uraia kwa wananchi, maana kile kituo cha haki za binadamu tuna mashaka nacho. inawezekana kabisa ni kitua cha kulinda haki za wawekezaji au watalii!! lakini jinsi ninavyoona mabo yanavyoenda, inawezekana kabisa tukapata walimu wengi sana wa madarasa ya uraia (makada) kila mkoa! hii ni dalili njema. (tulikubaliana kuwa ni vyema tukaalika wanachama wawe wengi ili merikebu ifike )pia ninaona kwenye hizi blogu tunazalisha maraisi na wabunge ambao kwa kweli tunawahitaji! penye nia pana njia. nilisoma pale global voices kuwa wanaglobu wameongezeka mara nyingi (sikumbuki asilimia ngapi) hadi kufika milioni na kitu ethiopia mara baada ya kuteswa na wenye nguvu kwenye uchaguzi uliopita.-ambao sijui hata kama matokeo yameishatangazwa. mimi nimeishafika ethiopia, bado simu za mikono ni za waheshimiwa - bado hazijachanganya, mtandao uko taratiibuu- na wa kuutafuta ile kishenzi!! na ni masikini sana! kazana sasa kuna kina kaka jeff hapa na wengine tunanoana. nimefarijika kusikia kuna kijana ana umri wa miaka 27 bungeni!! haya tuikosoe iliyo madarakani hayaaa!!! shot kulia kavimba mkia!!

    JibuFuta
  3. Heshima ifike kwako bwana CN!

    Imenibidi nichukue japo sekunde chache kukujulia hali wewe mwanaharakati uliye katika ardhi ya tanganyika na kukutia moyo katia kile unachosoma kwa sasa yaani UALIMU,FANI ILIYOTUKUKA!

    Nashukuru pia kama ulitambua ualimu ni fani yenye mchango mkubwa sana kwa maendeleo ya nchi yeyote iwayo na mimi siamini kua haina umaarufu!!!!

    Vita iliyo mbele yetu ni kukomboa wadogo,vijana wenzetu na ndugu zetu kifikra ili wawe chachu ya fikra chambuzi zinazojali maslahi ya bara letu hili.

    Nafasi uliyonayo kama mwalimu mtarajiwa naichukulia kama uwanja wa kuandaa wanamapambano wa kifikra.Nikipata fursa nitakuja mlimani tuongee na kujuana zaidi kwani kwasasa nipo zanzibar

    JibuFuta
  4. big up, no nio juu zaidi!

    kwa kipindi kifupi nimegundua kuwa bwana fikradhabiti yeye hupanga na kutekeleza. ni vizuri sana wanaglobu kuwasiliana kwa kutembeleana pia hata kula kitimoto pamoja! sasa hivi bwana makene naona amembana jeff hata makala hazionekani tena. naamini watatoka na kitabu huko waliko!

    cheers

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?