Jifunze Uhusiano wa Malezi na Vilema vya Haiba (Personality Disorders)

Kizazi chetu kinakabiliwa na magonjwa mengi yasiyoonekana. Tunaumwa, na wakati mwingine taabani, lakini hatujui kuwa tunaumwa. Tunatembea, tunakutana na watu, tunapiga picha zenye nyuso zilizochangamka, tunaonekana kufurahia maisha lakini tunateseka na mahangaiko mengi tusiyoweza kuyasema. Tazama kiwango chetu cha ukatili. Haiwezi kuwa kawaida, kwa mfano, kuona mwenzako anaumizwa na wala hujali. Unamuumiza mtu na bado unashangaa kwa nini analalamika. Unamtesa mwenzako kihisia na bado unamdhihaki anapougulia maumivu. Unajiuliza, tumefikaje mahali mwanadamu unaweza kumtesa mwenzako, ukamsababishia maumivu na hujisikii kujutia. Mbaya, wakati mwingine, kiwango hiki cha ukatili kinakuwa kama nyenzo ya kupata tunachokitaka. Tunataka madaraka, tunataka umaarufu, mali na kila kinachotufanya kujione tunnawazidi wengine. Tunakuwa waraibu wa ukatili dhidi ya binadamu wenzetu na hatujisikii kujutia. Tazama kiwango chetu cha ubinafsi. Kwa nini tumepoteza uwezo wa kuafikiria hisia...