NI VIGUMU kwa kijana aliye kwenye kilele cha msisimko wa mapenzi hii leo kudhania bashasha hiyo inaweza kabisa kugeuka kuwa hasira, uchungu, na kushuhudia ile shauku ya kuongea, kusikiliza, kutaniana na mpenzi wake huweza kupotea so naturally kwa jinsi hiyo hiyo mapenzi yalivyoanza. Aliyewahi kusema upo mstari mwembamba mno unaotenga mapenzi na chuki, alilitambua hili. Kwa jinsi msisimko wa mwanzo wa kimapenzi unavyokuwa-ga mkubwa, huwa haingii akili kwa kijana anaposikia kwamba wapo wanandoa huweza kuchelewa kurudi nyumbani katika jitihada za kujaribu kuyakimbia matatizo na wenzi wao. Kijana anashindwa kuelewa inakuwaje watu wawili wanaopendana kwa dhati, wanaweza kufikia mahali pa kutamani kuzungumzia matatizo yao kwa uwazi, lakini wasiweze, wakatamani kuwa karibu kihisia, wasiweze. Haya yote pamoja na kuwa mabaya kuyasikia, huweza kumpata mtu yeyote, tena mwenye mapenzi mazito, hatua kwa hatua. Mahusiano ni suala zito lakini linalowezekana Tunapoyasema haya, hatukusudii kum...