Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni, 2008

Ni kweli, Fossils, mabaki ya viumbe wa kale ni ushahidi wa Evolution?

Msomaji mwenye historia ya elimu ya viumbe anaweza kuuliza: Uhusiano tunaouona baina ya viumbe (phylogenetic relationship) una maana gani? Kusema kweli, viumbe wanaonekana kuhusiana kwa karibu. Na uhusiano huo unaleta mawazo kuwa huenda kila kiumbe ametokana na mwenzie. Kwa mfano inavyoonekana, maisha hasa ya viumbe yalianzia baharini. Kwa maana hii, viumbe wa kwanza waliishi majini wakibadilika badilika na kuishia kufanya aina nyingine ya maisha yasiyotegemea maji, yaani maisha ya nchi kavu. Sasa katika kuangalia mlolongo huu, tunaambiwa viumbe walijikuta wakijiongezea “viungo” (adaptive features) vilivyowawezesha kukabiliana na aina vyingine ya maisha. Kwa ule mfano wetu wa samaki, ni kwamba baadhi ya samaki walianza kupoteza uwezo wao wa kupumua kwa kutegemea maji, na badala yake, wakaanza kuwa na vitu kama mapafu vilivyowasababisha kugeukia maisha nje ya maji. Baadae makoleo yao yaliyotumika kuogelea (fins) yakatengenezeka kuwa (miguu?) ili waweze kuishi vizuri nchi kavu. Na

Ni kweli kuwa viumbe wametokana na mabadiliko 'ya kubahatisha'?

Tulichagua kutumia kanuni za Marehemu Charles Darwin kwa sababu ndiye aliyejaribu kujihusisha kwa kiasi kikubwa na asili ya mabadiliko ya viumbe kwa mtazamo wa kisayansi. Na kwa kuwa lengo letu ni kuitizama sayansi kwa jicho la haki, tunaona na ni vyema “kuweka kumbukumbu sawa”. Marehemu Darwin amejaribu kuonyesha kwamba viumbe vilitokea kwa bahati, vikapitia mabadiliko ya uasili wao kufanya asili nyingine iliosababisha kugeuka na kuwa viumbe vya aina nyingine kabisa. Ili kufafanua anachosema Darwin na rafiki zake, tuchukulie mfano wa viumbe kama samaki. Samaki, kwa mujibu wa kanuni ya “natural selection”, walipitia mageuzi kadhaa yaliyosababisha tofauti katika kundi lao la samaki. Tofauti hizi ziliendelea kuwa kubwa kiasi cha kusababisha kutengenezeka kwa aina fulani ya samaki waliokuja kufanya kundi la viumbe tofauti kabisa na samaki wengine waliobaki. [Kundi hili linafahamika kama amphibia lenye mifano ya viumbe kama mamba na vyura]. Maana yake ni kwamba katika samaki, walit

Sayansi na imani, mwendelezo

Niliandika mara kadhaa, nikijaribu kuonyesha matatizo ninayoyaona katika sayansi. Kusema kweli siandiki kudhihaki umaana na heshima ya sayansi. Ninaandika kuangalia kwa upya nafasi ya sayansi katika ulimwengu wetu kwa kutizama mipaka yake. Ningeomba msomaji awe mvumilivu tunapoelekea katika hitimisho la mjadala huu. Kama u msomaji mpya, unaweza kupitia hapa na ukaja hapa , kwa mtiririko huo huo ukasoma na hapa pia . Halafu tuendelee.

Urembo kikwetu, unakuwaje hasa?

Nilipodokeza kuhusu suala la mahangaiko ya akina mama na nywele, msomaji mmoja aliniandikia: " Mwanamke gani utaoa mwenye asili kamili ya uafrika?...". Nilimjibu. Katika kumjibu lilinijia swali kubwa: hivi mwanamke mrembo hasa ni yupi? Mrembo/mzuri kwa macho ya kiafrika yukoje? Ukisikiliza maoni ya wanaume wengi utaona namna ambavyo tumeathirika kufikiri kwetu. Utaona namna tusivyoipenda aisli yetu hata kama tunadai kuupenda uafrika kwa maneno yetu. Kwa wengi, mwanamke mrembo ni lazima awe mweupe kadiri iwezekanavyo. Awe mweupe peee hata kama ni kwa kulazimisha. Ndio maana kwa baadhi ya makabila mwanamke mweupe hulipiwa mahari kubwa zaidi ya mweusi. Mwanamke mrembo ni lazima awe mwembamba iwezekanavyo. Ndio maana wengine wanajikondesha sio kwa sababu wanaelewa umuhimu wa kupunguza mafuta mwilini, la hsha. Ni kwa sababu wanadhani ili wavutie ni lazima wakondeane. Kwa lugha rahisi mwanamke mrembo, ionekanavyo, ni yule awezaye kujipamba kwa kila kiwezekanachoo alimrad

Kwani akina mama wanatumia nywele za bandia? Ni ili iweje?

Kama kuna mambo ambayo huwa yanathibitisha kuwa waafrika wengi hatuoni raha ya kuwa waafrika ni hili la nywele za bandia. Wanawake wa kiswahili wanateketeza muda mwingi na fedha nyingi kutengeneza nywele zao ama 'kununua' nyingine zenye asili tofauti. Kwao huko ndio kupendeza. Ukibaki na za kwako ukazitunza zikawa nzuri, zikabaki za kiafrika, hujapendeza bado. Kwamba kwa kufanya hivyo wanapendeza ama vipi, hilo kwangu sio suala. Kinachonitatiza ni sababu ya kuzitengeneza ziwe na asili tofauti: Hivi ni kwa nini? Hawawezi kupendeza bila kubadili asili ya nywele? Si kwamba ni dalili flani ya kujiona mwenye asili duni kuliko watu fulani? Si kwamba hii ni dalili ya udhaifu wa kujielewa na kujiamini? Wewe unafikiri vipi kuhusiana na hili? Kwangu hii ni aibu moja wapo ya waafrika. Kabisa.