Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba, 2013

Tunawezaje kujinasua na matatizo ya msongo wa mawazo?

Hivi sasa imekuwa ni kawaida kukutana na mtu anayezungumza mwenyewe. Na si tu kuzungumza mwenyewe, bali hata kurusha rusha mikono huku na kule. Waweza kukutana na mtu anayetazama lakini haoni, anayesiki lakini hasikilizi, na anayesema asichojua anachokisema. Si hivyo tu. Imeanza kuzoeleka kukutana na mtu ofisini mwenye hasira za mafungu dhidi ya kila anayehitaji huduma yake. Hasira zinazoambatana na kufoka, kusema pasi mpangilio, na hata kutukana watu wasio na makosa ya moja kwa moja hovyo hovyo. Vile vile, ni kawaida kukutana na watu wenye ghadhabu katika sehemu za umma, kama kwenye usafiri wa wote, foleni za benki na kadhalika. Watu wanaonekana kuwa na hasira ambazo kimsingi chanzo chake si hapo alipo.  Hizi ni dalili za msongo wa mawazo. Na zipo nyingi. Kuyasema haya hatujaribu kuonyesha kuwa msongo wa mawazo/stress ni kitu kibaya moja kwa moja. Hapana. Kwa hakika kiasi fulani cha stress kinahitajika ili kutufanya tuhimizike kupiga hatua fulani. Hata hivyo, msongo huu ...

Kurudi Bloguni

Habari za miaka wapenzi wana-blogu. Tafadhali karibuni sana kwenye blogu yetu iliyokuwa mapumzikoni kwa takribani miaka miwili. Sababu za kupotea zilikuwa za kijamii na nje kabisa ya udhibiti wa kawaida. Sasa tunaweza kuahidi kuwa blogu yetu imerejea rasmi kwa nguvu mpya na mtazamo mpya tangu dakika hii. Na masuala ya kijamii yanayohusiana na mahusiano yetu na nafsi zatu pamoja na mahusiano yetu na wanaotuzunguka, tabia zetu, mitazamo yetu, na kadhalika, yataendelea kupewa kipaumbele kwa sura mpya zaidi. Karibuni sana.