Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei, 2012

Umemsoma Dambisa Moyo?

Picha
Kama una mpango wa kusoma kitabu kimoja tu mwaka huu, napendekeza hiki cha Dambisa Moyo kiitwacho "How the West was Lost". Ukikisoma utaelewa zaidi kwa nini hawa watawala wanaoitwa "The darling of the west" wanaopigana vikumbo kuhudhuria mkutano wa G8, wamepotea njia. Anacho kingine alichokiandika kabla ya hiki, kiitwacho cha Dead End, bado nakitafuta. Naambiwa ni moto.

Mafanikio ni umiliki wa muda wako

Picha
Mafanikio ni nini? Ajira ya uhakika? Uhakika wa mapato? Uhakika wa pensheni? Ongezeko la muamala mwisho wa mwezi? Tarakimu za shilingi kuongezeka? Kwa gharama ya kunyang'anywa muda wako? Si unajua? Kadri ziongezekavyo ndivyo uuzavyo muda wako? Mafanikio.... Ni madaraka kazini? Madaraka yaendanayo na ubize ? Kutwa u ziarani? U angani kikazi? Waondoka alfajiri, warudi usiku? Wanao hawakuoni? Mwenza yu mpweke? Haidhuru... Nyumba yanukia noti sio? Shilingi bila muda, kazi yake nini? Muda na familia ni sehemu ya mafanikio. Noti ziendazo sambamba na kukunyang'anya fursa hii, faida yake nini? | Picha ya blackmarriageworks.com/ Mafanikio... Ni kuongezeka kwa kibaba? Ankara zalipika kibaba kinabaki? Ni uhuru wa muda wako? Uhuru wa kujenga familia kwa karibu? Mwenzi achekelee? Wana wasome? Uifaidie jamii? Sadaka utoe? Wenye shida wakukimbilie? Si unajua lakini...? Bila shilingi hayo si mepesi? Shi...

Nani yu huru?

Picha
Wakurupuka alfajiri, haraka wende kazini Wajutia kuliacha shuka, waogopa kuchelewa Ukifanyacho kimepangwa, mpangaji ni mwajiri Muda ulohisi wako, ukweli si wako Mwajiri kaununua nira kakufungia Wajisifu na ajira? Mwajiriwa akilinda kibarua chake | Picha ya picturesof.net                                       Uhuru ni nini na aliye huru ni nani? Aliyehuru hufugwa na mwingine, ati? Aliye huru yuna muda Cha kufanya akipanga yeye, pa kwenda haamrishwi Huenda atakako kwa hiari ya muda wake Hupata mkate wake pasipo mauzo ya muda wake U huru? Mtumwa aongozwa na bwana wake Hiari na aendako hanayo Kazini ni lazima Ujira huupata kwa kuuza uhuru wake Hana mamlaka na muda alodhani wake Muda wake kauuza kwa mwajiri Nira kakabidhiwa Mabega yote j...