Watu wanapata taswira gani wanapokutazama?
Binadamu anao uwezo wa kujenga taswira yake - namna anavyoonekana - kwa wengine kwa kadiri apendavyo awe. Binadamu anaweza kuamua kuonekana mtu wa heshima zake, ama hata kuonekana mtu asiye na heshima zake. Uamuzi wa kujenga taswira hiyo, self-image kwa msisitizo, uko mikononi mwake yeye mwenyewe. Kwamba tunafikiri wengine wanatuchukuliaje ni suala la kujenga taswira zetu. Kwamba zaidi ya kule kujitathimini wenyewe, kujiangalia kwa macho yetu wenyewe, tunajaribu kujitazama kwa macho ya watu wengine. Tunajaribu kujifikiria kwa miwani ya wanaotuzunguka. Tukijiuliza swali kubwa: hivi huyu jamaa ananionaje hapo alipo? Self-image. Si tu kujiaminisha kuwa tu watu wa aina fulani kwa kutumia vigezo vyetu, bali kujaribu kurudusu, wengine wanatuonaje. Hatuwezi kujifahamu sisi ni akina nani kwa kujiangalia kwa macho yetu wenyewe. Macho yetu hutudanganya na mara zote hutafuta kutupendelea. Macho yetu hutafuta kutufanya tujisikie vizuri kuhusu nafsi zetu. Hivyo, tunapotaka kujifahamu kwa usahi...