Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei, 2007

Self-Esteem: Ni muhimu kwa mwanao

Ninaanza na kukupa hitimisho: Mzazi anayo nafasi muhimu sana ya kumfanya mwanae ajenge fikra-chanya kuhusu maisha yake mwenyewe zitakazomfanya ajiamini. Na mzazi huyohuyo asipokuwa mwangalifu, anaweza kumsababishia mwanae fikra-hasi na hivyo kumfanya ajione duni. Kujenga fikra chanya kwa mwanao si kazi rahisi sana. Ni kazi ngumu inayodai muda wa kutosha wa mahusiano ya karibu kati ya mzazi na mwanae. Kazi hii haifanywi na wazazi wengi ambao huzaa pasipo kuhesabu gharama za uzazi husika. Hii ni kwa sababu kitendo kinachosababisha uzazi huwa hakihesabiki kama kazi. Kitendo hicho hufanyika katika mazingira ya starehe ya tamaa ya mwili kiasi kwamba wapenzi wengi huwa hawafikiri zaidi ya tamaa hiyo. Kwa maana nyingine, inaweza kukubalika nikisema kuzaa si kazi. Ndio maana hata wahenga walilonga: Kuzaa si kazi, kazi ni kulea. Kila mmoja wetu anaweza kuzaa akipenda. Ndio maana unawafahamu wasichana wadogo walioshika mimba bila kupenda. Hii ina maana kwamba kila binadamu asiye na hitilafu ya

Vipi kuhusu mahausigeli?

Hapa nchini, hivi sasa karibu kila nyumba inamiliki mtumishi wa ndani anayejulikana kama hausigeli. Mahausigeli wamekuwa fasheni manyumbani mwetu. Bila hausigeli inaonekana kama vile haijatulia. Mwidimi Ndosi anawaona watumishi hawa kama watumwa. Mahausigeli wengi ni wasichana waliokata tamaa ya maisha. Ni mabinti walioonja machungu ya makali ya maisha vijijini kwao na hivyo kuuzwa utumwani na wazazi wao wenyewe. Wengine ni wasichana walioikosa shule, japo waliipenda shule. Kisa? Kuna wanaume wakora waliutumia umasikini wa wazazi wao kuwadanganya na kulazimisha mahusiano nao, mahusiano ambayo huhitimika ghalfa pale inapoonekana kwamba yametengenza kiumbe tumboni mwa binti. Matokeo yake, binti ndiye hufukuzwa nyumbani eti kwa kosa la kuiaibisha familia. Shule inakuwa ndio basi. Mwenye mimba anakana mashitaka ya kuhusika na kiumbe hicho. Nyumbani inakuwa polisi. Binti anakosa kimbilio kati ya watu wake mwenyewe isipokuwa kupotelea mjini. Matukio kama haya ya kinyama ndiyo hasa yamesabab

Tabia zetu zimekosewa

Juma lililopita tulijaribu kuona athari za malezi katika ujenzi wa tabia zetu. Tuliona namna ambavyo matendo yanayofanywa na wazazi wetu kwa kujua kwao ama kutokujua kwao, yanatusababisha tuwe hivi tulivyo. Tukasema kuwa tulivyo, ni matokeo ya walivyo/walivyokuwa wazazi wazazi wetu. Leo ningependa tuangalie ukweli mmoja kuwa asilimia kubwa ya watu unaowaona barabarani, unaofanya nao kazi, unaosoma nao na pengine wewe mwenyewe, wamekosewa. Kukosewa ninakokuzungumzia hapa ni katika ujenzi wa tabia ama haiba yetu. Sina neno zuri kushika nafasi ya “Personality”. (Pengine Mwalimu wangu Makene atanisaidia) Kila binadamu anayo haiba/tabia yake—yaani namna anavyofikiri, anavyojisikia, anavyofanya mambo yake, anavyovaa, anavyoonekana na vilevile anavyohusiana na watu wanaomzunguka. Makosa ya tabia zetu yanahusisha matendo ambayo yanakinzana na iliyokawaida ya utamaduni wetu na matarajio ya wanaotuzunguka. Hata hivyo si kila afanye kivyume na matarajio ya watu ana kilema cha tabia. Na wala ha