Ukifikiri Upendo ni Vitu Utamkinai Anayekupenda

Juzi naongea na kijana mmoja, umri nakadiria kavuka miaka thelathini, ananiambia ameanza kuhisi kama vile hakuumbiwa mapenzi. Ukisikia mtu anatoa kauli nzito hivi ujue kuna jambo. Kudodosa, kumbe, kayapambania mapenzi na yamekaribia kumtoa roho. Kila anayempenda kwa dhati anaishia kumwacha hewani. Haelewi afanye nini. “Hawa wanawake wanataka nini?” Kaniuliza. Tuliongea mengi. Naomba nikushirikishe, japo kwa muhtasari, maudhui ya mazungumzo yetu. Picha: Tony Cordoza | Getty Images Tumeanza kuwa na kizazi cha vijana werevu, watafutaji, wenye uwezo mkubwa wa kutafuta pesa lakini wenye hisia kificho, wasiojali hisia na wasio na haja ya kina cha mahusiano. Hiki ni kizazi, aghalabu, kilichozaliwa na kizazi cha wazazi wasomi, wenye maarifa zaidi na pesa zaidi kuliko kizazi kilichopita. Tunatumia muda mwingi kazini, kwenye biashara, na shughuli nyingine za kutafuta vitu. Ukiangalia kwa haraka unaona hiki ni kizazi chenye watu wenye kazi ...