Changamoto za kuwanyima watoto kufurahia utoto wao

Tunaishi kwenye dunia inayopitia mabadiliko mengi. Mabadiliko haya ya kijamii na kiuchumi, kwa kiasi kikubwa, yamezidisha matarajio tuliyonayo kwa maisha. Ukiacha matarajio mengi tuliyonayo kwetu binafsi, kuna matarajio mengi hata kwa wenzi wetu. Mke, kwa mfano, anatarajia mume awe kila kitu anachokifahamu kuhusu mwanamume. Mume ana kazi ya kuwa mcha Mungu, mtu wa sala, mtafutaji na mchapa kazi hodari, mcheshi, rafiki msikivu, kiongozi bora, baba mzuri na mume mzuri asiyechelewa kurudi nyumbani. Matarajio haya makubwa yana faida zake lakini pia yana upande wa pili unaochanga migogoro mingi katika familia. PICHA: Wikimedia Commons Hatuishii kuwa na matarajio makubwa kwa wenza wetu. Tunazidisha pia matarajio kwa watoto wetu kiasi cha kuwanyima fursa ya kufurahia utoto wao. Hebu fikiria mtoto asiyeruhusiwa kufanya makosa. Kila analojaribu kufanya, anapodadisi mazingira yake, anakuwa anatafsirika kama mtoto asiye na nidhamu na adabu kwa wa...