Kuwa mwenye furaha ni uamuzi wako mwenyewe!
Ni mara ngapi umewahi kukutana na mtu aliyekukwaza kiasi cha kumtupa katika kapu la “watu wa hovyo” wasiostahili heshima kama binadamu? Umewahi kupatwa na tukio ambalo lilibadili kabisa mtazamo wako kuhusu maisha, watu na maisha kwa ujumla? Kwa nini watu kukata tamaa? Umewahi kuwaza kwa nini kinachomkwaza huyu si lazima kimkwaze yule? Umewahi kuonana na mtu anayeshangaa inakuwaje “huyu bwana achukue uamuzi wa ajabu namna ile” wakati kilichotokea kinachukuliwa na wengi kuwa “ni jambo la kawaida”? Natamani ukimaliza kusoma hapa uelewe kwamba sehemu kubwa ya matatizo tunayokabiliana nayo kama binadamu kila siku, tunayasababisha wenyewe. Na kwa yale tusiyo naudhibiti nayo, tunaweza kubadili mtazamo wetu kwayo, na hilo linaloonekana kuwa tatizo ama likawa si tatizo au likabadilika kuwa changamoto. Wengi wetu tunapokumbana na vikwazo (ambavyo mara nyingi huwa ni watu, vile mambo yalivyo na matukio yanayokuwa katika namna tusiyoitegemea) hujenga mawazo kwamba vitu hivyo vi vibaya. Mato