tag:blogger.com,1999:blog-15356729.post3823908213720743816..comments2024-03-28T11:26:49.642+03:00Comments on Jielewe: Kipimo cha Kujitambua ni Tunavyowatendea Tusiowajua, WasioheshimikaChristian Bwayahttp://www.blogger.com/profile/13141394805539015266noreply@blogger.comBlogger2125tag:blogger.com,1999:blog-15356729.post-18702471077243986222016-08-23T21:49:10.836+03:002016-08-23T21:49:10.836+03:00Ndugu Maranya, asante sana kwa maoni yako makini. ...Ndugu Maranya, asante sana kwa maoni yako makini. Naamini wasomaji wa blogu hii watajifunza kwa uliyoyaandika pia.

Ni kweli kama unavyosema, hukumu ya kwa nini tunatenda tuyafanyayo inategemea sana na namna mwonesha tabia anavyohusiana na mwoneshwa. Msingi wa hoja ya makala haya ni kwamba tabia halisi ni zile tunazozionesha kwa wale tusiowachukulia kwa uzito katika maisha yetu na hivyo hatulazimiki kujenga taswira chanya kwao.

Nadhani utani wa kirafiki ni suala tofauti kidogo na linahitaji mjadala unaojitegemea. Hata hivyo, ni kweli kwamba huwa hatutaniani na kila mtu. Na tunapotaniana mara nyingi malengo yetu huwa si kujenga taswira fulani chanya kwa tunayetaniana naye. Kwa hiyo, ni vigumu maudhui ya makala haya kujibu suala hili ipasavyo. Christian Bwayahttps://www.blogger.com/profile/13141394805539015266noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-15356729.post-43894123443346331522016-08-23T21:31:03.922+03:002016-08-23T21:31:03.922+03:00Ndg Bwaya, kwanza nikupongeze kwa makala nzuri, bi...Ndg Bwaya, kwanza nikupongeze kwa makala nzuri, bila shaka wengi watajifunza kupitia makala hii kama nilivyojifunza mimi.

Binafsi nina maoni ya ziada juu ya badiliko la tabia kwa watu mbali mbali kulingana na mazingira. Tabia tofauti kwa watu (mazingira) tofauti yaweza kusababishwa na mambo mengi. Jambo la kwanza ni kama ulivyolieleza kwa kina katika makala hii.

Jambo la pili ni kuwa inategemea na mahusiano baina ya muonyesha tabia na muonyeshwa tabia. Mfano, kama tumezoea kutaniana, basi kila tunapokutana tabia ya kutaniana haiwi mbali. Habari Njema ni kwamba, wawili hao kwa muda wote watakaokuwa pamoja wanajua ni wapi walitania na ni wapi walimaanisha walichokifanya ama kusema.

Lakini kama mahusiano yetu hayako katika mazingira ya kutaniana, utategemea mawasiliano ya mwelekeo huo. Hii ni kusema kwamba, mara nyingine tunaweza kutoa hukumu isiostahili juu ya tabia za watu kama "hukumu" yetu haikuzingatia muktadha wa mawasiliano yao.

Maranya O'MayengoAnonymoushttps://www.blogger.com/profile/15228322429471199237noreply@blogger.com