tag:blogger.com,1999:blog-15356729.post114260595126228754..comments2024-03-28T11:26:49.642+03:00Comments on Jielewe: Elimu sio cheti na cheti sio elimuChristian Bwayahttp://www.blogger.com/profile/13141394805539015266noreply@blogger.comBlogger10125tag:blogger.com,1999:blog-15356729.post-1144003959972223422006-04-02T21:52:00.000+03:002006-04-02T21:52:00.000+03:00Usomi ni mojawepo ya uwekezaji mtaji. Kama wanavyo...Usomi ni mojawepo ya uwekezaji mtaji. Kama wanavyowekeza wafanyibiashara, wasomi nao wanawekeza katika elimu. Katika mataifa ya Afrika swala la maarifa haliji kwanza. Linalotangulia ni jinsi ambavyo mtu atakuwa na ukiritimba katika eneo fulani utakaompa ugali wa kila siku.

David Kyeu, mwalimu mwenzako mkenyaAnonymousnoreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-15356729.post-1143754391793623142006-03-31T00:33:00.000+03:002006-03-31T00:33:00.000+03:00Bwaya, nitajibu hoja zako kwenye ile makala kuhusu...Bwaya, nitajibu hoja zako kwenye ile makala kuhusu dini.Anonymousnoreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-15356729.post-1143754350047837232006-03-31T00:32:00.000+03:002006-03-31T00:32:00.000+03:00Freire aliamini kuwa elimu ni ile inayoweza kuweze...Freire aliamini kuwa elimu ni ile inayoweza kuwezesha wale watu Fanon aliwaita "waliolaaniwa." Hakuone umuhimu wa elimu inayoandaa watu ili wakaajiriwe wapate mshahara bila kuweza kubadili jamii inayowazunguka.

Kuna chuo India kinaongozwa na Bunker Roy kinaitwa Barefoot College. Moja ya kanuni za chuo hiki ni kuwa ukimaliza masomo hupewi cheti. Chuo hiki nia yake ni kuendeleza maisha vijijini, unapompa "msoni" cheti unampa tikiti ya kuhama vijijini kwenda mijini!Anonymousnoreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-15356729.post-1143399620616943142006-03-26T22:00:00.000+03:002006-03-26T22:00:00.000+03:00Nimekutana na maaandiko ya Mwanafalsafa mmoja wa K...Nimekutana na maaandiko ya Mwanafalsafa mmoja wa Kibrazil, Paul Freire aliyeamini kuwa katika jamii ya kijangili, elimu hutumika na wachache (bourgeoiseie)kama chombo cha kinyonyaji cha kuwakandamiza wananchi wasionacho ambao ndio wengi kimsingi.
Ukandamizajai huu unaanzia katika utoaji wa makaratasi ya vyeti eti ndio uthibitisho kuwa fulani kaelimika.
Hili ni tatizo ambalo linatupeleka pabaya. Turejee wosia wa Makene ule wa mwaka mpya. Tujisomee.
Msangi, unapimaje "kwenda darasani" na "kupitia" hapa na pale?Christian Bwayahttps://www.blogger.com/profile/13141394805539015266noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-15356729.post-1143385057704643632006-03-26T17:57:00.000+03:002006-03-26T17:57:00.000+03:00Elimu ndio ufunguo wa maisha. Ufunguo unaoweza kuf...Elimu ndio ufunguo wa maisha. Ufunguo unaoweza kufunga au kufungua kulingana na matumizi. Elimu ya kupitia shule hii na ile inayotunikiwa cheti imetusaidiaje kujikomboa? Jibu ni kwamba tumebaki kujisifu kuwa tumekanyaga madarasa wakati "madarasa" hayo hayajatusaidia katika kuwakomboa watu wetu. Elimu imetufungia nje. Imetufanya watumwa.
Wapo watu ambao elimu ya cheti iliwashinda lakini ndio walioleta mageuzi katika dunia ya leo. Watu kama akina Isaac Newton, Faraday na wengine. Hawakuwa na cheti lakini mambo yao yanawatambulisha kuliko hata vyeti kama wangevipewa.
Binafsi, sifikiri kama kuingia ama kutoka mahali (iwe chuo sijui shule na nini) kutatusaidia sana. Maana inawezekana kabisa hata usiingie kokote lakini bado ukawa na nafasi kubwa ya kutoa mchango wako kwa jamii.
Ukifuatilia watu walioingia hapa na pale unakuta wameharibikiwa tu maana wanajijengea tabaka lao tofauti na wananchi wa kawaida ambao ndio wengi. Hasara tupu, ndio matokeo.Christian Bwayahttps://www.blogger.com/profile/13141394805539015266noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-15356729.post-1143212861028636552006-03-24T18:07:00.000+03:002006-03-24T18:07:00.000+03:00kuna tofauti kubwa baina ya KUPITA na kKUINGIA mah...kuna tofauti kubwa baina ya KUPITA na kKUINGIA mahala fulani, na pengine hili ndilo linalowafanya baadhi ya watu kuamini kuwa wao ndio waliosoma sana huku wengine wakiwa katika daraja la UPE.(sijataja mtu mie, atakayejishuku shauri yale)

Kama tungeliweza kujua tofauti ya maneno hayo kikamilifu, bilashaka hali isingelikuwa mbaya kwa kiwango hiki cha sasa, ambapo wengi wetu tunaamini kuwa tumesoma, kumbe hatukusoma wala nini, kwa maana HATUKUINGIA madarasani, bali TULIPITIA katika shule fulani fulani tuRama Msangihttps://www.blogger.com/profile/08286872896038150882noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-15356729.post-1143212648285899122006-03-24T18:04:00.000+03:002006-03-24T18:04:00.000+03:00Kama tutaweza kutofautisha maana ya maneno 'KUINGI...Kama tutaweza kutofautisha maana ya maneno 'KUINGIA' na 'KUTOKA' mahali, bilashaka hapo patakuwa msingi mzuri wa kubadilishia masuala yetu yaliyoharibika zamaaaani sana. Wakati wengi wetu tunaamini kuwa tumesoma, ukweli ni kuwa hatukusoma kwa maana hatukuingia madarasani bali tulipitia shule fulani fulani tuRama Msangihttps://www.blogger.com/profile/08286872896038150882noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-15356729.post-1143018943767239962006-03-22T12:15:00.000+03:002006-03-22T12:15:00.000+03:00Ehuu! Kupumua huko ni kwa sababu mbili mosi ni kum...Ehuu! Kupumua huko ni kwa sababu mbili mosi ni kumaliza kusoma makala hii. Pili ni kupatikana tena kwa ndugu Bwaya. Sio katika viunga vingine bali cha kwake mwenyewe, maana kungine huja mara apatapo wasaa.

Kubwa ni hoja yako. Haya masuala unayoleta ndio mwale unaoonyesha tafsiri halisi ya elimu. Makene amesahau hili lakini analifahamu vema kuwa "Elimu ni kile kinachosalia baada ya kujifunza." Mie naongezea kidogo kuwa masalio hayo yaonyeshe mafanikio yanayoonekana katika jamii husika.

Nikija kwenye vyeti naona wengi wetu tunavitamani kwani ni hirizi ya kupata kazi kama alivyowahi kusema-ga Mtakatifu Nyerere wakati fulani. Ukishapata kazi tu basi waweza hata kukitia moto endapo hutarajii kuhama katika kazi hiyo. Kinachotufanya wengi wetu tunga'ng'anie kumiliki rundo la astashahada,shahada, shahada ya uzamili na ile ya udaktari ni kupata kazi ambayo mtu mwingine aliibuni. Mara chache huwa tuna mtazamo wa kubuni kazi zetu wenyewe kutokana na taaluma zetu. Hili limeshadidiwa sana na waajiri ambao hutaka alama za juu, na sio ushahidi wa ufanisi wa kutukuka. Kwa mtindo huu nani atataka cheti cha chini, achilia mbali kutokihitaji kabisa.

Pengine nimalizie na rai kuwa kwa kuwa utamaduni wa kupeana vyeti umeanza dahali nyingi tu basi ni vema sasa shinikizo liwe katika ushindani wa nani anajua zaidi na sio nani kafaulu zaidi. Mfano mdogo ni kuwa ughaibuni wakikwita kwenye usaili ni hatua ya mwanzo tena ndogo tu. Shughuli utaiona kwenye usaili ambao mosi utataka kudhihirisha yale uliyoyasoma lakini la muhimu ni kutaka kujua ufahamu wako hata wa mambo mengine, pengine katu hukuyadhania. Hapo ndipo wengi wetu tunapigwa bao. Sio nchini kwetu ambako msaili anakuuliza mulemule ambamo umesoma na ukimjibu vema basi kazi umepata.

Alamsik Binuur.John Mwaipopohttps://www.blogger.com/profile/11708584279197669683noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-15356729.post-1142689894910662892006-03-18T16:51:00.000+03:002006-03-18T16:51:00.000+03:00Na mimi nikunukuu; "Tutafika, cheza karata yako".Na mimi nikunukuu; "Tutafika, cheza karata yako".Christian Bwayahttps://www.blogger.com/profile/13141394805539015266noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-15356729.post-1142613737257940612006-03-17T19:42:00.000+03:002006-03-17T19:42:00.000+03:00Bwaya kuna kazi na hasa sasa Tanzania. Kama utakum...Bwaya kuna kazi na hasa sasa Tanzania. Kama utakumbuka salamu zangu za mwaka mpya zilijikita katika kauli hii ya kuhamasisha watu kusoma. Kusoma kumekufa kila mtu anasaka cheti. Sidanganyi kama tunataka kusoma kwa misingi ya vyeti subiri utatazama taifa letu litakavyozidi kutawaliwa na wageni. Tutabinafsisha hata madaraka ya kisiasa maana hatutakuwa na uwezo wa kupanga mambo. Lakini kifanyike nini, mabadiliko yanaanza na wewe kuchukia hali hii na kupigana kusaka maarifa yatakayosaidia kuendesha maisha yako. John Kerry alikuwa akisema, "Najua tunaweza kufanya vema" mwisho wa nukuu na tafsiri ni yangu. Nyerere aliwahi kusema, "Inawezekana, timiza nafasi yako." na mimi nijinukuu sasa, "tutafika, cheza karata yako."boniphacehttps://www.blogger.com/profile/15745336472193470752noreply@blogger.com