Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai, 2009

Kumradhi wadau...

Sitakuwepo kwa siku mbili tatu sita kumi hivi, kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu. Nimefanya hivi nikiamini si vibaya kupeana taarifa. Mpaka hapo nitakaporejea, Amani kwenu nyote!

Soma maoni marefu ya Silas Jeremia

Msomaji aliyejitambulisha kama Silas Jeremia amenitumia waraka mrefu kupitia barua pepe leo. Aliniandikia SMS akiniarifu kuwa ameshindwa kuweka maoni yake kwenye blogu (Nadhani ni kwa sababu mchango wenyewe ulikuwa mrefu kuzidi kiasi cha meneno yanayoruhusiwa kuwa maoni kwenye blogger.) Nami nikamwelekeza kutumia barua pepe ambayo ni njia rahisi kwake. Kwa kuheshimu mchango wake, kama wasomaji wengine, nimeona ni vyema niu –paste mchango wake hapa kusudi upate hadhira inayohusika kwa majadiliano zaidi: " Naomba kutoa maoni yangu kujibu hoja za upotoshaji zilizoletwa na msomaji wako. Kwanza kama yeye alivyojitambulisha kwa hoja zake kuwa ni Mwislamu, mimi ni Mkristo. Nitajibu hoja zake moja baada ya nyingine ili aelewe kama atakuwa tayari. 1. Walioendesha biashara ya utumwa walikuwa Waarabu wa kiislamu. Hawa walikuja Afrika mashariki kufanya biashara mbaya kabisa ya utumwa na kueneza dini yao. Watumwa walisombwa kutoka Afrika kwenda Uarabuni mahali panaposadikika kuwa chan

Global Voices: Dunia inaongea, unasikiliza?

Picha
Nimeamua kukata shauri na kujiunga na Jamii ya wanablogu wa Global Voices katika ukurasa wa Kiswahili . Ninajitolea kuusogeza ujumbe karibu na wasomaji wa kiswahili kwa kutafsiri makala zinazoandikwa na wanablogu wengine. Global Voices kimsingi ni jamii ya wanablogu kama 200 waliopo duniani kote ambao wanafanya kazi kwa pamoja kukuletea tafsiri na ripoti za yanayojiri kwenye ulimwengu wa blogu na uandishi wa kiraia. Global voices inapaza sauti ambazo kwa kawaida huwa hazisikiki katika vyombo vya habari vya kimataifa. Bonyeza hapa kusoma zaidi kuhusu jamii hiyo, halafu ukaribie kuchangia maoni kwenye ukurasa huo wa Kiswahili na kubadilishana mawazo na wanablogu wengine. Ndesanjo Macha , mtu aliyefanya kazi kubwa kutangaza teknolojia ya blogu kwa lugha ya kiswahili nchini na mmoja wa wahariri waandamizi wa Jamii hiyo, alikuwa na na haya ya kusema.

Soma maoni ya msomaji: Uislamu ulikuwepo tangu mwanzo

Namshukuru msomaji(ambaye hakutaja jina lake) kutupa maoni yake kuhusu hoja ya lini hasa Uislamu ulianza . Ikumbukwe, lengo hasa ni kujadiliana na si mabishano kama baadhi ya wasomaji walivyofikiri (Poleni nyote mliolalamika kwa SMS na e-mail). Hapa ni majibu ya msomaji huyo katika suala hilo: "...Salamu(amani) juu yenu. Naomba watu wafahamu ya kuwa uislamu si dini iliyopewa jina na muasisi fulani na kusema kuwa wafuasi wake waitwe waislamu, la hasha, bali Uislamu jina hili ukilitafsiri kwa lugha ya kiswahili ni amani, kujisalimisha, kunyenyekea ndiyo maana yake. Mtume Muhammad (S.A.W) si muanzilishi wa dini hii, na emeeleza wazi kuwa uislamu upo yaani (kujisalimisha kwa Mungu) toka kuumbwa kwa ulimwengu. Allah aliumba ulimwengu ili vitu vyote vimtii na kujisalimisha kwake, lakini viumbe hawa wawili (majini na watu) walipewa khiari na matamanio, na huo ndiyo mtihani wenyewe tulioumbiwa nao, ambao watu tunaelekezana, kuelimishana, kujadiliana, kuzozana mpaka tunafikia hata ku

Nini hukifanya kitabu kuwa kitakatifu?

Picha
Niliyapenda maswali ya mwanazuoni Kamala . Sijayajibu, nikisubiri wengine wayajibu kwa haki. Ninaandika kinachotoka moyoni na nimekitafakari muda mrefu. Ninahitaji kuuelewa 'utakatifu' wa vitabu fulani tunavyoviogopa. (picha kwa hisani ya 3.bp.blogspot.com) Vinaongoza 'ushabiki' wetu kidini, na vinafikirika kuwa mamlaka ya ufahamu wetu. Tukiwa wakweli, vitabu hivi viliandikwa na watu. Hata kama wengine walidai kuwa 'mabomba' ya ujumbe kutoka kwa Mungu, lakini walikuwa watu. Tafsiri 'sahihi' ya vitabu hivi inahitaji imani. Akikisoma asiye na imani, anapata ujumbe tofauti na yule mwenye 'imani.' Sentensi zinazoeleweka, zinapindwa-pindwa kukidhi mukhtadha wa kiimani. Ningependa kujua hasa, vipo vitabu vingapi vitakatifu? Utakatifu wa kitabu unatokea wapi na ni nani mwamuzi wa utakatifu huu? Je, kitabu kitakatifu hakiwezi kusomwa bila uumini na kikaeleweka vizuri zaidi? Je, kitabu kitakatifu ni kweli tupu?

Blogu zetu na uhuru wa maoni

Blogu ni nyezo ya kuuwezesha uandishi wa raia. Kutupa fursa ya kupaza sauti zetu bila masharti. Vyombo vya kizamani vya habari havitupi fursa hii. Mengi ya yanayotangazwa na kuandikwa ni yale anayoyataka mmiliki ama Mhariri. Wasomaji, wasikilizaji ama watazamaji hubaki na haki ya 'kumeza' kilichoandaliwa. Na hata maoni yao yanapoletwa, kazi kubwa huwa ni kuyaminya yalingane na msimamo wa mmiliki ama mhariri. Jambo hili ni tofauti katika blogu. Huku, msingi mkuu ni majadiliano. Anayeandika, hufanya hivyo akialika mawazo ya wasomaji yanayoweza kuwa bora kuliko yake. Kwa hivyo, nimwombe msomaji wangu mmoja anayeficha jina lake kuutumia huru huu, kusema kile anachodhani ni sahihi kwa njia yoyote anayoona inafaa lakini sio kujaribu kusitisha mijalada inayomkwaza. Vilevile, si lazima sana kuficha jina. Kama una uhakika na unachosema, kwa nini ujifiche kwenye kichaka cha majina bandia?

Dini ni ajali ya kuzaliwa

Wengi wetu hatukuchagua kufuata dini tulizonazo. Tumejikuta tunarithi dini za wazazi ambazo leo tunatoana nundu kuzitetea. Tumezivaa dini bila maamuzi na tumezishikilia utafikiri tunazijua. Na ajabu tunaamini kuwa dini nyingine zilizobaki kuwa haziko sahihi wakati kama tungezaliwa na wazazi wengine pengine ndizo zingekuwa zetu! Mkristo (ambaye ni mrithi wa dini ya baba yake) anaamini dini zote zilizobaki zimekosea. Mwislam naye (ambaye kajikuta mwislam kwa kuzaliwa) anaamini wote waliobaki ni 'makafri.' Kinachosikitisha ni kwamba tumejengewa uzio wa kutuzuia kujifunza dini za wenzetu. Na tunapojifunza dini hizo, kimsingi hutafuta kasoro na mapungufu yatakayotupa kuridhika kuwa dini zetu ndizo sahihi. Tungelijua kuwa dini ni ajali, basi ikiwa ni lazima, tungezipitia zote ili kuchagua moja au mbili. Vinginevyo tunabaki vipofu jeuri wanaojua kuelezea mkia wakidhani ndiye tembo.

Uislamu ulianza lini?

Picha
YAMEKUWEPO madai kwamba Uislam ulianza tangu kuumbwa kwa dunia. Na wapo watu wanaotuaminisha hayo. Ukweli ni kwamba Uislam ulianzishwa na Nabii Muhammad mwaka 622 BK huko Arabia. Kabla yake, dini zilizokuwepo zilikuwa ni Uyuda ambayo ni dini rasmi ya Wayahudi (Judaism) na Ukristo ambayo ni dini ya mataifa wasio Wayahudi ulioanza miaka kadhaa baada ya Yesu kuwa ameondoka mwaka 33BK. Yesu mwenyewe hakuanzisha Ukristo. Alisali katika misikiti ya Wayahudi. Masinagogi. Maelezo haya yana msingi wa kistoria na sio propaganda za kidini. Ndio ni propaganda kwa sababu dini zote zimekuwa na tabia ya kuonyesha kwamba zenyewe ndizo za kweli kuliko dini nyinginezo hata ikibidi kwa kuichezea historia. Na ni bahati mbaya kwamba Dini zimekuwa na tabia ya kufanana ya kuzima uwezo wa waumini wake kuhoji lolote kwa kuwajengea hofu ya kujitafutia laana. Qur’an inatupa maelezo yanayokinzana kuhusu lini hasa Uislamu ulianza. Baadhi ya mistari katika kitabu hicho zinadai kwamba ‘nabii’ Muhammad ndiye

Kulikoni mambo ya dini

Picha
Ule mjadala hatujauhitimisha. Kama unayo maoni unaweza kuyaacha pale. Kwa sasa ningependa kudurusu baadhi ya mambo yaliyojitokeza kwenye mjadala ule ambao ulipata maoni ya wasomaji mbalimbali. Ikumbukwe kwamba blogu zina maana hasa yanapokuwepo maoni ya wanaosoma na sio kuendeleza tu yale ya aliyeandika. Jambo la kwanza lililojitokeza katika majibizano ya wasomaji wawili walioficha majina yao, ni kuhusu historia ya Uislamu. Kwamba mmoja anadhani Uislamu ulianza tangu kuumbwa kwa Dunia, na mwingine anadhani Uislamu haukuwepo hata miaka 2000 iliyopita. Nijuavyo mimi, kabla ya miaka 2000 iliyopita, haukuwepo Ukristo wala Uislamu. Hizi zote ni dini za juzi juzi. Dini iliyokuwepo enzi hizo katika nchi hizo tunazoiita takatifu ilikuwa ni Judaism. Dini isiyo na uhusiano wa moja kwa moja na Uslamu wala Ukristo. Ibrahimu anayetajwa na msomaji mojawapo kuwa na mila ya dini mojawapo, alikuwa na mila na utamaduni wa Kiyahudi mwenye dini ya Uyuda (Judaism). Maana ya historia hii ni ni

Nimeikumbuka hii hapa...

Picha
Nimekuwa nikiamini kuwa tofauti ya mawazo ndiyo msingi wa majadiliano. Tofauti hizi ni pamoja na mitazamo na uelewa, namna tunavyo'react' tukiguswa kwenye maeneo tunadhani hayajadiliki, namna tunavyoheshimu mawazo ya wasemaji wengine wanaoamini tofauti na sisi, namna tunavyoweza kuvumiliana na bado tukajadiliana (hata kama inakuwa kama vurugu fulani vile) lakini mwishowe mnajifunza: Hakuna anayejua. Wote mnahitaji kujifunza kwa wengine. Nimefurahi kusoma maoni ya mchangiaji aliyeamua kujificha kwenye kichaka cha jina la 'Natiakasi.' Ni bahati mbaya kwamba alidhani mimi nina chuki na dini yake anayoitetea kwa nguvu zote. Nimeona pengine itafaa nikimwonyesha chuki yangu hasa ni ipi kwa kumpeleka kwenye makala hii , niliyoiandika miaka mitatu iliyopita. Enzi hizo nilikuwa bado naandika makala ndefu ndefu (kwa sasa huwa sioni ulazima wa kurefusha ninachotaka kukisema) kwa hiyo naomba msamaha kwa makala ndefu inayochosha. Pamoja na kwamba wachangiaji wa wakati huo wen

Uislam: Ndoa na mali havihusiani?

Jana nilikuwa nikitazama kipindi cha kiislamu kwenye televisheni ya Chaneli 10. Suala la mali katika ndoa za dini hiyo lilikuwa likijadiliwa. Kwamba Kiislam, mali katika ndoa si suala la wanandoa kwa pamoja. Kwamba mali anazoingia nazo mwanandoa kwenye ndoa, zinabaki kuwa zake mwenyewe. Na wakiachana, kila mmoja anaondoka na alichokuja nacho. Hata ndani ya ndoa, mali zinapatikana 'separately' kwa maana ya kwamba kila anachopata mwanandoa hicho ni haki yake yeye mwenyewe. Wakitengana, kila mtu anaondoka na vyake. Katika kufakari hayo, nilijaribu kumfikiria mwanamke na nafasi yake katika ndoa. Nikamwona kama kiumbe anayenyanyaswa na dini. Kwa nini? Wanaume wengi hutafuta mali kwanza ndio waoe, na hata wanapooa, huwaoa wanawake watakaowategemea wao. Katika hali hii nini salama ya mwanamke katika dini inayoruhusu talaka? Hizi si dalili za wazi za ukandamizaji wa jinsia ya kike?

Kipanya na tafakuri

Picha

Mkaribishe mwanablogu mpya wa dini/imani

Picha
Naomba kufahamisha blogu mpya yenye kugusa zaidi maisha na mienendo ya watu. Baadhi ya watu watakuwa wamemsoma Mhandisi na Mwelimishaji ndugu Sabato E. Tarimo katika gazeti la MsemaKweli kwenye makala zake mbalimbali. Sasa amejikita katika ulimwengu wa blogu ili kuwafikia wengi zaidi hasa wale wanaoishi nje ya Tanzania. Bonyeza hapa kumsoma.

'Testi' ya namna unavyojithamini

Jipime. Jipe alama kwa uaminifu, ili kujielewa namna ulivyo. Mwongozo: 0=Sikubali 1=Kiasi sikubali 2=Sina jibu 3=Kiasi nakubali 4=Nakubali | Najifurahia jinsi nilivyo mf. umbo, rangi, elimu nk | Nadhani watu wananikubali nilivyo | Nikikosolewa ama kupingwa mawazo yangu huwa sipati shida | Huwa naumia nisiposifiwa pale nnapohisi nastahili kupewa sifa | Wanavyonifaham na kuniona wengine, kwangu si muhimu | Ninachofanya si muhimu, kama nilivyo mimi mwenyewe | Huwa sitegemei kukosea ninapofanya jambo | Sina hofu na mwonekano wangu mf. mavazi, sura nk | Ninajua kuukubali uwezo na udhaifu wangu | Ninajua kwa hakika nilivyo mtu wa pekee Sasa jumlisha alama zote: 0-20 fanya kazi ya ziada kujithamini na kuona thamani uliyonayo ambayo huijui. 20-30 ni nzuri. Unajiamini na kujichukulia vizuri. 31-40 maana yake unajiamini kupita kiasi. kujiamini kupita kiasi ni tatizo katika kuhusiana na watu!

Nakutakieni mapumziko mema ya juma

Poleni na majukumu mazito ya juma zima. Wafanyakazi wa ofisi zote, hongereni sana. Wanaharakati wote, hongera sana. Wanafunzi wote kaza buti. Na wasomaji wote kwa ujumla, amani iwe nanyi nyote. Naitumia wikiendi hii kudesa pale kwa Prof. Matondo. Dokta mtarajiwa Chahali katuwekea desa muhimu pale. Usikose kupepesa macho pale. Hongera sana Chahali. Nakupendeni nyote.

Tujichunguze kabla ya kumshutumu Michael Jackson

Picha
Watu wengi wanamshutumu Michael Jackson utafikiri hawafanyi alichofanya. Walipewa nywele pilipili, wanazikaanga ziwe kama za Michael Jackson. Wana vyuso nyeupee lakini miguu myeusi tii. Eti nao wanamlaani Michael Jackson. Tumekuwa vipofu. Wengi wetu hatukufikia hatua ya kuchonga pua, kwa sababu tu hatukujaliwa pesa za kufanya hivyo! Nilimwambia dada mmoja hivyo, nusura anitoe ngeu. Lakini meseji senti. Wengi wetu hatuna tofauti na mzungu Michael Jackson. Halafu tunajidai kumshambulia. Je, huu ni uungwana kweli?

Bila upendo, usihangaike kuonya!

Kuna watoto hawajawahi kujua kupendwa kukoje. Tunazungumzia watoto wenye wazazi. Watoto wanavalishwa. Wanalishwa. Wanasoma shule za 'watakatifu.' Lakini hawajawahi kujihisi kupendwa! Wazazi wanazo pesa, lakini si mapenzi kwao. Wazazi wanapendana wao (chumbani of coz), lakini hawaonyeshi mapenzi ya kweli kwa watoto wao. Na ni bahati mbaya ilioje kuwa kila mtu anahitaji kupendwa. Athari za kutokupendwa ni mbaya. Watoto wasiopendwa, ni vigumu kujielewa. Ni vigumu kujiamini. Ni vigumu kusikiliza na kushaurika. Ni wakaidi. Wagomvi. Watoto wasioujua upendo wa wazazi, huutafuta upendo huo kwa marafiki, ambao nao pia hawaujui upendo. Ni rahisi kudanganyika. Ni rahisi kuangukia mikononi mwa 'mafataki'. Kile tunachokiona kwenye tangazo la TAMWA kwamba 'sidanganyiki', bila upendo wa wazazi, ni ndoto. Kama unatumia muda mwingi kuonya wanao bila kuwaonyesha upendo, bado una kazi ya kufanya.

Zijue changamoto zinazowakabili wanao

Watoto wa sasa wanakulia katikati ya shinikizo gumu la kimaamuzi. Taarifa zilizozagaa, na zinazopatikana kirahisi ni upotoshaji. Magazeti mengi yananadi ngono na mienendo mingine ambayo kama mzazi usingependa mwanao aiige. Vipindi vya televisheni vinajaribu kuonyesha kana kwamba kusalitiana ni jambo la kawaida. Watoto wanakua wakijua ngono inafanywa na yeyote kwa wakati wowote ule. Niliwahi kusoma ushauri aliopewa kijana mmoja aliyekuwa akilalamika kujisikia hukumu kila anapofanya ngono na rafiki yake. Yule 'mshauri' akamjibu 'usijisikie hukumu...ifurahie.' (Na bado tunajiuliza kwanini watoto wengi wanapata mimba siku hizi?) Wakati huo wewe mzazi uko bize na kutafuta hela. Huna mazungumzo ya maana na mwanao. Unashauri kwa ukali na kwa kuchelewa. Sasa kama wewe huongei, na wapo wanaoongea kwa sauti, unadhani upande upi utashinda? Wa kwako? Zijue changamoto walizonazo wanao.

Naomba msaada wa lugha

Blogu zetu zinatusaidia kukuza lugha yetu ya kiswahili. Lazima tuwe wazi kuwa mara nyingine tunalazimika kutumia sentensi nzima kufafanua neno moja. Hapa nina maneno kadhaa ninayohitaji kiswahili chake. Conscious, sub-conscious, compulsion na obsession. Naomba mwenye msaada wa karibu anisaidie kupata maneno fasaha ya kiswahili. Natanguliza shukrani.

Michael Jackson na athari za malezi

Si muda mrefu nilikuwa nikitazama ibada ya maziko ya Michael Jackson. Kwa wengi, Michael ni alama ya watu wasiojikubali. Wengi wanamlaumu kwa uamuzi wake wa kujifanyia marekebisho sura yake. Wengine wakamwita 'Wacko' yaani chizi. Kama umefuatilia historia ya uhusiano wake na wazazi wake utabashiri nini kilikuwa chanzo cha yote hayo. Uhusiano wake na baba yake haukuwa mzuri. Mzee si tu kwamba alikuwa mkali sana, lakini pia alikejeli maumbile ya mwanae huyo. Nadhani yapo zaidi ya haya yasiyosemwa wazi. Maana fikiria hata wosia aliouacha Michael umeonya kuwa wazazi wake wasihusishwe na mirathi. Hata katika maziko, wazazi hawakuongea! Inasemwa, wakati Michael anaanza kujikwatua, mzee alimwonya sana pasipo mafanikio. Kisiki kwa wazazi wengi: Wanadhani kumwonya mtoto msiyehusiana nae kwa karibu, mtoto aliyekufuta akini mwake, kunasaidia...! Mzazi usifanye kosa la Mzee Joseph Jackson.

Hebu na tujilinganishe na wenzetu...

Picha
TUNAWEZA kulitazama suala la malezi kwa mtazamo mpana zaidi ya sisi binadamu. Kwa sababu sisi ni sehemu ya wanyama, basi nadhani, tunaweza kujifunza kutoka kwa "wenzetu". Wanyama wengine hawatoi ushirikiano kwa 'watoto' wao baada ya kuwazaa. Kwao, shughuli ya msingi ni kuzaa, kisha watoto huachwa wakizagaa. Kila mmoja hutawanyika kutafuta kinachoweza kumfaa kumwezesha kusogeza siku. Kwa sababu ya wepesi wa shughuli yenyewe, wanyama wengi huzaa kwa mikupuo mingi. Chukulia aina nyingi ya samaki ambao 'hulipua' maelfu ya vijisamaki kwa mkupuo huu (mmoja). Mara tu baada ya uzazi, kila samaki hujitafutia maisha yake mwenyewe. Matokeo yake wengi wao hujifilia bila taarifa. Hali ni hiyo hiyo kwa wanyama wengine wengi. Lakini jamii kubwa ya ndege imethibitika kuwa na maandalizi kabla ya uamuzi wa kuzaa. Kutengeneza kiota na kadhalika. Na hata baada ya kutotoa mayai, wengi wao wanao uwezo mzuri wa kufuatilia maendeleo ya 'vifaranga' vyao mpaka wataka

Wazazi wanaweza kukwepa lamawa?

Nilibahatika kushuhudia ugomvi mzito wa wazazi wenye hasira kali kwenye daladala. Halmanusra wamteketeze rafiki yangu. Ilivyokuwa ni kwamba konda alimporomoshea matusi ya mwilini abiria mwenzetu. Kuona vile, kila abiria alimsulubu konda kwa kosa la kushindwa kuudhibiti mdomo wake. Basi, rafiki yangu kuona vile, akawaomba wazazi wale kutokumlaumu konda, akidai kuwa kosa hasa ni la wazazi wa konda yule. Kauli ile ilileta tafrani la kutisha kiasi kwamba mashambulizi yote yalihamishiwa kwa rafiki yangu. Japo mjadala ule haukuweza kufikia tamati nzuri, lakini ulinipa tafakari. Kwamba, kwa nini wazazi walewale wanaogeuka mbogo pale malezi yao yalipohusianishwa na udhalimu wa watoto wao, hao hao hujipiga piga kifua wanapohusishwa na mafanikio ya watoto wao? Kwanini mtoto anapoharibika wazazi hukwepa kuwajibika moja kwa moja lakini watoto wanapofanya vizuri, wazazi kudai sifa kwa lazima?

Mbona hutumii kipaji chako?

Tulidokeza awali kwamba ni makosa kujaribu kutafuta tusivyonavyo, ilhali tukiviacha tulivyonavyo vikiteketea bila taarifa. Vipaji ni mojawapo ya vingi tulivyonavyo. Tunapozungumzia vipaji, tunaanisha uwezo asilia ambao tunazaliwa nao bila kujifunza. Na kila mtu ana kipaji hata kama hakijui. Inasikitisha kuwa watu wengi wanatumia maisha yao hapa duniani kujaribu kubadili vipaji walivyozaliwa navyo. Wanakana uwezo wao na kukimbilia vitu dhaifu kama sifa za bure bure, heshima kwa jamii isiyojitambua, pesa na vitu kama hivyo. Matokeo yake, wanakaanga vipaji vyao. Wanapotea njia. Wanafanya kazi zisizowapa furaha. Wanaishi maisha ya wengine. Hayo yote ni kwa kutokuvijua na kuvitumia vipaji vyao. Kwa nini tusianzie na hapa tulipo? Kwa nini tusianzie na tulivyonavyo? Na kama tulivyonavyo ni vipaji, kwa nini tusivitumie? Itaendelea...

Pa kuanzia, ni pale uliko

Ni vizuri kuanza na kile ulichonacho, na si kile usichonacho. Fursa mara zote, huwa pale ulipo na katu si kule ulipokuwaga. Suala la msingi ambalo kila mmoja anapaswa kuliweka sawa, si kile ambacho angeweza kukifanya kama angekuwa na muda, elimu na namna ya kufanya, lakini kile ambacho angepaswa kukifanya kwa kutumia vile alivyonavyo. Mara nyingi tunapuuza vile tulivyonavyo, na kupoteza nguvu nyingi kutafuta kile tusichonacho. Matokeo yake tunajikuta tunapoteza hata kile tulichonacho. Ni hivi. Yafaa sana kufanya kiwezekanacho, kwa kutumia ulichonacho, pale pale uliko. Usiozeshe ulichonacho kwa kutamani usichokuwanacho. Pengine unadhani huwezi kukitumia ulichonacho. Ukweli ni kwamba huwezi jua uwezacho mpaka kwanza ujaribu. Anzia na uliko kufikia unakotaka kwenda. Pengine hujui ulichonacho. Nikwambie? Niseme, sisemage? Itaendeleaga...

Unayatumiaje masaa ishirini na mane?

Binadamu wote ni sawa kwa maana nyingi. Usawa mmoja wapo ni kiasi cha muda ambacho kila mmoja wetu anacho. Kila binadamu anayo masaa ishirini na mane kwa siku. Masaa yaliyotimia yenye dakika sitini. Kinacholeta tofauti, ni namna tunavyoyatumia masaa haya kwa faida. Kile tunachofanya katika kila 'lisaa' linalopita mikononi mwetu. Wakati wapo wanaoweza kupangilia mgawanyo wa muda kwa siku inayofuata, na kutathimini adabu waliyo nayo kwa kile walichopanga, wengi tunajikuta tunafanya yale tusiyoyapanga na hivyo hatuna namna ya kutathmini matendo yetu ya siku. Watumiaji wazuri wa muda wanao uwezo mzuri wa kusema 'hapana sikupanga hili' wakati watumiwaji wa muda hawana uwezo huo. Ninaposhindwa kusema hapana mahala ambapo nilipaswa kufanya hivyo, ni namna bora zaidi ya kuteketeza muda. Ikiwa tutaweza kudhibiti matumizi ya muda, tutakuwa tumeweza kuyadhibiti maisha yetu.